مَا لَا يَسَعُ المُسْلِمَ جَهْلُهُ
Mambo ya Msingi ambayo haitakikani kwa Muislamu kutoyajua
اللَّجْنَةُ العِلْمِيَّةُ
بِرِئَاسَةِ الشُّؤُونِ الدِّينِيَّةِ بِالمَسْجِدِ الحَرَامِ وَالمَسْجِدِ النَّبَوِيِّ
Kamati ya Kielimu ya usimamizi wa mambo ya Dini ya Msikiti Mtukufu wa Makkah na Madinah
بِسْمِ اللهِ الرَّحمَنِ الرَّحِيمِ
Kwa jina la Mwenyezi Mungu Mwingi wa rehema Mwenye kurehemu
Utangulizi
Kila sifa njema ni za Mwenyezi Mungu Mola Mlezi wa walimwengu, na rehema na amani zimfikie yule aliyetumwa kuwa rehema kwa walimwengu, na kwa watu wake, na Maswahaba zake, na wale waliofuata mwenendo wake, na wakaongoka kwa muongozo wake, mpaka siku ya Malipo. Ama baada ya hayo:
Huu ni ujumbe mfupi, uliokusanya mambo muhimu anayoyahitaji Muislamu katika itikadi yake, ibada zake na miamala yake. Tumeyakusanya haya kwa ajili ya mwenye kutembelea Misikiti Miwili Mitukufu, mwanaume na mwanamke; ili wawe na elimu na utambuzi wa mambo ya dini yao, tukitaraji kutoka kwa Mkarimu, Mwingi wa kuneemesha awanufaishe kwa ujumbe huu, na aufanye kuwa wenye kufaa, na uwe kwa ajili ya kutaka uso wake tu. Kwani, Yeye ndiye mbora wa wenye kuombwa, na Mkarimu zaidi mwenye kutarajiwa.
Kamati ya Kielimu ya usimamizi wa Masuala ya Kidini katika Msikiti wa Makkah na Msikiti wa Mtume.
Sura ya kwanza:
Yanayohusiana na Akida (Itikadi)
Mada ya Kwanza: Maana ya Uislamu na nguzo zake:
Uislamu: Ni kujisalimisha kwa Mwenyezi Mungu kwa kumpwekesha, na kunyenyekea kwa kumtii, na kujiepusha na ushirikina na washirikina.
Na nguzo zake ni tano:
Nguzo ya kwanza: Ni kushuhudia kuwa hakuna mungu apasaye kuabudiwa kwa haki isipokuwa Mwenyezi Mungu peke yake na Muhammad ni Mtume wa Mwenyezi Mungu.
Ya pili: Kusimamisha swala.
Ya Tatu: Kutoa zaka.
Ya nne: Kufunga mwezi wa Ramadhani.
Ya tano: Kuhiji Nyumba Tukufu ya Mwenyezi Mungu, ikiwa ataweza gharama za kwenda huko.
Umuhimu wa Tauhidi:
Jua kwamba Mwenyezi Mungu Mtukufu aliumba viumbe ili wamuabudu, na wasimshirikishe na chochote. Amesema Mwenyezi Mungu Mtukufu:
﴿وَمَا خَلَقۡتُ ٱلۡجِنَّ وَٱلۡإِنسَ إِلَّا لِيَعۡبُدُونِ 56﴾
"Nami sikuwaumba majini na watu ila waniabudu Mimi." [Surat Adh-Dhariyaat: 56] Na ibada hii haiwezi kujulikana ila kwa elimu, kama alivyosema Mwenyezi Mungu Mtukufu:
﴿فَٱعۡلَمۡ أَنَّهُۥ لَآ إِلَٰهَ إِلَّا ٱللَّهُ وَٱسۡتَغۡفِرۡ لِذَنۢبِكَ وَلِلۡمُؤۡمِنِينَ وَٱلۡمُؤۡمِنَٰتِۗ وَٱللَّهُ يَعۡلَمُ مُتَقَلَّبَكُمۡ وَمَثۡوَىٰكُمۡ 19﴾
"Basi jua ya kwamba hakuna mungu ila Mwenyezi Mungu, na omba maghufira (msamaha) kwa dhambi zako na za Waumini wanaume na Waumini wanawake. Na Mwenyezi Mungu anajua mahali penu pa kwenda na kurudi, na mahali penu pa kukaa." [Muhammad: 19] Hivyo Basi akaanza na elimu kabla ya kauli na matendo. Kwa hivyo, jambo muhimu zaidi ambalo ni juu ya Muislamu kujifunza, ni kumpwekesha Mwenyezi Mungu Mtukufu (Tauhidi); kwa kuwa ndilo chimbuko la Dini na msingi wake. Dini haisimami isipokuwa kwa Tauhidi, nayo ndiyo wajibu wa kwanza kwa Muislamu, nayo ndiyo wajibu wa mwisho. Na Tauhidi ndiyo nguzo ya kwanza katika Nguzo za Uislamu ambazo ni wajibu juu ya kila Muislamu kuzijua na kuzifanyia kazi, nazo ni nguzo tano. Kama ilivyopokelewa kutoka kwa Abdallah bin Omari, radhi za Mwenyezi Mungu ziwe juu yao wote wawili, kwamba alisema: Nilimsikia Mtume wa Mwenyezi Mungu, rehema na amani za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake akisema: "Uislamu umejengwa juu ya mambo matano: Kushuhudia kwamba hakuna mungu apasaye kuabudiwa kwa haki ila Mwenyezi Mungu, na kwamba Muhammad ni Mtume wa Mwenyezi Mungu, na kusimamisha Swala, na kutoa Zaka, na kuhiji katika Nyumba Tukufu ya Mwenyezi Mungu, na kufunga Ramadhani."1
Inapasa kwa Muislamu kujifunza maana ya Tauhidi; nayo ni kumpwekesha Mwenyezi Mungu kwa ibada. Basi asishirikishwe Mwenyezi Mungu na yeyote katika ibada zake; si Malaika aliyekaribu wala Nabii aliyetumwa.
Maana ya kushuhudia kuwa "Hakuna mungu apasaye kuabudiwa kwa haki isipokuwa Mwenyezi Mungu":
Ni kwamba mja anakiri kwa itikadi thabiti isiyokuwa na shaka kwamba hakuna muabudiwa wa haki isipokuwa Mwenyezi Mungu Mtukufu. Kwa hivyo, akamuabudu Mwenyezi Mungu peke yake, na kuifanya ibada katika aina zake zote iwe mahususi kwa ajili yake Yeye aliyetakasika na kutukuka, na ibada hizo ni kama vile dua, hofu, kutaraji, kutegemea, na mengineyo.
Wala Shahada haitimii isipokuwa kwa nguzo mbili:
Ya kwanza: Kukanusha haki ya uungu na ibada kwa yeyote asiyekuwa Mwenyezi Mungu; miongoni mwa washirika wote, miungu yote na mashetani wote.
Ya pili: Kuthibitisha uungu na ibada ya haki kwa Mwenyezi Mungu peke Yake, bila kumshirikisha na yeyote mwingine. Amesema Mwenyezi Mungu Mtukufu:
﴿وَلَقَدۡ بَعَثۡنَا فِي كُلِّ أُمَّةٖ رَّسُولًا أَنِ ٱعۡبُدُواْ ٱللَّهَ وَٱجۡتَنِبُواْ ٱلطَّٰغُوتَ...﴾
"Na kwa hakika kwa kila umma tuliutumia Mtume kwamba: Muabuduni Mwenyezi Mungu, na muepukeni Shetani..." [An Nahli: 36].
Na ama masharti ya "hakuna mungu apasaye kuabudiwa kwa haki ila Mwenyezi Mungu peke yake" ni:
La kwanza: Ni Elimu inayoondoa kutojua.
La pili: Yakini inayoondoa shaka.
La tatu: Ikhlasi inayoondoa ushirikina.
La nne: Ukweli ulio kinyume na uongo.
La tano: Mapenzi yanayoondoa chuki.
La sita: Utiifu unaopingana na ukaidi.
La saba: Kukubali ambako ni kinyume cha kukataa.
La nane: Ni kukufuru yote yanayoabudiwa kinyume na Mwenyezi Mungu Mtukufu.
Masharti haya ni lazima yafanyiwe kazi, na yame kusanywa katika beti mbili zifuatazo:
Elimu, yakini, ikhlasi na ukweli wako, pamoja na upendo, utiifu na kuyakubali
Na lilizidishwa la nane ambalo ni kukufuru kwako vitu vyote viabudiwavyo visivyokuwa Mwenyezi Mungu
Na kutekeleza shahada sawasawa kunakuwa kwa kumuabudu Mwenyezi Mungu Mtukufu peke yake hana mshirika wake, na kuitakasa ibada kwa ajili ya Mwenyezi Mungu peke yake. Basi haifai kumuomba isipokuwa Mwenyezi Mungu, na wala kutegemea isipokuwa kwa Mwenyezi Mungu, na wala kutaraji isipokuwa kwa Mwenyezi Mungu, na wala kusali isipokuwa kwa ajili ya Mwenyezi Mungu, na wala kuchinja isipokuwa kwa ajili ya Mwenyezi Mungu -ametakasika na ametukuka.
Basi yale yanayofanywa na baadhi ya watu ya kutufu (kuzunguka) makaburi, na kutafuta kuokolewa kutoka kwa waliomo makaburini na kuwaomba wasio kuwa Mwenyezi Mungu, hayo yote ni kumshirikisha Mwenyezi Mungu katika ibada. Basi ni lazima tujihadhari na hilo na kuonya dhidi yake; kwani hili ni katika aina ya yale yanayofanywa na washirikina ya kuabudu masanamu, mawe na miti kinyume na Mwenyezi Mungu Mtukufu. Na huu ndio ushirikina ambao Mwenyezi Mungu aliteremsha Vitabu na akawatuma Mitume ili kutahadharisha dhidi yake na kuukataza.
Maana ya kushuhudia kuwa Muhammadi ni Mtume wa Mwenyezi Mungu:
Ni kumtii katika yale aliyo yaamrisha, na kumsadikisha katika yale aliyo yaeleza, na kujiepusha na yale aliyo yakataza na kuyakemea, na asiabudiwe Mwenyezi Mungu isipokuwa kwa namna alivyoelekeza. Basi Muislamu anapaswa kukiri kwamba Muhammad bin Abdullah Al-Qurashi Al-Hashimi ni Mtume wa Mwenyezi Mungu Mtukufu kwa viumbe wote; majini na wanadamu. Kama alivyosema Mwenyezi Mungu Mtukufu:
﴿قُلۡ يَٰٓأَيُّهَا ٱلنَّاسُ إِنِّي رَسُولُ ٱللَّهِ إِلَيۡكُمۡ جَمِيعًا...﴾
"Sema: Enyi watu! Hakika mimi ni Mtume kwenu nyinyi nyote..." [Al-A'raaf: 158]
Na kwamba Mwenyezi Mungu alimtuma ili afikishe Dini yake na kuwaongoza waja wake. Kama alivyosema Mwenyezi Mungu Mtukufu:
﴿وَمَآ أَرۡسَلۡنَٰكَ إِلَّا كَآفَّةٗ لِّلنَّاسِ بَشِيرٗا وَنَذِيرٗا وَلَٰكِنَّ أَكۡثَرَ ٱلنَّاسِ لَا يَعۡلَمُونَ 28﴾
"Na hatukukutuma ila kwa watu wote, uwe mbashiri, na muonyaji. Lakini watu wengi hawajui." [Saba: 28] Na kama alivyosema Allah Mtukufu:
﴿وَمَآ أَرۡسَلۡنَٰكَ إِلَّا رَحۡمَةٗ لِّلۡعَٰلَمِينَ 107﴾
"Nasi hatukukutuma ila uwe ni Rehema kwa walimwengu wote." [Al Anbiyaai: 107].
Na matakwa ya shahada hii ni: Usiamini kwamba Mtume wa Mwenyezi Mungu, rehema na amani ziwe juu yake, ana haki yoyote katika Umola na kupangilia mambo ya ulimwengu, au haki yoyote ya kuabudiwa, bali bwana Mtume -rehema na amani ziwe juu yake- ni mja tu wala haabudiwi, na ni Mtume asiye kadhibishwa, wala hamiliki juu ya nafsi yake wala kwa mwingine chochote katika manufaa wala madhara, ila apendavyo Mwenyezi Mungu. kama alivyosema Allah Mtukufu:
﴿قُل لَّآ أَقُولُ لَكُمۡ عِندِي خَزَآئِنُ ٱللَّهِ وَلَآ أَعۡلَمُ ٱلۡغَيۡبَ وَلَآ أَقُولُ لَكُمۡ إِنِّي مَلَكٌۖ إِنۡ أَتَّبِعُ إِلَّا مَا يُوحَىٰٓ إِلَيَّ...﴾
"Sema: Mimi sikwambiini kuwa ninazo hazina za Mwenyezi Mungu. Wala sijui mambo yaliyofichikana. Wala sikwambiini kuwa mimi ni Malaika. Mimi sifuati ila yanayofunuliwa kwangu..." [Al-An'am: 50].
Sehemu ya 2: Maana ya Imani na Nguzo zake:
Imani: Ni kuitakidi kwa moyo, na kutamka kwa ulimi, na kutenda kwa moyo na kwa viungo, inazidi kwa kutii, na inapungua kwa kufanya maasi.
Imani ni sharti la usahihi na kukubaliwa kwa ibada zote. Kama vile ushirikina na ukafiri huharibu ibada zote, kama ambavyo Mwenyezi Mungu haikubali swala pasina udhu, pia haikubali ibada pasina imani. Amesema Mwenyezi Mungu Mtukufu:
﴿وَمَن يَعۡمَلۡ مِنَ ٱلصَّٰلِحَٰتِ مِن ذَكَرٍ أَوۡ أُنثَىٰ وَهُوَ مُؤۡمِنٞ فَأُوْلَٰٓئِكَ يَدۡخُلُونَ ٱلۡجَنَّةَ وَلَا يُظۡلَمُونَ نَقِيرٗا 124﴾
"Na anayefanya mema, akiwa mwanamume au mwanamke, naye ni Muumini - basi hao wataingia Peponi wala hawatadhulumiwa hata kadiri ya tundu la kokwa la tende." [An-Nisaa: 124].
Na akaweka wazi kuwa ushirikina huharibu matendo, kama alivyosema Allah Mtukufu:
﴿وَلَقَدۡ أُوحِيَ إِلَيۡكَ وَإِلَى ٱلَّذِينَ مِن قَبۡلِكَ لَئِنۡ أَشۡرَكۡتَ لَيَحۡبَطَنَّ عَمَلُكَ وَلَتَكُونَنَّ مِنَ ٱلۡخَٰسِرِينَ 65﴾
"Na kwa yakini yamefunuliwa kwako na kwa walio kuwa kabla yako: Bila ya shaka ukimshirikisha Mwenyezi Mungu amali zako zitaanguka, na lazima utakuwa miongoni mwa wenye kupata hasara." [Az-Zumar: 65]
Na nguzo za Imani ni sita: Ni kumuamini Mwenyezi Mungu, na Malaika wake, na Vitabu vyake, na Mitume wake, na Siku ya Mwisho, na kuamini Kadari kheri yake na shari yake.
1) Kumuamini Mwenyezi Mungu Mtukufu kunajumuisha mambo matatu:
1- Kuamini umola wake:
Nayo ni kumpwekesha Mwenyezi Mungu Mtukufu kwa matendo yake; kama vile kuumba, kuruzuku, kuhuisha na kufisha. Hivyo basi, hakuna muumba isipokuwa Mwenyezi Mungu, wala hakuna mtoa rizki isipokuwa Mwenyezi Mungu, wala hakuna anayehuisha isipokuwa Mwenyezi Mungu, wala hakuna anayefisha isipokuwa Mwenyezi Mungu, wala hakuna anayeendesha mambo katika ulimwengu isipokuwa Yeye Mwenyezi Mungu Mtukufu.
Wala haikujulikana kwamba yupo yeyote miongoni mwa viumbe aliyeukanusha Umola wa Mwenyezi Mungu Aliyetakasika, isipokuwa kama ni mkaidi, asiyeamini anachokisema, Kama ilivyotokea kwa Firauni, aliposema kuwaambia watu wake:
﴿...أَنَا رَبُّكُمُ الْأَعْلَى﴾
Akasema: "Mimi ndiye Mola wenu Mlezi mkuu kabisa." [An-Nazi'at: 24]. Lakini hilo halitokani na itikadi, kama alivyosema Mwenyezi Mungu Mtukufu kuhusu Mussa, amani imshukie:
﴿قَالَ لَقَدۡ عَلِمۡتَ مَآ أَنزَلَ هَٰٓؤُلَآءِ إِلَّا رَبُّ ٱلسَّمَٰوَٰتِ وَٱلۡأَرۡضِ بَصَآئِرَ وَإِنِّي لَأَظُنُّكَ يَٰفِرۡعَوۡنُ مَثۡبُورٗا 102﴾
Musa akasema: "Wewe unajua bila ya shaka kuwa haya hakuyateremsha ila Mola Mlezi wa mbingu na ardhi ili kuwa ni ushahidi wa kuonekana. Na hakika mimi bila ya shaka nakuona wewe, Firauni, kuwa umekwisha angamia." [Al-Israa: 102] Na akasema Mwenyezi Mungu Mtukufu:
﴿وَجَحَدُوا بِهَا وَاسْتَيْقَنَتْهَا أَنْفُسُهُمْ ظُلْمًا وَعُلُوًّا... ﴾
"Na wakazikataa kwa dhuluma na kujivuna, na hali ya kuwa nafsi zao zina yakini nazo..." [An-Naml: 14].
Kwa hakika viumbe hivi lazima viwe na Muumbaji, Kwa kuwa kitu hakiwezi kujileta chenyewe; Kwa sababu kitu hakiwezi kujiumba chenyewe, wala hakiwezi kupatikana ghafla; kwa sababu kila chenye kuzuka ni lazima kiwe na mletaji, Na kwa kuwa kuwapo kwake katika mfumo huu wa ajabu wenye ustadi na ulinganifu ulioshikamana kunafanya isiwezekane kudai kwamba kuwepo kwake ni matokeo ya bahati nasibu, imebainika kwamba ni lazima liwe na Muumbaji, naye ni Mwenyezi Mungu Mola wa Walimwengu, amesema Mwenyezi Mungu Mtukufu:
﴿أَمۡ خُلِقُواْ مِنۡ غَيۡرِ شَيۡءٍ أَمۡ هُمُ ٱلۡخَٰلِقُونَ 35 أَمۡ خَلَقُواْ ٱلسَّمَٰوَٰتِ وَٱلۡأَرۡضَۚ بَل لَّا يُوقِنُونَ 36﴾
"Au wao wameumbwa pasina kutokana na kitu chochote, au ni wao ndio waumbaji?
Au wao wameziumba mbingu na ardhi? Bali hawana yakini." [Surat Tuur: 35-36]
Washirikina walikuwa wakikiri umola wa Mwenyezi Mungu Mtukufu, huku wakimshirikisha katika ibada, na hilo halikuwaingiza katika Uislamu. Mtume, rehema na amani za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake, akawapiga vita, na akaona kuwa halali damu zao na mali zao; kwa sababu walimshirikisha Mwenyezi Mungu katika ibada. Basi wakaabudu pamoja na Mwenyezi Mungu asiyekuwa Yeye; kama Masanamu, Mawe na Malaika na wengineo.
2- Kuamini Uungu wake:
Kuamini Uungu wake; yaani kwamba Yeye peke yake ndiye anayestahiki kuabudiwa kwa haki, hana mshirika. Na (Al-Ilaahu) kwa maana ya (anayeabudiwa), yaani (muabudiwa) kwa kumpenda na kumtukuza na kujinyenyekeza kwake.
Amesema Mwenyezi Mungu Mtukufu:
﴿وَإِلَٰهُكُمۡ إِلَٰهٞ وَٰحِدٞۖ لَّآ إِلَٰهَ إِلَّا هُوَ ٱلرَّحۡمَٰنُ ٱلرَّحِيمُ 163﴾
"Na Mungu wenu ni Mungu mmoja tu, hapana mungu ila Yeye. Mwingi wa rehema, Mwenye kurehemu." [Al-Baqarah: 163].
Na kila atakayejiwekea mungu mwingine pamoja na Mwenyezi Mungu, akamuabudu kinyume na Yeye; basi uungu wake ni batili, amesema Mwenyezi Mungu Mtukufu:
﴿ذَٰلِكَ بِأَنَّ ٱللَّهَ هُوَ ٱلۡحَقُّ وَأَنَّ مَا يَدۡعُونَ مِن دُونِهِۦ هُوَ ٱلۡبَٰطِلُ وَأَنَّ ٱللَّهَ هُوَ ٱلۡعَلِيُّ ٱلۡكَبِيرُ 62﴾
"Hayo ni kwa kuwa Mwenyezi Mungu ndiye Wa Kweli, na kwamba wale wanaowaomba badala yake, ni batili, na hakika Mwenyezi Mungu ndiye Aliye Juu na ndiye Mkubwa." [Surat Al-Hajj: 62].
Na kwa sababu hiyo Mitume amani iwafikie, kuanzia kwa Nuhu mpaka kwa Muhammad rehema na amani za Allah ziwe juu yake, walikuwa wakiwalingania watu wao katika kumuabudu Mwenyezi Mungu peke yake, kumfanyia ibada Yeye tu, na kuacha ibada ya asiyekuwa Yeye. Mwenyezi Mungu Mtukufu amekifutilia mbali kitendo cha washirikina cha kujifanyia miungu wanaowaabudu pamoja na Mwenyezi Mungu Aliyetakasika na kutukuka, na kujitafutia ushindi kupitia kwao, na kutafuta msaada kutoka kwao; na hilo ni kwa hoja mbili za kiakili:
Jambo la kwanza: Hakuna katika miungu hii waliyo jitwalia hata chembe ya sifa mahususi za uungu; bali hiyo inaumbwa, haiumbi chochote, wala haileti manufaa kwa waabudu wake, wala haiwakingi madhara, wala haimiliki mauti, wala uhai, wala kufufuka.
kama alivyosema Allah Mtukufu:
﴿وَٱتَّخَذُواْ مِن دُونِهِۦٓ ءَالِهَةٗ لَّا يَخۡلُقُونَ شَيۡـٔٗا وَهُمۡ يُخۡلَقُونَ وَلَا يَمۡلِكُونَ لِأَنفُسِهِمۡ ضَرّٗا وَلَا نَفۡعٗا وَلَا يَمۡلِكُونَ مَوۡتٗا وَلَا حَيَوٰةٗ وَلَا نُشُورٗا 3﴾
"Na wamechukua badala yake miungu ambayo haiumbi chochote, bali hiyo inaumbwa, haijimilikii nafsi zao madhara wala manufaa, wala haimiliki mauti, wala uhai, wala kufufuka." [Al-Furqan: 3].
Jambo la pili: Kwamba washirikina hawa walikuwa wakikiri kuwa Mwenyezi Mungu Mtukufu ndiye Muumbaji na Mwenye kuendesha mambo peke Yake, pasina mwingine yeyote; na hili linawajibisha wam pwekeshe katika uungu kama walivyomkiri kuwa wa pekee katika umola. kama alivyosema Allah Mtukufu:
﴿قُل لِّمَنِ ٱلۡأَرۡضُ وَمَن فِيهَآ إِن كُنتُمۡ تَعۡلَمُونَ 84 سَيَقُولُونَ لِلَّهِۚ قُلۡ أَفَلَا تَذَكَّرُونَ 85 قُلۡ مَن رَّبُّ ٱلسَّمَٰوَٰتِ ٱلسَّبۡعِ وَرَبُّ ٱلۡعَرۡشِ ٱلۡعَظِيمِ 86 سَيَقُولُونَ لِلَّهِۚ قُلۡ أَفَلَا تَتَّقُونَ 87 قُلْ مَنْ بِيَدِهِ مَلَكُوتُ كُلِّ شَيْءٍ وَهُوَ يُجِيرُ وَلَا يُجَارُ عَلَيْهِ إِنْ كُنْتُمْ تَعْلَمُونَ 88 سَيَقُولُونَ لِلَّهِ قُلْ فَأَنَّى تُسْحَرُونَ 89﴾
"Sema: Ni ya nani ardhi na viliomo ndani yake, kama nyinyi mnajua? *
Watasema: Ni vya Mwenyezi Mungu! Sema: Basi, je, hamkumbuki? 85 *
Sema: Ni nani Mola Mlezi wa mbingu saba na Mola Mlezi wa A'rshi Kuu? 86
Watasema: Ni vya Mwenyezi Mungu. Sema: Basi je, hamuogopi? 87
Sema: Ni nani mkononi mwake umo Ufalme wa kila kitu, naye ndiye anayelinda, wala hakilindwi asichotaka, kama mnajua? 88
Watasema: (Ufalme huo) ni wa Mwenyezi Mungu. Sema: Basi vipi mnadanganyika? 89 [Al-Muminun: 84-89] Basi wakikiri Tauhid Ar-rububiyya, (umola) ni lazima wamuabudu Mwenyezi Mungu Mtukufu peke yake, wala wasimshirikishe pamoja naye yeyote katika ibada yake.
3- Kuamini majina ya Mwenyezi Mungu na sifa zake:
Yaani: Kuthibitisha yale aliyoyathibitisha Mwenyezi Mungu kwa nafsi yake katika Kitabu chake, au Mtume -rehema na amani ziwe juu yake- akamthibitishia hilo katika Sunna yake; miongoni mwa majina na sifa, kwa namna inayomstahiki Mwenyezi Mungu Mtukufu, pasina kuzibadailisha wala kuzipinga. wala kuainisha namna yake, wala kufananisha. Amesema Mwenyezi Mungu Mtukufu:
﴿وَلِلَّهِ ٱلۡأَسۡمَآءُ ٱلۡحُسۡنَىٰ فَٱدۡعُوهُ بِهَاۖ وَذَرُواْ ٱلَّذِينَ يُلۡحِدُونَ فِيٓ أَسۡمَٰٓئِهِۦۚ سَيُجۡزَوۡنَ مَا كَانُواْ يَعۡمَلُونَ 180﴾
"Na Mwenyezi Mungu ana majina mazuri kabisa, basi muombeni kwa hayo. Na waacheni wale wanao haribu utakatifu wa majina yake. Hao watakuja lipwa waliyo kuwa wakiyatenda." [Al-A'raf: 180] Na akasema Mwenyezi Mungu Mtukufu:
﴿...لَيۡسَ كَمِثۡلِهِۦ شَيۡءٞۖ وَهُوَ ٱلسَّمِيعُ ٱلۡبَصِيرُ﴾
"Hapana kitu kama mfano wake. Naye ni Mwenye kusikia Mwenye kuona." [Ash-Shuraa: 11].
Vigawanyo vya Ushirikina ni vitatu:
1- Shirki kubwa.
2- Shirki ndogo.
3- Ushirikina uliofichika.
1- Shirki kubwa:
Na kigezo chake ni: Kumlinganisha kiumbe na Mwenyezi Mungu Mtukufu katika mambo maalumu kwa Mwenyezi Mungu Mtukufu pekee. kama alivyosema Allah Mtukufu:
﴿إِذۡ نُسَوِّيكُم بِرَبِّ ٱلۡعَٰلَمِينَ 98﴾
"Tulipo kufanyeni ni sawa na Mola Mlezi wa walimwengu wote." [Ash-Shu'ara: 98].
Nalo linajumuisha: Kumfanyia ibada asiyekuwa Mwenyezi Mungu aliyetukuka, Au kuelekeza baadhi ya ibada kwa asiyekuwa Mwenyezi Mungu Mtukufu; kama vile kuomba dua, kutafuta kuokolewa, kuweka nadhiri na kuchinja, na mengineyo katika aina za ibada.
Au linajumuisha: Kuhalalisha yale ambayo Mwenyezi Mungu Mtukufu ameyaharamisha, au kuharamisha kilichohalalishwa na sheria, au kutengua yale ambayo Mwenyezi Mungu Mtukufu amewajibisha, Kama kuha lalisha yale yanayojulikana kwa dharura katika dini kuwa ni haramu; kama kuhalalisha zinaa au pombe au kuwaasi wazazi wawili au riba au yanayofanana na hayo.
Au kuharamisha yale ambayo Mwenyezi Mungu ameyahalalisha miongoni mwa vitu vizuri, au kubatilisha yale ambayo Mwenyezi Mungu amewajibisha; Kama kuamini kuwa swala sio wajibu, au kuwa saumu sio wajibu, au kuwa zaka sio wajibu.
Ushirikina mkubwa unapelekea kuharibika kwa matendo, na kukaa milele Motoni kwa wale wanaokufa bila ya kuuacha. kama alivyosema Allah Mtukufu:
﴿...وَلَوۡ أَشۡرَكُواْ لَحَبِطَ عَنۡهُم مَّا كَانُواْ يَعۡمَلُونَ﴾
"Na lau wangelimshirikisha yangeliwaharibikia waliyokuwa wakiyatenda." [Surat Al-An'am: 88].
Na kwamba yeyote atakayekufa bila ya kuuacha, hatasamehewa, na itakuwa haramu kwake kuingia Peponi, kama alivyosema Allah Mtukufu:
﴿إِنَّ ٱللَّهَ لَا يَغۡفِرُ أَن يُشۡرَكَ بِهِۦ وَيَغۡفِرُ مَا دُونَ ذَٰلِكَ لِمَن يَشَآءُ...﴾
"Hakika Mwenyezi Mungu hasamehe kushirikishwa, na husamehe yaliyo duni ya hilo kwa amtakaye..." [An-Nisaa: 48]. Na akasema Mwenyezi Mungu Mtukufu:
﴿إِنَّهُۥ مَن يُشۡرِكۡ بِٱللَّهِ فَقَدۡ حَرَّمَ ٱللَّهُ عَلَيۡهِ ٱلۡجَنَّةَ وَمَأۡوَىٰهُ ٱلنَّارُ...﴾
"Hakika anayemshirikisha Mwenyezi Mungu, hakika Mwenyezi Mungu atamharamishia Pepo, na mahala pake ni Motoni..." [Al-Ma’idah: 72].
2- Shirki ndogo:
Nayo ni kile kilichothibitishwa kwa maandiko kuitwa shirki, lakini hakifikii kiwango cha ushirikina mkubwa; hivyo hiki kinaitwa ushirikina mdogo; kama kuapa kwa asiyekuwa Mwenyezi Mungu Mtukufu; kama vile kuapa kwa Al-Kaaba, na Manabii, na amana, na uhai wa fulani, na mengineyo, kama alivyosema Mtume -rehema na amani ziwe juu yake-: “Mwenye kuapa kwa asiyekuwa Mwenyezi Mungu, basi hakika amekufuru au ame shirikisha.”2.
Na huenda likawa kubwa kulingana na yaliyomo moyoni mwa mja, Iwapo muapaji kwa Mtume, rehema na amani ziwe juu yake, au shekhe fulani, ataitakidi moyoni mwake kwamba yeye ni kama Mwenyezi Mungu, au kwamba anaombwa kinyume na Mwenyezi Mungu, au kwamba anatawala mambo ya ulimwengu; basi hiyo ni shirki kubwa. Ama ikiwa anayeapa kwa asiyekuwa Mwenyezi Mungu hakukusudia hilo, bali limetoka tu kwenye ulimi wake bila makusudio hayo, kwa kuwa amezoea jambo hilo; basi itakuwa katika shirki ndogo. Na hili hutokea mara nyingi katika baadhi ya maeneo; basi wajibu ni kutanabahi kwa hilo, na kutahadhari nalo, ili kuilinda tauhidi na kuihami.
3- Ushirikina uliofichika:
Ni yale yanayokuwa mioyoni katika riyaa (kujionyesha); Kama yule anayeswali au anayesoma Qur'ani ili kujionyesha kwa watu, au anayemsabihi Mwenyezi Mungu ili watu wamhimidi, au anayetoa sadaka ili watu wamsifu, na hili linaharibu lile tendo alilolifanya kwa kujionyesha kwa watu, bila kuathiri matendo mengine aliyoyatakasia nia kwa ajili ya Mwenyezi Mungu.
Na amesema rehema na amani ziwe juu yake: "Ushirikina katika Umma huu umefichikana zaidi kuliko kutambaa kwa mdudu chungu kwenye jiwe jeusi katika giza la usiku, na kafara yake ni kusema: “Ee Mwenyezi Mungu, hakika mimi najikinga Kwako nisije nikakushirikisha chochote hali ninajua, na ninakuomba msamaha kwa dhambi nisiyoijua.”3.
Aina za Ukafiri:
La kwanza: Ukafiri mkubwa:
Huo ndio unaopelekea kudumu motoni, na huo una aina tano:
1- Ukafiri wa kukanusha:
Nayo ni itikadi ya kuwakadhibisha Mitume, na hili ni nadra miongoni mwa makafiri; kwa kuwa Mwenyezi Mungu aliwasaidia Mitume wake, amani iwe juu yao, kwa hoja zilizo wazi, Kwa hakika hali ya hawa wanao kadhibisha ni kama alivyowasifu Mwenyezi Mungu Mtukufu:
﴿وَجَحَدُوا بِهَا وَاسْتَيْقَنَتْهَا أَنْفُسُهُمْ ظُلْمًا وَعُلُوًّا...﴾
"Na wakazikataa kwa dhuluma na kujivuna, na hali ya kuwa nafsi zao zina yakini nazo..." [An-Nahl: 14].
2- Ukafiri wa kufanya kiburi na kukataa:
Na huu ni mfano wa ukafiri wa Ibilisi; kwani hakukataa amri ya Mwenyezi Mungu Mtukufu wala hakukanusha, bali akaikabili kwa kukataa, kwa ujeuri na kiburi. Amesema Mwenyezi Mungu Mtukufu:
﴿وَإِذۡ قُلۡنَا لِلۡمَلَٰٓئِكَةِ ٱسۡجُدُواْ لِأٓدَمَ فَسَجَدُوٓاْ إِلَّآ إِبۡلِيسَ أَبَىٰ وَٱسۡتَكۡبَرَ وَكَانَ مِنَ ٱلۡكَٰفِرِينَ 34﴾
"Na tulipowaambia Malaika: Msujudieni Adam, wakamsujudia wote isipokuwa Ibilisi, alikataa na akajivuna na akawa katika makafiri." [Al-Baqara: 34].
3- Kufuru ya kupuuza:
Na hilo ni kwa kupuuza kwa masikio yake na moyo wake kuifuata haki; haigeukii, wala haitilii maanani. Amesema Mwenyezi Mungu Mtukufu:
﴿وَمَنۡ أَظۡلَمُ مِمَّن ذُكِّرَ بِـَٔايَٰتِ رَبِّهِۦ ثُمَّ أَعۡرَضَ عَنۡهَآۚ إِنَّا مِنَ ٱلۡمُجۡرِمِينَ مُنتَقِمُونَ 22﴾
"Na ni nani dhalimu mkubwa kuliko yule anaye kumbushwa kwa Ishara za Mola wake Mlezi, kisha akazikataa? Hakika Sisi tutajilipiza kwa wakosefu." [As-Sajda: 22].
Ama kupuuza baadhi ya sehemu; hilo ni uasi wala si ukafiri; kama yule anayepuuza kujifunza baadhi ya yale ya wajibu katika dini, kama hukumu za Saumu au Hija na mfano wake.
4- Ukafiri wa shaka:
Na hilo huwa kwa kusitasita, wala hasemi kwa yakini juu ya jambo la haki, bali anakuwa na shaka kwalo, kama ilivyo katika kauli ya Mwenyezi Mungu Mtukufu:
﴿وَدَخَلَ جَنَّتَهُ وَهُوَ ظَالِمٌ لِنَفْسِهِ قَالَ مَا أَظُنُّ أَنْ تَبِيدَ هَذِهِ أَبَدًا 35 وَمَا أَظُنُّ السَّاعَةَ قَائِمَةً وَلَئِنْ رُدِدْتُ إِلَى رَبِّي لَأَجِدَنَّ خَيْرًا مِنْهَا مُنْقَلَبًا 36﴾
"Na akaingia kitaluni kwake, naye hali anajidhulumu nafsi yake. Akasema: Sidhani kabisa kuwa haya yataharibika.
Wala sidhani kuwa hiyo Saa (ya Kyama) itatokea. Na ikiwa nitarudishwa kwa Mola wangu Mlezi, bila ya shaka nitapata marejeo bora zaidi kuliko haya." [Al-Kahf: 35-36].
5- Ukafiri wa unafiki:
Nayo ni kudhihirisha imani kwa ulimi, na kuficha moyoni kukadhibisha. Amesema Mwenyezi Mungu Mtukufu:
﴿وَمِنَ ٱلنَّاسِ مَن يَقُولُ ءَامَنَّا بِٱللَّهِ وَبِٱلۡيَوۡمِ ٱلۡأٓخِرِ وَمَا هُم بِمُؤۡمِنِينَ 8﴾
"Na katika watu, wako wasemao: Tumemwamini Mwenyezi Mungu na Siku ya Mwisho, wala wao si wenye kuamini." [Al-Baqara: 8].
Na hizi ndizo aina za Ukafiri mkubwa unaomtoa mtu katika mila ya Uislamu.
Aina ya pili: Ukafiri mdogo:
Na aina hii haimfanyi mtu kukaa Motoni milele, nayo ni yale yaliyokuja katika Kitabu na Sunna yakaitwa ukafiri bila ya Alifu na Laam, bali yametajwa kwa hali ya Nakira (pasina kuanza na Alif na Laam). Na mifano yake ni mingi sana, miongoni mwayo:- Kutoka kwa Abuu Huraira -radhi za Allah ziwe juu yake- amesema: Amesema Mtume wa Mwenyezi Mungu -rehema na amani za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake:-
"Mambo mawili kwa watu hayo kwao ni ukafiri: Kutukana ukoo, na kulia kwa kumuomboleza maiti"4.
2) Kuamini Malaika:
Nao ni ulimwengu wa ghaibu, Mwenyezi Mungu -Aliyetukuka- aliwaumba kutokana na nuru, nao wana muabudu Mwenyezi Mungu Mtukufu, wala hawana chochote katika sifa za vitendo vya Mwenyezi Mungu, wala sifa za kuabudiwa, nao hawamuasi Mwenyezi Mungu kwa yale aliyowaamrisha, na wanafanya wanayo amrishwa, nao ni wengi, idadi yao haiwezi kuhesabiwa isipokuwa na Mwenyezi Mungu Mtukufu.
Na kuamini Malaika kunakusanya mambo manne:
1- Kuamini uwepo wao.
2- Kuwaamini wale ambao tumeyafahamu majina yao miongoni mwao; kama: Jibril, Mikaeli, Israfili, na wengineo. Na yeyote ambaye hatujui jina lake, tuna mwamini kwa ujumla.
3- Kuamini yale tuliyoyajua miongoni mwa sifa zao, zilizokuja katika kitabu cha Mwenyezi Mungu na mafundisho ya Mtume -rehema na amani ziwe juu yake-; Kuhusu sifa ya Jibrili, Mtume -rehema na amani ziwe juu yake- alieleza kwamba alimuona kwa sifa yake ambayo Mwenyezi Mungu kamuumba nayo, na ana mbawa mia sita, ambazo zimeziba anga.
4- Kuamini yale tuliyoyajua kuhusu matendo yao; kama kumsabihi kwao Mwenyezi Mungu Aliyetukuka, na kumuabudu usiku na mchana bila kuchoka wala kulegea.
Kwa mfano: Jibril: Mwaminifu wa Ufunuo.
Na Israfili: Aliyekabidhiwa jukumu la kupuliza Baragumu.
Na Malaika wa mauti: Aliye wakilishwa kwa ajili ya kuchukua roho wakati wa mauti.
Na Malik: Mlinzi wa Moto. Na Ridhwan: Mlinzi wa Pepo, na wengine.
3) Kuamini vitabu:
Na kinachokusudiwa kwa vitabu: Ni vitabu vya mbinguni ambavyo ameviteremsha Mwenyezi Mungu kwa Mitume wake, Ni uongofu kwa wanadamu na ni rehema kwao, ili wafikie furaha ya Dunia na Akhera.
Na kuamini Vitabu, yanaingia ndani yake mambo manne:
1- Kuamini kuwa vimeteremshwa kutoka kwa Mwenyezi Mungu kwa hakika.
2- Kuamini vile ambavyo tumejua majina yake miongoni mwavyo; kama Qur'ani iliyoteremshwa kwa Muhammadi -rehema na amani ziwe juu yake-, na Taurati iliyoteremshwa kwa Mussa- amani iwe juu yake, na Injili iliyoteremshwa kwa Issa amani iwe juu yake, Na Zaburi aliyopewa Nabii Daudi, amani iwe juu yake.
Ama kile tusichojua jina lake, tunakiamini kwa ujumla.
3- Kusadikisha yale yaliyoyaelezwa na vitabu hivyo; kama yale yaliyoyaelezwa katika Qur'ani, na yale yaliyoyaelezwa katika vitabu vilivyotangulia ambavyo havijabadilishwa na kugeuzwa.
4- Kutekeleza hukumu za yale ambayo hayajafutwa (kisheria), na kuridhia na kujisalimisha kwa hukumu hizo, iwe tumeifahamu hekima yake au hatujaifahamu. Na vitabu vyote vilivyotangulia vimefutwa na Qur'ani hii kubwa, Si halali kutekeleza hukumu yoyote miongoni mwa hukumu za vitabu vya awali isipokuwa ile iliyothibiti kwa usahihi, na ikathibitishwa na Qur'ani au sunna ya Mtume -rehema na amani ziwe juu yake-.
4) Kuwaamini Mitume, amani iwe juu yao:
Neno Mitume: Ni wingi wa Mtume; naye ni yule aliyefunuliwa wahyi miongoni mwa wanadamu kwa Sheria na akaamrishwa kuifikisha. Na wa mwanzo wao ni Nuhu amani ziwe juu yake, na wa mwisho wao ni Muhammad rehema na amani ziwe juu yake, Nao ni binadamu walioumbwa, Hawana chochote katika sifa za vitendo vya Mwenyezi Mungu (kama vile kutoa riziki na kuhuisha n.k), wala sifa za kuabudiwa.
Na kuamini Mitume kunajumuisha:
1- Kuamini kuwa ujumbe wao ni haki kutoka kwa Allah, Na mwenye kuukufuru utume wa mmoja wao, basi hakika amewakufuru wote.
2- Kuwaamini kwa majina yao wale tunaoyajua majina yao miongoni mwao; kama vile Muhammad, Ibrahim, Mussa, Issa, na Nuhu - rehema na amani ziwe juu yao. Nao ni wenye azma thabiti miongoni mwa Mitume.
Na yeyote ambaye hatujui jina lake miongoni mwao, tunamwamini kwa ujumla. Amesema Mwenyezi Mungu Mtukufu:
﴿وَلَقَدۡ أَرۡسَلۡنَا رُسُلٗا مِّن قَبۡلِكَ مِنۡهُم مَّن قَصَصۡنَا عَلَيۡكَ وَمِنۡهُم مَّن لَّمۡ نَقۡصُصۡ عَلَيۡكَ...﴾
"Na bila ya shaka tuliwatuma Mitume kabla yako. Wengine katika hao tumekusimulia habari zao, na wengine hatukukusimulia..." [Ghafiri: 78].
3- Kusadikisha yale yaliyothibiti kutoka kwao, amani za Mwenyezi Mungu ziwe juu yao, miongoni mwa habari zao.
4- Kutekeleza Sheria ya yule miongoni mwao aliyeletumwa kwetu, naye ni Mwisho wa Manabii na Mitume, Muhammad rehema na amani ziwe juu yake.
5) Kuamini siku ya mwisho:
Nayo ni Siku ya Kiyama, ambayo watu watafufuliwa humo kwa ajili ya hesabu na malipo, na imeitwa Siku ya Mwisho; kwa sababu hakuna siku nyingine (ya kidunia) baada yake, kiasi ambacho watatulizana watu wa Peponi katika makazi yao, na watu wa Motoni katika makazi yao.
Na kuamini Siku ya Mwisho kunajumuisha mambo matatu:
A- Kuamini ufufuo:
Nayo ni kuwafufua watu litakapopulizwa baragumu kwa mara ya pili, na watu watasimama mbele ya Mweyezi Mungu, Mlezi wa viumbe vyote, bila viatu, uchi, na wakiwa hawajatahiriwa, Amesema Mwenyezi Mungu Mtukufu:
﴿كَمَا بَدَأْنَا أَوَّلَ خَلْقٍ نُعِيدُهُ وَعْدًا عَلَيْنَا إِنَّا كُنَّا فَاعِلِينَ 104﴾
"Kama tulivyo anza umbo la mwanzo tutalirudisha tena. Ni ahadi iliyo juu yetu. Hakika Sisi ni watendao. [Al-Anbiya: 104].
b. Kuamini kuhesabiwa na malipo:
Ambapo mja atahesabiwa kwa amali zake, na atapata malipo yake kulingana nazo, Amesema Mwenyezi Mungu Mtukufu:
﴿إِنَّ إِلَيۡنَآ إِيَابَهُمۡ 25 ثُمَّ إِنَّ عَلَيۡنَا حِسَابَهُم 26﴾
"Hakika ni kwetu Sisi ndio marejeo yao.
Kisha hakika ni juu yetu Sisi hisabu yao!" [Al-Ghashiya: 25-26].
C- Kuamini Pepo na Moto.
Na kwamba viwili hivyo ni hatima ya milele kwa viumbe; Basi Pepo ndiyo nyumba ya neema aliyoiandaa Mwenyezi Mungu Mtukufu kwa waumini wacha-Mungu na waliotekeleza utiifu kwa Mwenyezi Mungu na Mtume wake ﷺ. Ndani yake kuna yale ambayo jicho halijawahi kuona, wala sikio halikuwahi kusikia, wala moyo wa mwanadamu haukuwahi kufikiria.
Ama Moto; Hayo ni makao ya adhabu, ambayo Mwenyezi Mungu Mtukufu amewaandalia makafiri waliomkufuru Mwenyezi Mungu na waliowaasi Mitume Wake. Humo kuna aina za adhabu na mateso ambayo mfano wake haujawahi kupitia katika fikira.
6) Kuamini Kadari kheri zake na shari zake:
Na makusudio ya Kadari: Ni Mipangilio ya Mwenyezi Mungu Mtukufu kwa yatakayotokea kulingana na yaliyo tangulia na elimu yake Mwenyezi Mungu na namna hekima yake ilivyopelekea.
Na kuamini Kadari, inaingia ndani yake kuamini mambo manne:
1- Elimu: Nayo ni kuamini elimu ya Mwenyezi Mungu Mtukufu, na kwamba yeye ni mjuzi kwa yale yaliyokuwepo na yatakayokuwepo na jinsi yatakavyo kuwa, kwa ujumla na kwa undani, tangu azali hadi abadi. Naye Mwenyezi Mungu Mtukufu ndiye Mjuzi wa yale ambayo hayakutokea; lau yangetokea yange kuwaje, kama alivyosema Mwenyezi Mungu Mtukufu:
﴿وَلَوۡ رُدُّواْ لَعَادُواْ لِمَا نُهُواْ عَنۡهُ ...﴾
"Na kama wangelirudishwa bila ya shaka wange yarejea yale yale waliyokatazwa ..." [Al-An'am: 28].
2- Kuandika: Nayo ni kwamba Mwenyezi Mungu Mtukufu aliandika makadirio ya kila kitu mpaka kusimama Kiyama. kama alivyosema Allah Mtukufu:
﴿أَلَمۡ تَعۡلَمۡ أَنَّ ٱللَّهَ يَعۡلَمُ مَا فِي ٱلسَّمَآءِ وَٱلۡأَرۡضِۚ إِنَّ ذَٰلِكَ فِي كِتَٰبٍۚ إِنَّ ذَٰلِكَ عَلَى ٱللَّهِ يَسِيرٞ 70﴾
"Je! Hujui kwamba Mwenyezi Mungu anayajua yaliomo mbinguni na katika ardhi? Hakika hayo yamo Kitabuni. Hakika hayo kwa Mwenyezi Mungu ni mepesi." [Al-Hajj: 70].
3- Matashi: Nayo ni kuamini kwamba katika ulimwengu huu hakitokei chochote isipokuwa kile alichokitaka Mwenyezi Mungu Mtukufu. Amesema Mwenyezi Mungu Mtukufu:
﴿وَرَبُّكَ يَخۡلُقُ مَا يَشَآءُ وَيَخۡتَارُ ...﴾
"Na Mola wako Mlezi huumba na huteuwa atakavyo..." [Al-Qasas: 68], Na mwanadamu ana utashi ambao hautoki nje ya matashi ya Mwenyezi Mungu, kama alivyosema Mwenyezi Mungu Mtukufu:
﴿وَمَا تَشَآءُونَ إِلَّآ أَن يَشَآءَ ٱللَّهُ رَبُّ ٱلۡعَٰلَمِينَ 29﴾
"Wala nyinyi hamtataka isipokuwa atake Mwenyezi Mungu Mola Mlezi wa walimwengu wote." [At-Takwir: 29].
4- Uumbaji: Ni kuamini kuwa Mwenyezi Mungu Mtukufu ndiye aliyeumba viumbe na matendo yao na vitendo vyao vyote, vya kheri na vya shari. Amesema Mwenyezi Mungu Mtukufu:
﴿ٱللَّهُ خَٰلِقُ كُلِّ شَيۡءٖۖ وَهُوَ عَلَىٰ كُلِّ شَيۡءٖ وَكِيلٞ 62﴾
"Mwenyezi Mungu ndiye Muumba wa kila kitu, na Yeye ndiye Mlinzi juu ya kila kitu." [Az-Zumar: 62].
Haya yamekusanywa katika beti hii:
Ni ujuzi wa Mwenyezi Mungu wa kujua vitu vyote, na kuviandika, na kutaka kwake viwe; na kuumba kwake, nako ni kuviweka katika kuwako na kuviunda.
Mjadala wa Tatu: (Ihsan) Kufanya ibada kwa wema
Ihsan: Ni nguzo moja; nayo nikuwa umuabudu Mwenyezi Mungu kana kwamba unamuona, na ikiwa humuoni basi Yeye anakuona.
Yaani: Mwanadamu ayafanye yale ambayo Mwenyezi Mungu amemuamrisha katika ibada kana kwamba amesimama mbele ya Mola wake. Na hivyo kunalazimu ukamilifu wa kumhofu Mwenyezi Mungu, na kurejea Kwake Mtukufu. Na kunalazimu kuitekeleza ibada kwa mujibu wa Sunna za Mtume, rehema na amani ziwe juu yake.
Na Ihsani iko katika daraja mbili, na wafanyao ihsani katika Ihsani wamo katika vyeo viwili vilivyotofautiana:
Nafasi ya kwanza: Na ndio ya juu zaidi, ni nafasi ya kushuhudia; nayo ni kwamba mja atende kana kwamba anamuona Mwenyezi Mungu kwa moyo wake, hivyo moyo ukatiwa nuru kwa Imani, hadi ghaibu iwe kama dhahiri.
Nafasi ya pili: Nafasi ya kutakasa matendo kwa ajili ya Allah na kuhisi Allah anakuona, Nayo ni kuwa mja ajitahidi kuleta moyoni kuwa anatazamwa na Mwenyezi Mungu, na kwamba Yeye ni Mjuzi wa hali yake; akihudhurisha hilo moyoni, basi huyu ndiye mtakasifu kwa Mwenyezi Mungu Mtukufu.
Mada ya Nne: Muhtasari mfupi wa baadhi ya misingi ya Ahlus-Sunna wal-Jamaa:
La Kwanza: Kufuata yale yaliyokuja katika Qur'ani Tukufu na sunna kwa siri na kwa dhahiri, na kuto kutanguliza kauli ya mtu yeyote mbele ya kauli ya Mwenyezi Mungu Mtukufu na kauli ya Mtume wake -rehema na amani ziwe juu yake-.
Pili: Usafi wa nyoyo zao na ndimi zao kwa Maswahaba wa Mtume rehema na amani ziwe juu yake, Wanaona kuwa Khalifa baada ya Mtume rehema na amani ziwe juu yake: Ni Abubakari, kisha Omari, kisha Othman, kisha Ali, radhi za Mwenyezi Mungu ziwe juu yao wote.
Tatu: Mapenzi ya watu wa nyumba ya Mtume wa Mwenyezi Mungu - rehema na amani ziwe juu yake - na kuwafanya kuwa vipenzi; na watu wa nyumba yake - rehema na amani ziwe juu yake - ni wale watu wema miongoni mwao hasa.
Ya nne: Kutojitoa katika utiifu kwa viongozi wa Waislamu, na watawala, hata kama watafanya dhuluma. Na huombewa uadilifu na afya, na wala hawaombewi mabaya. Na kuwatii wenye mamlaka ni katika kumtii Mwenyezi Mungu Mtukufu; ni faradhi, ilimradi wasi amrishe kumuasi Mwenyezi Mungu. Ikiwa wataamrisha kufanya maasi, basi hapaswi kuwatii katika hilo. Na hubakia utiifu wao katika mambo mema yasiyokuwa hayo.
Ya Tano: Kuamini Karama za Mawalii; Nayo ni yale ambayo Mwenyezi Mungu huyafanya yatokee kwa mikono yao katika mambo ambayo yako nje ya mazoea ya kawaida.
Sita: Hawawakufurishi Wanaoelekea Kibla (Waislamu) kwa maasi kwa ujumla wala kwa madhambi makubwa. Kama wafanyavyo Makhawariji, bali udugu wa kiimani unabaki thabiti pamoja na maasi, na wanasema kuhusu muasi: Yeye ni muumini kwa imani yake, muovu kwa dhambi yake kubwa.
Sura ya pili: Katika yale yanayohusiana na ibada mbalimbali.
Sehemu ya Kwanza: Twahara (Usafi).
Twahara kilugha: Ni usafi na kujiepusha na uchafu wa kimwili na wa kimaana.
Kisheria: Ni kuondoa uchafu usioonekana, na kuondoka kwa uchafu. Na twahara (usafi) ndiyo ufunguo wa swala, kwa hivyo, kujifunza hilo ni miongoni mwa majukumu muhimu zaidi katika mambo ya Dini, ambayo ni wajibu kwa kila Muislamu kujifunza na kulipa kipaumbele.
Kwanza : Vigawanyo vya Maji.
1- Tahuru (Masafi mno); Inasihi kujisafisha nayo. sawa sawa iwe yamebakia katika umbile lake la asili; kama maji ya mvua au ya mito au ya bahari, au kitu safi kikachanganyika nayo, kisichoshinda asili wala kuyaondolea jina lake.
2- Najisi; haifai kuyatumia, basi hayaondoi hadathi (hali ya kuwa mchafu inayotokana na kujamiiana au kutokwa na maanii), na wala hayaondoshi najisi, nayo ni yale yaliyobadilika rangi yake, au ladha yake, au harufu yake kwa najisi.
Pili: Yaliyonajisika:
Yaliyonajisika: Nao ni uchafu mahususi, aina yake huzuia swala. Kama mkojo, kinyesi, damu na vinginevyo, hupatikana katika mwili, sehemu, na katika nguo.
Na hali ya asili (kanuni ya msingi) katika vitu ni kwamba vinaruhusiwa na ni safi, basi yeyote anayedai kuwa kitu fulani kina Najisi, basi anatakiwa kuleta ushahidi. Si miongoni mwa najisi: Makohozi, jasho la mwanadamu, na jasho la punda; bali hivyo ni twahara, ingawa ni vya kuchukiza. Kila kilicho najisi ni uchafu, lakini si kinyume chake.
Na najisi ina daraja tatu:
La kwanza: Najisi nzito;
Mfano: Najisi ya kile ambacho mbwa amelamba ndani yake, na njia ya kusafisha kwake: Huoshwa mara saba, mara moja kwa udongo.
La pili: Najisi nyepesi:
Kama mkojo wa mtoto wa kiume mchanga anaye nyonya ukipata kwenye nguo na mfano wake. Na njia ya kuisafisha: Itanyunyiziwa maji juu yake mpaka yaloweshe yote, wala haihitaji kufikicha wala kukamua.
La tatu: Najisi ya wastani:
Kama vile mkojo wa mwanadamu na kinyesi chake, na nyingi katika aina za Najisi, vinapoangukia juu ya ardhi au nguo na mfano wa hivyo. Na njia ya kuisafisha: Ni kuondoa kitu chenyewe cha najisi endapo kipo, na kusafisha maeneo yake kwa maji au kwa vinginevyo katika vitu vya kusafishia.
Na miongoni mwa mambo ambayo ushahidi ume thibitisha kuwa ni najisi:
1- Mkojo wa mwanadamu na kinyesi chake.
2- Madhi na wadi5.
3- Kinyesi cha mnyama ambaye nyama yake hailiwi.
4- Damu ya hedhi na nifasi.
5- Mate ya Mbwa.
6- Mzoga, isipokuwa:
A- Mwanadamu anapokufa.
B- Mzoga wa Samaki na Nzige.
J- Mzoga wa kiumbe kisichokuwa na damu yenye kutiririka; kama vile nzi, sisimizi, nyuki na mfano wake.
D- Mifupa ya Maiti na Pembe zake na Kucha zake na Nywele zake na Manyoya yake.
Na jinsi ya kusafisha najisi huwa:
1- Kwa maji, nayo ndiyo asili katika kusafisha Najisi; hivyo haijuzu kugeukia kisichokuwa maji.
2- Yaliyobainishwa na Sheria kuhusu namna ya kusafisha vitu vilivyo najisi au vilivyopata najisi:
a. Ngozi ya mzoga hutwaharika kwa kuisafisha kwa chumvi na mkunazi.
b- Kutakasa chombo ikiwa mbwa amelamba ndani yake; kitaoshwa mara saba; mara ya kwanza iwe kwa udongo.
Jawabu: Kutwaharisha nguo iwapo itapatwa na damu ya hedhi; kwa kuisugua, kisha kuikamua kwa maji, kisha kuinyunyizia maji; na ikibaki athari baada ya hayo, haidhuru.
D- Kutakasa pindo la vazi la mwanamke; kwa kinachokuja baada yake katika ardhi iliyo safi.
E- Kusafisha nguo kutokana na mkojo wa mtoto mchanga wa kiume anayenyonya; kwa kunyunyizia maji, na kwa kuosha kwa maji kutokana na mkojo wa mtoto mchanga wa kike.
W- Kusafisha nguo kutokana na madhi; kwa kunyu nyiza maji juu ya sehemu.
Z- Kuisafisha sehemu ya chini ya kiatu; kwa kui pangusa katika ardhi iliyo safi.
Y- Kuisafisha ardhi kutokana na najisi; kwa kumimina ndoo ya maji juu ya sehemu husika, au kuiacha hadi ikauke kwa jua au upepo; ikishaondoka athari ya najisi, basi inakuwa safi.
Tatu: Mambo yanayoharamishwa kwa aliyetengukiwa na Udhu kuyafanya:
Vitu vilivyoharamishwa kwa aliyeharibikiwa na Udhu, awe na haja ndogo au kubwa:
1- Swala ya Faradhi au ya Sunna; Na imepokelewa kutoka kwa bin Omari, Mwenyezi Mungu awe radhi nao wote wawili, kwamba Mtume, rehema na amani ziwe juu yake, alisema: "Haikubali Mwenyezi Mungu swala pasina twahara."6.
2- Kushika msahafu; Kwa yale yaliyokuja katika Ujumbe aliomwandikia Mtume -rehema na amani ziwe juu yake- A'mru bin Hazmi, na ndani yake ikaja kauli yake kuwa: «Asiiguse Qur’ani isipokuwa aliye takasika»7.
3- Kutufu katika nyumba ya kale (Alkaaba) Kwa maneno yake Mtume -rehema na amani ziwe juu yake: "Twawafu katika nyumba (Alkaaba) ni Swala, isipokuwa Mwenyezi Mungu ameruhusu mazungumzo hapo."8 Alitawadha Mtume -rehema na amani ziwe juu yake- kwa ajili ya Tawafu, na imepokelewa kwa usahihi kutoka kwa Mtume -rehema na amani ziwe juu yake- kwamba alimkataza mwenye hedhi kuzunguka Kaaba mpaka atwaharike.
Ama mambo yanayoharamishwa kwa aliye katika Hadathi kubwa peke yake ni:
1- Kusoma Qur'ani Kwa mujibu wa hadithi ya Ally -radhi za Allah ziwe juu yake-: "Hakuna chochote kinachomzuia — yaani Mtume -rehema na amani ziwe juu yake- — kutosoma Qur'ani; kisichokuwa janaba"9.
2- Kukaa Msikitini pasina udhu. Kwa maneno yake Mtukufu:
﴿يَٰٓأَيُّهَا ٱلَّذِينَ ءَامَنُواْ لَا تَقۡرَبُواْ ٱلصَّلَوٰةَ وَأَنتُمۡ سُكَٰرَىٰ حَتَّىٰ تَعۡلَمُواْ مَا تَقُولُونَ وَلَا جُنُبًا إِلَّا عَابِرِي سَبِيلٍ حَتَّىٰ تَغۡتَسِلُواْ...﴾
"Enyi mlio amini! Msikaribie Sala, hali mmelewa, mpaka myajue mnayo yasema, wala hali mna janaba - isipo kuwa mmo safarini - mpaka mkoge..." [An-Nisaa: 43].
Basi, atakapotawadha aliye na hadathi kubwa, inajuzu kwake kubakia Msikitini; na vivyo hivyo, inajuzu kwa mwenye hadathi kubwa kupita Msikitini kwa ajili ya kupita tu, bila kukaa ndani yake.
Nne: Adabu za Kukidhi Haja.
Inapendekezwa wakati wa kukidhi haja:
1- Kujitenga na kuwa mbali na watu, na kujificha katika faragha.
2- Kusema dua iliyopokelewa wakati wa kuingia, nayo ni: "Ewe Mwenyezi Mungu hakika mimi najilinda kwako kutokana na mashetani wa kiume na mashetani wa kike."10
Na ni wajibu wakati wa kukidhi haja:
1- Kujisafisha kutokana na mkojo.
2- Kusitiri uchi.
Yaliyoharamu wakati wa Kukidhi Haja:
1- Kuelekea kibla au kuipa mgongo Kibla.
2- Kukidhi haja katika njia za watu na sehemu zao za umma.
3- Kukojoa ndani ya maji yaliyotuwama.
Na ni machukizo wakati wa kukidhi haja:
1- Kugusa dhakari (uume) kwa mkono wa kulia wakati wa kukidhi haja.
2- Kustanji na kutumia mawe kwa mkono wa kulia.
3- Inachukiza kuzungumza, hasa kumtaja Mwenyezi Mungu, wakati wa kujisaidia.
Ya tano: Hukumu za kustanji na kutumia mawe:
Kustanji: Ni kuondoa athari za kilichotoka katika sehemu mbili za kutolea haja kwa maji.
Na kujipangusa: Nako ni kufuta athari za kilichotoka katika njia mbili pasina kutumia maji; kama kwa jiwe na mfano wake.
Masharti ya kile kinachotumika katika kujipangusa kwa mawe:
1- Halali.
2- Awe na twahara.
3- Iwe nadhifu.
4- Lisiwe mfupa au kinyesi cha wanyama.
5- Isiwe kwa kitu kinachoheshimiwa; kama vile karatasi zenye jina la Mwenyezi Mungu Mtukufu.
Inaruhusiwa kutosheka na kujipangusa kwa masharti mawili:
1- Kitu kinachotoka kisivuke sehemu ya kawaida.
2- Kustanji kuwe kwa mawe matatu yanayotakasa, au zaidi.
Sita: Hukumu za Udhu:
Ni lazima kuwa na Udhu katika ibada tatu:
1- Swala ya aina yoyote sawa iwe ya Faradhi au iwe ya Sunna.
2- Kushika msahafu.
3- Kuzunguka Al-kaaba.
Masharti ya udhu:
1- Uislamu.
2- Akili.
3- Kupambanua.
4- Nia: Na mahala pake ni moyoni, na kuitamka ni uzushi, na kila atakayetaka kutawadha basi tayari ameweka nia. Ama kuosha viungo vya udhu kwa nia ya kujipoza au kujitia usafi; si udhu.
5- Kuambatanisha hukumu zake: kuwa asinuie kuikatisha mpaka twahara yake mpaka ikamilike.
6- Kukoma kwa kinachowajibisha udhu, na inavuliwa katika hili: Mwenye tatizo la kutojizuia endelevu, na mwenye damu ya ugonjwa.
7- Kustanji na kujipangusa kabla yake, kwa yule aliyetokwa na mkojo au kinyesi.
8- Kuwa maji ni yenye kutwaharisha, na uhalali wake.
9- Kuondoa kinachozuia kufika kwa maji kwenye ngozi.
10- Kuingia wakati wa Sala kwa mwenye hadathi ya daima.
Mambo ya lazima katika kushika Udhu:
1- Kuosha uso ikiwa ni pamoja na kusukutua na kupandisha maji puani.
2- Kuosha mikono miwili pamoja na viwiko viwili.
3- Kukipaka maji kichwa kizima pamoja na masikio mawili.
4- Kuosha miguu miwili pamoja na fundo mbili.
5- Kupangilia baina ya viungo vya udhu.
6- Kufululiza: Basi asitenganishe baina ya viungo kwa muda mrefu.
Namna ya Kutawadha:
1- Kusema Bismillah.
2- Kuosha viganja viwili mara tatu.
3- Kuosha uso mara tatu, ikiwa ni pamoja na kusukutua na kupandisha maji puani.
4- Kuosha mikono miwili pamoja na viwiko viwili mara tatu, na kuanza kwa mkono wa kulia kisha wa kushoto.
5- Kupaka maji kichwa pamoja na masikio mawili.
6- Kuosha miguu miwili mpaka katika kongo mbili mara tatu, kwa kuanza na mguu wa kulia kisha wa kushoto.
Vyenye kuharibu Udhu:
1- Kile kinachotoka katika njia mbili, kama: Mkojo, na upepo, na haja kubwa.
2- Kitu chenye najisi kinachotoka mwilini kwa wingi.
3- Kuondokwa na akili kwa kulala au vinginevyo.
4- Kugusa utupu wa mbele au wa nyuma bila kizuizi.
5- Kula nyama ya Ngamia.
6- Kuritadi kutoka katika Uislamu, Allah atuepushe sisi na waislamu kutokana na hilo.
Saba: Hukumu za kufuta juu ya khofu mbili au soksi mbili:
1- Khufu: Ni kiatu kinachovaliwa mguuni kilicho tokana na ngozi na mfano wake.
2- Soksi: Ni kile kinachovaliwa mguuni kinacho tengenezwa kwa sufu au pamba na mfano wake.
Masharti ya ufutaji juu ya hizo mbili:
1- Azivae baada ya kukamilika kwa twahara.
2- Kufunika miguu miwili pamoja na fundo mbili.
3- Ziwe khufu au soksi mbili ni twahara.
4- Na iwe upakaji ni katika muda maalumu uliowekwa.
5- Iwe kupangusa ni katika udhu pekee, si katika kuoga.
6- Khofu na mfano wake viwe Halali; iwapo ni vya wizi au hariri kwa wanaume, hairuhusiwi kufuta juu yake, kwa sababu kilichoharamishwa hakitumiwi kupata ruhusa.
Muda wa kupaka:
Kwa mkazi: Mchana na usiku, na kwa msafiri: Siku tatu na usiku wake.
Namna ya ufutaji:
Huloweshwa mkono kwa maji, na hupitishwa mkono ulioloana juu ya Khofu mbili au soksi mbili, kuanzia kwenye vidole vya miguu mpaka mwanzo wa muundi, mara moja.
Venye kuharibu ufutaji
1- Kuisha muda wa kupaka.
2- Kuvua soksi mbili au moja kati ya hizo.
3- Kupatikana kwa hadathi kubwa.
Hukumu ya kufuta juu ya Khofu mbili:
Hakika hiyo ni ruhusa, na kufuta juu ya khufu mbili ni bora zaidi kuliko kuzivua na kuosha miguu miwili; kwa kuchukua ruhusa ya Mwenyezi Mungu Mtukufu, na kwa kuiga Mtume -rehema na amani ziwe juu yake-, na kwa kwenda kinyume na watu wa bid'a.
3- Kufuta juu ya bandeji na plasta za kubandika:
Vibanio vya mifupa: Ni vile vinavyofungwa na kukazwa juu ya mifupa iliyovunjika; iwe ni gipsi au vijiti na vinavyofanana navyo.
Al-‘Asaaib: Ni kile kinachofungwa juu ya jeraha au kuumia kwa kupondwa au jeraha la kuungua; kutokana na kitambaa na mfano wake.
Na kiraka cha dawa: Ni kile kinachobandikwa juu ya majeraha au mapele kwa ajili ya tiba.
Hukumu ya kupangusa juu yake:
Inajuzu: Kukiwa na haja ya kubakia kwake, kwa sharti la kutozidi mahali pa haja.
Hairuhusiwi: Pale ambapo haja ya hilo imekwisha, au ikiwa kuiondoa hakutapelekea mashaka au madhara.
Jinsi ya kufuta juu ya khofu mbili:
Aoshe yaliyo kandokando yake, na afute juu yake kutoka pande zote, Wala hapangusi zaidi ya sehemu ya Udhu.
Nane: Hukumu za Kutumia Udongo katika (Kutayammamu):
Kutayammam: Ni kupangusa uso na viganja viwili kwa udongo, kwa nia ya twahara, kwa namna maalumu.
Hukumu yake:
Ni wajibu kutayamamu badala ya kutawadha na kuoga wakati maji yamekosekana au kutokuwa na uwezo wa kuyatumia.
Hekima ya kuweka sheria yake:
Kutayamamu ni miongoni mwa mambo maalumu kwa Umma wa Muhammadi rehema na amani ziwe juu yake. Wala halikuwa likijulikana katika Umma zilizopita; ni upana wa fadhila za Mwenyezi Mungu Mtukufu juu ya Umma huu, na wema wake kwao.
Hali ambazo zinaruhusiwa kisheria Kutayamamu:
1- Ikiwa maji hayakupatikana, iwe katika makazi au safarini, na akayatafuta maji lakini hakuyapata.
2- Ikiwa ana maji anayoyahitaji kwa ajili ya kupikia na kunywa, basi kama angejitwaharisha kwa maji hayo, ingalidhuru haja yake, hadi akahofia kiu kwa nafsi yake, au kiu ya mwingine, awe mwanadamu au mnyama anayeheshimiwa.
3- Akihofia kupata madhara katika mwili wake kwa kuyatumia maji kwa sababu ya maradhi au kuchelewa kupona.
4- Ikiwa hakuweza kuyatumia maji kutokana na maradhi yasiyomuwezesha kusogea, wala hana wa kumtia udhu, na akahofia asipitwe na wakati wa swala.
5- Akihofia baridi kwa kuyatumia maji, na asipate cha kuyapasha moto, basi atajitwaharisha kwa kutayamamu na ataswali.
Namna ya Kutayammamu:
Ni apige katika udongo kwa mikono yake miwili huku vidole vikiwa vimeachana, kisha apake uso wake kwa ndani ya vidole vyake, na apake viganja vyake kwa vitanga vyake viwili, na aeneze upakaji huo uso wote na viganja vyote.
Mambo yanayoharibu Kutayammamu:
1- Kupatikana maji ikiwa tayamamu ulifanywa kwa sababu ya kuto patikana Maji. Au uwezo wa kuyatumia maji, iwapo tayamamu ilifanywa kwa kukosa uwezo wa kuyatumia.
2- Hubatilika kwa mojawapo ya vinavyobatilisha udhu, au kwa mojawapo ya vinavyolazimisha kuoga, kama Janaba, na Hedhi, na Nifasi.
Hukumu ya asiyeweza kutumia maji wala kutayamamu:
Asiyepata maji wala udongo, au akafikia hali ambayo hawezi kugusisha ngozi yake kwa maji au udongo; basi ataswali kwa mujibu wa hali yake, bila udhu wala tayamamu; kwa kuwa Mwenyezi Mungu haikalifishi (hailazimishi) nafsi ila kwa kadiri ya uwezo wake. Na lau ikikadiriwa kwamba baada ya hapo yakapatikana maji na udongo, au akaweza kuvitumia vyote viwili; basi hatairudia swala aliyoiswali; kwa sababu amefanya aliloamrishwa nalo. Kwa maneno yake Mtukufu:
﴿...فَٱتَّقُواْ ٱللَّهَ مَا ٱسۡتَطَعۡتُمۡ...﴾
"Basi mcheni Mwenyezi Mungu kama mwezavyo" [At-Taghabun: 16] Na kwa kauli ya Mtume, rehema na amani za Mwenyezi Mungu zimshukie, "Ninapo kuamrisheni jambo fulani basi litekelezeni kadira muwezavyo"11.
Faida: Ikiwa alifanya tayammamu kwa sababu ya kupata Janaba kisha akapata maji, basi itamlazimu kuoga.
Tisa: Hukumu za Hedhi na Nifasi:
Kwanza: Hedhi:
Ni damu ya maumbile, hutoka kwenye kina cha mfuko wa uzazi katika nyakati maalum. Na kwa kawaida damu ya Hedhi hutoka katika kila Mwezi Siku Sita au Saba, na huenda ikaongezeka au ikapungua, Na mwezi wa mwanamke hurefuka na kupungua; kulingana na maumbile aliyoyaweka Mwenyezi Mungu.
Hukumu za mwenye Hedhi:
1- Mwenye hedhi haswali wala hafungi wakati wa hedhi yake, na si sahihi kwake kuswali wala kufunga.
2- Mwanamke aliyekuwa na hedhi atalipa swaumu pekee, si swala, atakapotwaharika kutokana na hedhi yake.
3- Hairuhusiwi kwake kuzunguka Nyumba (Al-Ka'ba). Na wala hasomi Qur’ani, Wala hakai msikitini. 4- Na ni haramu kwa mume wake kumwingilia katika tupu mpaka hedhi ikatike, na aoge.
5- Inafaa kwa mume wa mwenye hedhi kujistarehesha naye pasina kufanya tendo la ndoa katika tupu, kama kubusu na kugusa kwa matamanio na mfano wake.
6- Haijuzu kwa mume wake kumtaliki akiwa katika hedhi.
Twahara ni kukatika kwa damu; damu ikikatika basi ametwaharika, na muda wa hedhi yake umemalizika, basi inawajibika juu yake kuoga josho la hedhi. Kisha atafanya yote aliyokuwa amezuiliwa kuyafanya kwa sababu ya hedhi.
Ikiwa mwanamke ataona baada ya twahara maji maji ya kahawia au ya njano, basi asiyatilie maanani.
La pili: Nifasi:
Nayo ni damu ambayo hutolewa na mfuko wa uzazi wakati wa kujifungua na baada yake, nayo ni mabaki ya damu iliyozuiliwa wakati wa mimba.
Na nifasi ni kama hedhi katika yale yanayofaa; kama kustarehe na mke katika sehemu yoyote ya mwili wake isiyokuwa uke.
Na miongoni mwa yaliyo haramu; kama kufanya tendo la ndoa, na kufunga, na kusali, na kutoa talaka, na kuzunguka Al-ka'ba, na kusoma Qur'ani, na kukaa Msikitini. Na uwajibu wa kuoga pale inapokatika damu yake ni kama wa mwenye hedhi.
Anawajibika kulipa swaumu pekee, na si swala; hivyo, halipi swala, kama mwanamke mwenye hedhi.
Wingi wa muda wake ni: Siku arobaini. Ikikatika damu ya mwanamke mwenye nifasi kabla ya siku arobaini, basi nifasi yake imekwisha; ataoga, na ataswali, na atafanya yote aliyozuiliwa kuyafanya kwa sababu ya nifasi.
Sehemu ya pili: Sala:
Kwanza: Hukumu za Adhana na Ikama:
Adhana iliwekwa kisheria katika mwaka wa kwanza wa Hijiria (kuhama kwa Mtume), na sababu ya kusuniwa kwake: ni kwamba, ilipowawia vigumu kwao kuzijua nyakati, wakashauriana juu ya kusimamisha alama ya kuzibainisha, basi Abdallah bin Zaidi radhi za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake akaonyeshwa adhana hii katika ndoto, na wahyi ukaikubali.
Adhana: Ni tangazo la kuingia wakati wa Sala. Ikama: Ni tangazo la kusimamisha swala.
Adhana na Ikama ni faradhi kifaya (wakifanya baadhi inawatosheleza wengine) kwa jamaa ya wanaume katika Swala zilizofaradhishwa. Na hizo mbili ni miongoni mwa alama za Uislamu zilizo dhahiri, basi haijuzu kuacha kuzitekeleza.
Masharti ya Adhana:
1- Muadhini awe mwanamume.
2- Adhana iwe kwa mpangilio.
3- Adhana iwe kwa mfululizo.
4- Adhana iwe baada ya kuingia wakati wa swala. Na miongoni mwa vinavyotolewa katika hilo: Adhana ya kwanza ya Alfajiri na ya Ijumaa.
Sunaa za Adhana:
1- Aweke vidole vyake viwili ndani ya masikio yake.
2- Adhana mwanzoni mwa wakati.
3- Mtu kugeuka kulia na kushoto wakati wa kusema “Hayya ‘ala as-salāh” na “Hayya ‘ala al-falāh”.
4- Awe na sauti nzuri.
5- Kutamka maneno ya adhana kwa utulivu bila kuyarefusha wala kuvuta sauti kupita kiasi.
6- Kusimama mwisho wa kila sentensi ndani yake.
7- Aelekee kibla anapoadhini.
Na Adhana ina maneno kumi na tano, kama alivyokuwa Bilal -Mwenyezi Mungu amridhie- akiadhini kwa hayo mbele ya Mtume -rehema na amani ziwe juu yake- daima.
Matamshi ya Adhana:
Allaahu Akbaru": Mara nne.
"Ash-hadu an laa ilaaha illa llaah" (Ninashuhudia kuwa hapana Mola apasaye kuabudiwa kwa haki isipokuwa Mwenyezi Mungu): Mara mbili.
"Ash-hadu anna Muhammadan Rasuulu llaah" Yaani: Ninashuhudia kuwa Muhammad ni mjumbe wa Mwenyezi Mungu: mara mbili.
"Hayya a'las swalaa" (Njooni kwenye swala): mara mbili,
"Hayya 'alal falaah" Yaani: Njooni kwenye mafanikio: Mara mbili.
Kisha anasema: "Allahu Akbaru" mara mbili.
Kisha ahitimishe kwa (Laa ilaaha illa llaah): mara moja.
Na huongezwa katika adhana ya Alfajiri baada ya: Hayya a'lal falaah: Asswalaatu khairun minan nauum, mara mbili. Yaani: Swala ni bora kuliko usingizi. Kwa kuwa ni wakati ambapo watu mara nyingi huwa wamelala.
Ikama ina matamshi kumi na moja, na yatamkwe kwa haraka, yaani atamke kwa kasi; kwa kuwa ni kwa ajili ya kuwatangazia waliokaribu na waliojiandaa kwa ajili ya swala, basi hakuna haja ya kutamka taratibu.
Na namna yake ni kama ifuatayo:
Allaahu Akbaru" Mara mbili.
"Ash-hadu an laa ilaaha illa llaah" Yaani: Ninashuhudia kuwa hapana Mola apasaye kuabudiwa kwa haki isipokuwa Mwenyezi Mungu: mara moja.
"Ash-hadu anna Muhammadan Rasuulu llaah" Yaani: Ninashuhudia kuwa Muhammad ni mjumbe wa Mwenyezi Mungu: Mara moja.
"Hayya a'las swalaah" (Njooni kwenye swala): mara moja.
"Hayya a'lal falaah" (Njooni kwenye mafanikio): Mara moja.
"Qad-qaamatis swalaatu" Yaani: Swala imesimama: Mara mbili.
Allaahu Akbaru": Mara mbili.
(Laa ilaaha illa llaah): Mara moja.
Inapendekezwa kwa aliyesikia adhana aseme kama anavyosema muadhini, isipokuwa katika (Hayya a'las swalaa) na (Hayya a'lal falaah), hapo atasema: (Laa haulaa walaa quwwata illa billaah). Kisha atamswalia Mtume rehema na amani ziwe juu yake. Kisha atasema baada ya hayo: "Allaahumma rabba haadhihid da'watit taamma, was swalaatul qaaima, aati Muhammadanil wasiilata wal fadhwiila, wab'ath-huu maqaaman mah muudanil ladhii wa a'ttah, innaka laa tukhliful mii'aad."
Tafsiri: Ewe Mwenyezi Mungu Mola wa wito huu uliotimia, na swala iliyosimama, mpe Muhammadi wasiila (daraja) na fadhila, na umfufue nafasi yenye kusifiwa uliyomuahidi, hakika Wewe huvunji miadi.12
Na atasema: "Radhwiitu billaahi Rabban, wabil Islaami diina, wabi Muhammadin Swalla llaahu a'laihi wasallam Nabiyyan" Yaani: Nimeridhia Mwenyezi Mungu kuwa Mola Mlezi, na Uislamu kuwa dini, na Muhammadi (Rehema na amani ziwe juu yake) kuwa Nabii.13
Ni haramu kutoka msikitini baada ya Adhana bila udhuru au nia ya kurejea.
Na wakati wa kukusanya kati ya swala mbili, yatosha adhana moja tu, na ikama moja kwa kila swala.
Ya pili: Nafasi ya Sala na fadhila zake:
Swala ndiyo nguzo yenye kutiliwa mkazo zaidi miongoni mwa nguzo za Uislamu baada ya shahada mbili. Nayo ina nafasi maalumu, ambapo Allah Mtukufu aliifaradhisha juu ya Mtume wake rehema na amani zimshukie usiku aliopandishwa mbinguni, Hivyo, hilo liliashiria utukufu wake, na msisitizo wa uwajibu wake, na cheo chake mbele ya Mwenyezi Mungu Mtukufu.
Na hadithi kuhusu fadhila zake na wajibu wake juu ya kila mtu binafsi ni nyingi mno. Na ulazima wake unajulikana kwa dharura katika Dini ya Uislamu.
Na miongoni mwa yanayoonyesha ulazima wake na kusisitika kwake ni maandiko mengi kutoka katika Kitabu cha Mwenyezi Mungu na Sunnah za Mtume wake, rehema na amani za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake, ikiwa ni pamoja na:
1-Ni kauli ya Mwenyezi Mungu Mtukufu:
﴿...إِنَّ ٱلصَّلَوٰةَ كَانَتۡ عَلَى ٱلۡمُؤۡمِنِينَ كِتَٰبٗا مَّوۡقُوتٗا﴾
"Hakika Sala kwa Waumini ni faradhi iliyo wekewa nyakati maalumu." [An Nisaai: 103]. Yaani: Imefara dhishwa kwa nyakati ambazo Mtume -rehema na amani ziwe juu yake- amezibainisha.
2- Na kauli yake Mtukufu:
﴿وَمَا أُمِرُوا إِلَّا لِيَعْبُدُوا اللَّهَ مُخْلِصِينَ لَهُ الدِّينَ حُنَفَاءَ وَيُقِيمُوا الصَّلَاةَ...﴾
"Nao hawakuamrishwa kitu ila wamuabudu Mwenyezi Mungu kwa kumtakasia Dini, wawe waongofu, na washike Swala..." [Al-Bayyina: 5]
3- Na kauli yake Mtukufu:
﴿فَإِنْ تَابُوا وَأَقَامُوا الصَّلَاةَ وَآتَوُا الزَّكَاةَ فَإِخْوَانُكُمْ فِي الدِّينِ...﴾
"Basi wakitubu na wakashika Swala na wakatoa Zaka, basi ni ndugu zenu katika Dini..." [Tauba: 11].
4- Imepokelewa kutoka kwa Jaabir -radhi za Allah ziwe juu yao yeye na baba yake- kwamba Mtume wa Mwenyezi Mungu -rehema na amani ziwe juu yake- alisema: "Hakika kilicho kati ya mtu na ushirikina na ukafiri ni kuacha swala"14.
5- Kutoka kwa Buraida -radhi za Allah ziwe juu yake- Amesema: Amesema Mtume wa Mwenyezi Mungu -rehema na amani za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake: "Ahadi iliyopo kati yetu na wasiokuwa waislamu ni swala, na atakayeiacha swala basi huyo ni kafiri"15.
Na wamekubaliana wanachuoni juu ya ukafiri wa yeyote atakayekanusha uwajibu wake, ama atakayeiacha kwa uvivu na kuipuuzia, basi kauli sahihi zaidi ni kwamba ni kafiri pia, kwa Hadithi sahihi iliyotangulia, na kwa makubaliano ya Maswahaba juu ya hilo.
Ya tatu: Masharti ya swala:
1- Kuingia wakati wake:
Kwa kauli yake Mtukufu:
﴿...إِنَّ ٱلصَّلَوٰةَ كَانَتۡ عَلَى ٱلۡمُؤۡمِنِينَ كِتَٰبٗا مَّوۡقُوتٗا﴾
"Kwani hakika Swala kwa Waumini ni faradhi iliyo wekewa nyakati maalumu." [An Nisaa]. Yaani: Imefaradhishwa kwa nyakati maalumu.
Na nyakati za Swala za faradhi ni kama ifuatavyo:
A- Alfajiri: Kuanzia kuchomoza kwa Alfajiri hadi kuchomoza jua.
B- Adhuhuri: Kuanzia kupinduka kwa jua mpaka kivuli cha kila kitu kiwe mfano wake kwa urefu.
C- Na wakati wa swala ya Alasiri: Ni toka kuisha kwa wakati wa swala ya Adhuhuri mpaka jua likiwa la njano, (na wakati wa) dharura (kwa ajili ya swala ya Lasiri) ni mpaka kuzama kwa jua.
D- Magharibi: Ni toka kuzama kwa jua mpaka kupotea kwa wekundu unaotokea angani wakati wa kuzama kwa jua.
Na wakati wa swala ya Ishaa: Ni kutoka kuisha wakati wa swala ya Magharibi mpaka nusu ya usiku.
2- Kusitiri uchi:
Nayo ni yale yanayopasa kufunikwa, na haifai yaonekane hadharani, na huonewa aibu kwayo. Uchi wa mwanaume ni kati ya kitovu chake na magoti yake, Na mwili wote wa mwanamke katika sala ni uchi isipokuwa uso wake. Na afunike uso wake anapokuwa mbele ya wanaume wasio maharimu wake; yaani, ambao si maharimu wake.
3- Kuiepuka najisi:
Na Najisi: Ni uchafu mahsusi unaozuia kuswihi kwa swala; kama mkojo, kinyesi, damu na vinginevyo; na huwa mwilini, kwenye eneo, na katika nguo.
4- Kuelekea kibla:
Kibla ni Al-Kaaba tukufu, imeitwa Kibla kwa sababu ya watu kuielekea.
Haisihi swala pasina kukielekea Kibla, Kwa maneno yake Mtukufu:
﴿...وَحَيۡثُ مَا كُنتُمۡ فَوَلُّواْ وُجُوهَكُمۡ شَطۡرَهُ...﴾
"...na popote mnapokuwa zielekezeni nyuso zenu upande huo..." [Al-baqara: 144]
5- Nia:
Kwa lugha: Kusudio; na kisheria: Kuazimia kufanya ibada kwa kujikurubisha kwa Mwenyezi Mungu Mtukufu. Nia mahali pake ni moyoni, kwa hivyo haihitaji kuitamka, bali kufanya hivyo ni uzushi katika dini.
La nne: Nguzo za swala:
Nazo ni nguzo kumi na nne:
Nguzo ya kwanza: Kusimama uwezo ukiwepo:
Kwa maneno yake Mtukufu:
﴿...وَقُومُواْ لِلَّهِ قَٰنِتِينَ﴾
"...na simameni kwa ajili ya Mwenyezi Mungu nanyi ni wenye kunyenyekea." [Al-Baqara: 238]. Na Hadithi ya Imran -radhi za Allah ziwe juu yake- Marfu'u: "Swali ukiwa umesimama, usipoweza basi swali ukiwa umekaa, usipoweza basi ukiwa umelala ubavu"16.
Ikiwa hatoweza kusimama kwa sababu ya maradhi, basi ataswali kulingana na hali yake, akiwa amekaa au akiwa amelalia ubavu. Na mfano wa mgonjwa: Pia hata anayeogopa, na aliye uchi, na anayehitaji kukaa au kulalia ubavu kwa ajili ya matibabu yanayolazimu asisimame. Na vivyo hivyo hupewa udhuru kuacha kusimama anayesali nyuma ya Imamu wa mtaa aliye shindwa kusimama; na ikiwa ataswali akiwa amekaa, basi walio nyuma yake wataswali wakiwa wamekaa kwa kumfuata imamu wao. Inajuzu kuswali swala za sunna kwa kukaa hata kama anaweza kusimama, lakini malipo hayawi kama malipo ya swala ya aliyesimama.
Nguzo ya pili: Takbira ya kufungua swala (Takbiratul ihramu) mwanzoni mwake:
Kwa maneno yake Mtume -rehema na amani ziwe juu yake: «Kisha elekea kibla, na takbiri»17.
Namna yake ni kwamba aseme: "Allahu Ak-bar", na halimtoshelezi neno lolote lisilokuwa hili.
Nguzo ya tatu: Kusoma Suratul Fatiha:
Kwa maneno yake Mtume -rehema na amani ziwe juu yake: "Hana swala yeyote ambaye hakusoma sura kifunguzi cha kitabu (suratul faatiha)"18.
Nguzo ya nne: Kurukuu katika kila rakaa:
Kwa maneno yake Mtukufu:
﴿يَاأَيُّهَا الَّذِينَ آمَنُوا ارْكَعُوا وَاسْجُدُوا...﴾
"Enyi mlio amini! Rukuuni na msujudu..." [Al-Hajj: 77].
Nguzo ya tano na ya sita:
Kunyanyuka kutoka katika rukuu, na kusimama wima kama alivyokuwa kabla yake, kwa kuwa yeye - rehema na amani za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake - alikuwa akidumu kulifanya.
Na amesema Mtume, rehema na amani ziwe juu yake, kumwambia aliyekosea katika swala yake: "Kisha unyanyuke mpaka usimame sawasawa."19
Nguzo ya saba: Kusujudu juu ya viungo saba:
Yaani paji la uso pamoja na pua, na mikono miwili, na magoti mawili, na ncha za miguu miwili. Kwa maneno yake Mtume -rehema na amani ziwe juu yake: "Tumeamrishwa tusujudu kwa viungo saba: Kwa paji la uso, na akaashiria kwa mkono wake katika pua yake, na mikono miwili, na magoti mawili, na ncha za miguu miwili"20.
Nguzo ya nane: Kunyanyuka kutoka katika sijida na kukaa kati ya sijida mbili:
Kwa mujibu wa Hadithi ya Aisha, Mwenyezi Mungu amridhie: "Alikuwa Mtume -rehema na amani ziwe juu yake- anaponyanyua kichwa chake kutoka katika sijida, hakuwa akisujudu mpaka akawa amekaa sawa sawa."21
Nguzo ya tisa: Kutulizana katika nguzo zote:
Nayo ni utulivu hata kama ni kwa kiasi kidogo, na kauli yake Mtume, rehema na amani ziwe juu yake, alipokuwa akimwambia aliyekosea katika swala yake: "Mpaka utulie"(22).22
Nguzo mbili: Ya kumi na ya kumi na moja:
Tashahudi ya mwisho na kikao chake: Kwa mujibu wa hadithi ya Ibn Mas'ud -radhi za Allah ziwe juu yake- iliyonasibishwa kwa Mtume -rehema na amani ziwe juu yake-: "Anaposwali mmoja wenu basi aseme: Attahiyyaatu lillaahi, wasswalawaatu wattwayyibaatu. Assalaamu a'laika ayyuhan nabiyyu, warahmatullaahi wabarakaatuh. Assalaamu 'alainaa wa 'alaa 'ibaadillaahi sswaalihiin. Ash-hadu anlaa ilaaha illa llaahu, wa ash-hadu anna Muhammadan 'abduhu warasuuluhu." Tafsiri yake: Maamkizi (Amani) ni ya Mwenyezi Mungu, na swala na vile vilivyo vizuri. Amani iwe juu yako, ewe Nabii na rehema ya Mwenyezi Mungu na baraka zake. Amani iwe juu yetu na juu ya waja wema wa Mwenyezi Mungu. Ninashuhudia kuwa hapana mungu isipokuwa Mwenyezi Mungu, na ninashuhudia kuwa Muhammadi ni mja wake na ni Mtume wake.23
Nguzo ya kumi na mbili: Kumtakia rehema Mtume rehema na amani ziwe juu yake katika tashahudi ya mwisho:
kwa kusema: «Ewe Mwenyezi Mungu mpe rehema Muhammad»24، Na kinachozidi juu ya hayo ni Sunna.
Nguzo ya kumi na tatu: Kufuatanisha baina ya nguzo:
Kwa sababu Mtume, rehema na amani za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake, alikuwa akifanya kwa mpangilio. Na akasema: "Swalini kama mlivyoniona nikiswali."25 Na yule aliyekosea katika swala yake alifundishwa kwa mpangilio ulioratibiwa kwa kiunganishi "Kisha".
Nguzo ya kumi na nne: Kutoa salamu:
Kwa maneno yake Mtume -rehema na amani ziwe juu yake: "Na mwisho wake ni salamu." Na kauli yake: "Na kuifungua kwake ni salamu"26.
La tano: Wajibu za swala:
Nayo ni mambo manane:
1- Takbira zote isipokuwa takbira ya kuhirimia swala (Ile kuanza swala)
2- Kauli ya: "Sub-haana rabbiyal A'dhwiim" mara moja katika rukuu. Imesuniwa kuongeza hadi mara tatu, nayo ndiyo ukamilifu wa chini kabisa, Na hadi kumi, na ndiyo ukomo wa juu.
3- Kauli ya: "Sami'allaahu liman hamidah" katika kuinuka kutoka katika rukuu; kwa imamu na anayeswali peke yake.
4- Kauli ya: "Rabbanaa walakal hamdu" katika kusi mama sawasawa baada ya rukuu.
5- Kauli ya: "Sub-haana rabbiyal A'laa" mara moja katika sijida. Na inasuniwa kuongeza hadi mara tatu.
6- Kauli ya: "Rabbigh-firlii" kati ya sijida mbili mara moja. Na imesuniwa kuongeza hadi mara tatu.
7- Tahiyatu ya kwanza; nayo ni kusema: "Attahiyyaatu lillaahi, wasswalawaatu wattwayyibaatu, assalaamu a'laika ayyuhan nabiyyu, warahmatullaahi wabarakaatuh, assalaamu a'lainaa wa a'laa ibaadillaahi sswaalihiin, ash-hadu anlaa ilaaha illa llaahu, wa ash-hadu anna Muhammadan 'abduhu warasuuluhu." Tafsiri yake: Maamkizi (amani) ni ya Mwenyezi Mungu, na swala na vile vilivyo vizuri. Amani iwe juu yako, ewe Nabii, na rehema ya Mwenyezi Mungu na baraka zake. Amani iwe juu yetu na juu ya waja wema wa Mwenyezi Mungu. Nashuhudia kuwa hapana Mola isipokuwa Mwenyezi Mungu, na ninashuhudia kuwa Muhammadi ni mja wake na ni mjumbe wake.27
8- Kukaa kwa ajili ya tahiyatu ya kwanza.
Sita: Sunna za swala:
Na Sunna za Swala hazibatilishi Swala kwa kuziacha. Nazo zina sehemu mbili: Sunna za kauli, na Sunna za vitendo.
Kwanza: Sunaa za Kauli:
1- Dua ya ufunguzi wa sala, nayo ina namna, na miongoni mwa hizo ni: (Sub-haanaka llaahumma wabihamdika, watabaarakasmuka, wa ta'alaa jadduka, walaa ilaaha ghairuka) -Kutakasika ni kwako ewe Mola na kushukuriwa ni kwako, limetukuka jina lako, na umetukuka utukufu wako na hakuna Mola mwingine zaidi yako-.28
2- Kuomba kinga kabla ya kusoma suratul faatiha, Nayo ni kusema: "A'udhubillaahi minash-shaitwanir rajiim" Yaani: Ninajikinga kwa Allah kutokana na shetani aliye laaniwa.
3- Bismillah kabla ya kusoma, Ni kusema: "Bismillaahir Rahmaanir Rahiim" yaani: Kwa jina la Mwenyezi Mungu, Mwingi wa rehema, Mwenye kurehemu.
4- Tasbihi ya zaidi ya moja wakati wa kurukuu na kusujudu.
5- Kauli isemwayo zaidi ya mara moja: "Mola wangu nisamehe" Kati ya sijida mbili.
6- Kauli: "Mil-as samaawaati, wamil-al Ardhwi, wamil-amaa baynahumaa, wamil-amaa shiita min shaiin baad" Baada ya kauli: "Rabbanaa walakal hamdu" Mola wetu na sifa njema ni zako. (29)29
7- Kusoma baada ya suratul Faatiha.
8- Kauli: "Allaahumma inni a'udhubika min adhaabi jahannama, wa min adhaabil qabri, wamin fitnatil mahyaa wal mamaati, wamin sharri fitnatil masiihid dajjaali." Ewe Mwenyezi Mungu, hakika mimi ninajilinda kwako kutokana na adhabu za Jahanamu, na adhabu ya kaburi, na fitina za uhai na za kifo, na kutokana na fitina za Masihi Dajali.30 Na kilicho zaidi ya hayo miongoni mwa dua katika tashahudi ya mwisho.
Ya pili: Sunna za vitendo:
1- Kunyanyua mikono mpaka usawa wa mabega au usawa wa masikio katika sehemu nne:
A- Wakati wa takbira ya kuhirimia swala.
B- Wakati wa kurukuu.
C- Wakati wa kunyanyuka kutoka katika kurukuu.
D- Wakati wa kusimama kwa ajili ya rakaa ya tatu.
2- Kuweka kiganja cha mkono wa kulia juu ya kiganja cha kushoto juu ya kifua wakati anapokuwa amesimama, kabla ya rukuu na baada yake.
3- Kutazama mahali pa kusujudia.
4- Kuweka mikono mbali na mbavu wakati wa kusujudu.
5- Kuweka tumbo mbali na mapaja wakati wa sijida mbili.
6- Kukaa mkao wa kukalia mguu wa kushoto na kusimamisha wa kulia (Iftirashi) katika vikao vyote vya swala, isipokuwa katika tahiyatu ya mwisho katika swala za rakaa tatu na rakaa nne.
7- Kukalia kalio la kushoto na kulaza mguu wa kushoto ndani ya mguu wa kulia (Tawaruku) katika tashahudi ya mwisho katika swala ya rakaa tatu au ya rakaa nne.
Saba: Sifa ya Swala:
Alikuwa Mtume rehema na amani ziwe juu yake, anaposimama kuswali, anaelekea kibla, na hunyanyua mikono yake, na upande wa ndani wa vidole vyake huuelekeza kibla, kisha husema: "Allaahu Akbar" Yaani: Mwenyezi Mungu ni mkubwa.
2- Kisha atashika mkono wake wa kushoto kwa mkono wake wa kulia, na ataweka mikono yake juu ya kifua chake.
3- Kisha atasema dua ya ufunguzi wa swala, na wala hakuwa akidumu juu ya dua moja ya ufunguzi wa swala. Basi dua zote za ufunguzi zilizothibiti kutoka kwake, rehema na amani ziwe juu yake, inajuzu kufungulia nazo swala, na miongoni mwazo ni: "Sub-haanaka llaahumma wabihamdika, watabaarakas muka, wa ta'alaa jadduka, walaa ilaaha ghairuka." Yaani: Umetakasika ewe Mwenyezi Mungu, na sifa njema ni zako. Jina lako ni lenye baraka, na utukufu wako ni wa juu sana, wala hakuna mungu mwingine isipokuwa Wewe.
4- Kisha aseme: "A'udhubillaahi minash-shaitwanir rajiim, Bismillaahir Rahmaanir Rahiim" Yaani: Ninajikinga kwa Allah kutokana na shetani aliye laaniwa; Kwa jina la Allah, Mwingi wa rehema, Mwenye kurehemu.
5- Kisha atasoma suratul fatiha, akiimaliza atasema: (aaamiin).
6- Kisha atasoma kiasi anachokiweza katika Qur'ani, Na atasoma kwa sauti kubwa katika swala ya Al-fajiri, na katika rakaa mbili za mwanzo katika swala ya Magharibi na Ishaa. Na atafanya kisomo kwa siri katika swala zisizokuwa hizo. Na atarefusha rakaa ya kwanza ya kila swala iwe ndefu kuliko rakaa ya pili.
7. Kisha atanyanyua mikono yake kama alivyo inyanyua katika takbira ya kuhirimia swala. Kisha atasema: "Allahu Akbaru", Na atainama kwa kurukuu, Na ataweka mikono yake juu ya magoti yake hali ya kutawanya vidole vyake, na kuiweka imara, na atau nyoosha mgongo wake, na ataweka kichwa chake kiwe sambamba na mgongo; asikinyanyue wala kukishusha, na atasema: "Sub-haana Rabbiyal a'laa" Utakasifu ni wa Mola wangu aliye wa juu, mara moja, Na kiwango cha chini cha ukamilifu: Ni mara tatu, kama ilivyotangulia.
8. Kisha atanyanyua kichwa chake huku akisema: "Sami'allaahu liman hamidah" Amemsikia Mwenyezi Mungu mwenye kumhimidi. Na atanyanyua mikono yake kama anavyoinyanyua wakati wa kurukuu.
9- Anaposimama sawa sawa atasema: "Allahumma Rabbanaa walakal hamdu, hamdan kathiira twayyiban mubaarakan fiihi, mil-as samaa’i, wamil-al ardhwi, wamil-a maa baynahumaa, wamil-amaa shi’ita min shaiin baad, Ahluth’thanaa walmajd, ahaqqu maaqaalal ‘abdu, wakulluna laka ‘abdu, laa maani’a limaa a’atwaita, walaa mu’utwiya limaa mana’ata, walaa yanfa’u dhaljaddi minkal jaddu." Yaani: Ewe Mwenyezi Mungu, Mola wetu, sifa njema ni zako, shukrani nyingi nzuri zenye baraka ndani yake, kwa ujazo wa mbingu, na ujazo wa ardhi, na ujazo wa vilivyo baina yao, na ujazo wa chochote ukitakacho baada yake. Unastahiki zaidi sifa njema na utukufu, haya ni maneno ya haki zaidi aliyoyasema mja, nasi sote ni waja wako. Ewe Mwenyezi Mungu, hakuna wa kuzuia uliyoyatoa, wala wa kuyatoa uliyoyazuia, wala hawezi kunufaisha mwenye utukufu (yeyote) kuliko wewe ewe Mtukufu.31 Na alikuwa akirefusha kusimama wima huku.
10- Kisha atatoa takbira na atasujudu, na wala hatonyanyua mikono yake, na atasujudu juu ya paji la uso wake pamoja na pua yake, na mikono miwili, na magoti mawili, na ncha za vidole vya miguu miwili. Na ataelekeza vidole vya mikono yake na vidole vya miguu yake kibla, na awe sawa sawa katika sijida yake, na kuhakikisha paji la uso wake na pua yake kuwa ardhini, na atajiegemeza juu ya viganja vyake, na kunyanyua viwiko vyake, na aweke mbali miundi yake ya mikono na mbavu zake, na atalinyanyua tumbo lake lisiyaguse mapaja yake mawili, na mapaja yake mbali na miundi yake, na atasema kwenye kusujudu kwake: "Sub-haana Rabbiyal a'laa" Utakasifu ni wa Mola wangu aliye wa juu Mara moja, Na ukamilifu wa chini kabisa ni mara tatu, kama ilivyotangulia. Na aombe kwa dua zilizopokelewa.
11- Kisha atanyanyua kichwa chake huku akisema: "Allahu Akbaru". Kisha atatandika mguu wake wa kushoto, na kuukalia, na atasimamisha mguu wake wa kulia, Na ataweka mikono yake juu ya mapaja yake, kisha aseme: "Allahummagh-firlii warhamnii, waj-burnii, wahdinii, warzuq-nii" Yaani: Ewe Mola wangu nisamehe, na unihurumie, na unipe nguvu, na uniongoze, na uniruzuku (32).32
12- Kisha atatoa takbira na atasujudu, na atafanya katika sijida ya pili kama alivyofanya katika sijida ya kwanza.
13- Kisha atanyanyua kichwa chake huku akitoa takbira, na atainuka juu ya sehemu za mbele za nyayo zake, huku akiegemea magoti yake na mapaja yake.
14- Basi anapokuwa amesimama sawasawa; ataanza kisomo, ataswali rakaa ya pili kama ya kwanza.
15- Kisha atakaa kwa ajili ya tahiyatu ya kwanza kama anavyokaa kati ya sijida mbili. Na ataweka mkono wake wa kulia juu ya paja lake la kulia, na mkono wake wa kushoto juu ya paja lake la kushoto. Ataweka kidole gumba cha mkono wake wa kulia juu ya kidole chake cha kati, kama umbo la pete. Na ataashiria kwa kidole chake cha shahada, na atakitazama, na atasema: "Attahiyyaatu lillaahi, wasswalawaatu wattwayyibaatu, assalaamu a'laika ayyuhan nabiyyu, warahmatullaahi wabarakaatuh, assalaamu a'lainaa wa a'laa ibaadillaahi sswaalihiin, ash-hadu anlaa ilaaha illa llaahu, wahdahu laa shariika lahu, wa ash-hadu anna Muhammadan 'abduhu warasuuluhu" Tafsiri yake: Maamkizi (Amani) ni ya Mwenyezi Mungu, na swala na vile vilivyo vizuri, amani iwe juu yako ewe Nabii na rehema ya Mwenyezi Mungu na baraka zake, amani iwe juu yetu na juu ya waja wema wa Mwenyezi Mungu, nashuhudia kuwa hapana Mola apasaye kuabudiwa kwa haki isipokuwa Mwenyezi Mungu, Yeye peke yake hana mshirika, na nina shuhudia kuwa Muhammadi ni mja wake na ni mjumbe wake. Na alikuwa akihafifisha kikao hiki.
16- Kisha atanyanyuka huku akitoa takbira, kisha ataswali rakaa ya tatu na ya nne, na atazifupisha kuliko mbili za mwanzo, Na asome ndani ya rakaa hizo mbili Al-Fatiha.
17- Kisha atakaa mkao wa kulaza mguu katika tashahudi ya mwisho, na tawaruku ni: Kuutandika mguu wa kushoto na kuutoa upande wa kulia, na kuusimamisha wa kulia, na kuweka kalio moja katika ardhi.
18- Kisha atasoma Tahiyatu ya mwisho, nayo ni: Kama Tahiyatu ya kwanza, na atazidisha juu yake: "Allaahumma swalli a'laa Muhammad wa a'laa aali Muhammad, kama swallaita a'laa aali Ibraahiima, Ewe Allah shusha rehema juu ya Muhammad na jamaa zake Muhammad kama ulivyo shusha rehema juu ya jamaa za Ibrahim, hakika wewe ni mwenye sifa tukufu, na shusha baraka juu ya Muhammad na jamaa zake Muhammad kama ulivyo shusha baraka juu ya jamaa za Ibrahim, hakika wewe ni mwenye sifa tukufu.
19- Na atajilinda kwa Mwenyezi Mungu kutokana na adhabu za Jahanamu, na kutokana na adhabu za kaburi, na kutokana na majaribu ya uhai na ya kifo, na kutokana na majaribu ya Masihi Dajali. Na atafanya dua kwa yale yaliyopokelewa miongoni mwa dua katika Qur'ani na Sunna.
20- Kisha atatoa salamu kuliani kwake atasema: (Assalaamu 'alaikum warahmatullaah) Amani iwe juu yenu na rehema za Mwenyezi Mungu. Na kushoto kwake kadhalika; huanza salamu akiwa ameelekea Kibla, na huihitimisha anapokamilisha kugeuka.
Nane: Mambo yanayochukiza katika swala:
1- Kugeuka bila haja.
2- kunyanyua macho juu mbinguni.
3- Kufunga macho bila haja.
4. Kutandika dhiraa (mikono) wakati wa kusujudu.
5- Kujifunika mdomo na pua bila haja.
6- Kuswali wakati wa kuhimili haja ndogo au kubwa, au panapokuwapo chakula anachokitamani.
7- Kupangusa paji la uso wake na pua yake kutokana na athari za kusujudu zilizoshikamana juu yake, na hakuna ubaya wa kupangusa hivyo baada ya kumaliza Swala.
8- Kuegemea ukuta na mfano wake wakati wa kusimama bila uhitaji.
La tisa: Mambo yanayobatilisha swala:
1. Kula na kunywa.
2- Maneno yasiyohusiana nayo.
3- Kucheka na kujikohoza.
4- Kuacha mojawapo ya nguzo zake au mojawapo ya wajibu zake kwa makusudi.
5. Kuzidisha kwa makusudi nguzo au rakaa.
6- Kutoa salamu kwa makusudi kabla ya imamu.
7- Harakati nyingi za kufululiza zisizo katika aina ya swala bila ya haja.
8- Kufanya jambo linalopingana na mojawapo ya masharti ya sala; kama kutengukiwa na udhu, na kudhihirika tupu kwa makusudi, na kugeuka sana kwa mwili kutoka kibla bila dharura, na kukata nia.
Ya Kumi: Sijida ya kusahau:
Kusahau: Ni kughafilika, na bila shaka Nabii rehema na amani ziwe juu yake alisahau katika Swala; kwa kuwa kusahau ni miongoni mwa mambo yanayotokana na tabia ya kibinadamu. Na kusahau kwake kulikuwa miongoni mwa kutimia kwa neema ya Mwenyezi Mungu Mtukufu juu ya umma wake na kukamilika kwa dini yao, ili wamfuate yeye katika yale anayowawekea sheria wakati wa kusahau.
Sababu zinazowekwa kisheria kwa ajili ya Sijida ya Kusahau:
1- Hali ya kwanza:
Kuongeza katika Sala, nayo ni ima ziada ya vitendo au ziada ya kauli:
A- Kuzidisha matendo: Ikiwa kuzidisha huko ni katika swala yenyewe: kama kusimama mahala pa kukaa, na kukaa mahala pa kusimama, au akazidisha kurukuu au kusujudu; basi akifanya hivyo kwa kusahau, atasujudu sijida ya kusahau.
b- Ziada katika kauli: Kama kusoma Qur'ani wakati wa kurukuu na kusujudu,
Na ikiwa atafanya hivyo; itapendekezwa kwake Sijida ya Kusahau.
2- Hali ya pili:
Upungufu katika Swala kwa kusahau, nao huwa kwa moja ya mambo mawili:
A- Kuacha nguzo: Iwapo nguzo hii ni Takbiira ya kuhirimia swala, swala yake haitothibiti, wala sijida ya kusahau haitosaidia. Na ikiwa ni nguzo isiyokuwa Takbira ya kuhirimia swala kama rukuu au sijida, na akakumbuka kabla ya kuanza kusoma katika rakaa nyingine; basi itamlazimu kurudi, na ataileta nguzo hiyo na ya baada yake.
Na ikiwa ataikumbuka baada ya kuanza kusoma katika rakaa nyingine, itakuwa imebatilika ile aliyoiacha, na inakuwa ile inayofuata ni badala yake.
A- Kuacha wajibu: Kama vile: Kusahau tahiyatu ya kwanza, au tasbihi katika rukuu. Basi katika hali hii: Asujudu kwa kusahau.
3- Hali ya tatu: Shaka:
Mfano: Akipata shaka kama kaswali rakaa tatu au nne katika swala ya Adhuhuri, basi katika hali hii:
a- Akipata uhakika wa jambo; basi atalifanyia kazi, na atasujudu sijida ya kusahau.
b- Ikiwa hakuna jambo alilo na uhakika nalo; basi atajenga yakini, na atasujudu sijida ya kusahau.
Ikiwa shaka itakuwa baada ya swala, au ikiwa ni mwenye shaka nyingi; basi asiitilie maanani shaka hiyo.
Faida: Sijida ya kusahau huwa kabla ya salamu: Ikiwa ni kwa upungufu, au kwa shaka bila ya kupata upande wenye uzito. Na huwa baada ya salamu: Ikiwa ni kutokana na ziada, au kwa shaka ambapo amefuata lililo na nguvu zaidi, na swala hili katika hilo ni pana, Mwenyezi Mungu Mtukufu akipenda.
Wa kumi na moja: Nyakati zilizo katazwa kusali:
Asili ni uhalali wa kuswali katika nyakati zote, Lakini Sheria ya Kiislamu imekuja kuharamisha kusali katika baadhi ya nyakati, nazo ni kama ifuatavyo:
1- Baada ya swala ya Alfajiri mpaka jua linapo chomoza, na linyanyuke kiasi cha mkuki kutoka ardhini kwa mtazamo wa jicho.
2- Pindi jua linapofika kati kati ya mbingu mpaka linapoondoka kutoka kati kati ya mbingu, nao ndio muda mfupi zaidi miongoni mwa nyakati za katazo.
3- Toka swala ya Alasiri mpaka lizame Jua, na huo ndio mrefu zaidi miongoni mwa nyakati zilizokatazwa kusali.
Swala ambazo inafaa kuzifanya katika nyakati zilizokatazwa kusali:
1- Kulipa Faradhi zilizopita wakati wake.
2- Swala zenye sababu, kama vile: Swala ya Tahiyyatul-Masjid (salamu ya msikiti), rakaa mbili za Tawafu, Swala ya Kusuf, na Swala ya Jeneza.
3- Kulipa sunna ya Alfajiri baada ya swala ya Alfajiri.
Kumi na mbili: Swala ya jamaa:
Nayo ni alama adhimu miongoni mwa alama za Uislamu, nayo ni Swala ya pamoja katika misikiti, Waislamu wameafikiana kwamba kutekeleza swala tano katika misikiti ni miongoni mwa amali za utiifu zilizo na msisitizo mkubwa zaidi, na ni miongoni mwa amali kubwa zaidi za kujikurubisha kwa Allah, bali yenyewe ndiyo alama kubwa zaidi za Uislamu.
1- Hukumu ya Swala ya jamaa:
Na Swala ya pamoja ni wajibu msikitini kwa Swala tano, kwa wanaume wenye uwezo. Nyumbani na Safarini, Katika hali ya amani na katika hali ya hofu, ni wajibu kwa kila mtu.
Na ushahidi unaothibitisha ulazima wa Swala ya Jamaa ni: Qur'ani na Sunna, na matendo ya Waislamu karne baada ya karne, kizazi baada ya kizazi.
Ama ushahidi katika Qur'ani ni maneno yake Mwenyezi Mungu Mtukufu:
﴿وَإِذَا كُنتَ فِيهِمۡ فَأَقَمۡتَ لَهُمُ ٱلصَّلَوٰةَ فَلۡتَقُمۡ طَآئِفَةٞ مِّنۡهُم مَّعَكَ...﴾
"Na unapokuwa pamoja nao, ukawasalisha, basi kundi moja miongoni mwao wasimame pamoja nawe..." [An-Nisaa: 102]. Na Aya hii inaonyesha kwamba uwajibu wa swala ya jamaa umesisitizwa, ambapo hawakuruhusiwa Waislamu kuiacha katika hali ya hofu, basi lau isingekuwa wajibu; udhuru unao stahiki zaidi kwa kuondoka kwake ungekuwa udhuru wa hofu. Kuacha swala ya jamaa na kuzembea kuihudhuria ni miongoni mwa sifa mashuhuri za wanafiki.
Na katika mafundisho ya Mtume rehema na amani ziwe juu yake: Zimekuja Hadithi nyingi, ikiwa ni pamoja na:
Yaliyokuja katika Sahihi Muslim Mtu mmoja kipofu alimwambia Mtume -rehema na amani ziwe juu yake-: Ewe Mjumbe wa Mwenyezi Mungu, sina muongozaji wa kunileta msikitini, akamuomba amruhusu asali nyumbani kwake, akamruhusu, alipoondoka akamuita akasema: "Je, unasikia wito wa swala?" Akasema: Ndiyo, akasema: "Basi ujibu".33
Basi Mtume rehema na amani ziwe juu yake akamwamuru kuhudhuria msikitini kwa swala ya jamaa na kuitikia wito wa swala, hata ni kipofu na pamoja na tabu anazokutana nazo. Hivyo, dalili hiyo imeonyesha kwamba Swala ya jamaa ni ya lazima.
2-Kinachofanya kuipata Swala ya jamaa:
Jamaa hupatikana kwa kuipata rakaa moja ya swala pamoja na imamu. Kwa kauli yake Mtume -rehema na amani ziwe juu yake: "Mwenye kuipata rakaa moja ya swala basi kwa hakika atakuwa ameipata swala"34.
3- Kinachofanya kuipata rakaa:
Kuipata rakaa kunakuwa kwa kuikuta rukuu, pindi mfuataji aliyechelewa akimkuta imamu wake yuko katika rukuu: basi ni wajibu atoe takbira ya kuhirimia swala akiwa amesimama, kisha arukuu huku akitoa takbira mara nyingine kwa ajili ya rukuu. Na ikiwa ataishia tu katika Takbiiratul Ihraam wakati wa kisimamo chake, itamtosheleza badala ya Takbira ya rukuu.
4- Dharura zinazoruhusu mtu kuacha Swala ya jamaa:
1- Maradhi, ikiwa kuhudhuria Ijumaa na sala ya jamaa kunaleta tabu.
2- Kuzuia mkojo au haja kubwa; kwa kuwa kuzuia huko husababisha kupotea kwa khushuu (utulivu) katika swala, na kunaleta madhara kwa mwili.
3- Uwepo wa chakula na mtu akiwa na njaa au nafsi yake ikitamani chakula, mradi tu isifanywe ada wala hila ya kukwepa kuhudhuria Swala ya jamaa.
4- Uoga usio na shaka juu ya nafsi au mali au vinginevyo.
Kipengele cha kumi na tatu: Swala ya hofu:
Swala ya hofu imewekwa kisheria katika kila kupigana kunakoruhusiwa kisharia, kama kupigana na wale waliokufuru, na waasi, na wanyang’anyi wa barabarani, kwa maneno yake Mwenyezi Mungu Mtukufu:
﴿...إِنۡ خِفۡتُمۡ أَن يَفۡتِنَكُمُ ٱلَّذِينَ كَفَرُوٓاْ...﴾
"...iwapo mnachelea wasije wale walio kufuru wakakuleteeni maudhi..." [An-Nisaa: 101] Na pima kwa hilo waliobaki miongoni mwa wale wanaojuzu kupigana nao vita.
Na Swala ya hofu imewekwa kisheria kwa masharti mawili:
La kwanza: Adui awe ni yule ambaye imehalalishwa kupigana naye.
2) Kuhofiwa shambulizi lake dhidi ya Waislamu wakati wa swala.
Jinsi ya kuswali Swala ya hofu:
Ina namna nyingi; zilizo mashuhuri zaidi ni kama ilivyopokelewa katika hadithi ya Sahl, Mwenyezi Mungu amridhie: Kundi moja liliunga safu pamoja na Mtume, na kundi jingine likawaelekea maadui; akawaswalisha wale waliokuwa pamoja naye rakaa moja, kisha wakabaki wamesimama na wakakamilisha swala wao wenyewe, kisha wakaondoka, na wakaunga swafu wakiwaelekea maadui; na likaja kundi jingine, Mtume akawaswalisha rakaa iliyobakia katika swala yake, kisha Mtume akabakia amekaa, na wao wakakamilisha wenyewe, kisha akawatolesha salamu.35
Na tunafaidika kutokana na Swala ya hofu:
1- Umuhimu wa swala katika Uislamu, na umuhimu wa swala ya jamaa, kwani haikuondolewa hata katika hali hizi za dharura.
2- Kuondolewa uzito kwa umma huu, na urahisi wa sheria na kufaa kwake kwa kila zama na mahali.
Ukamilifu wa sheria ya Uislamu, na kwamba imeweka kwa kila hali hukumu zinazoiendana nayo.
La kumi na nne: Swala ya Ijumaa:
Kwanza: Hukumu yake:
Swala ya Ijumaa ni faradhi ya lazima, kwa kila Muislamu mwanamume aliyebaleghe mwenye akili timamu mkaazi asiye na udhuru.
Kwa maneno yake Mtukufu:
﴿يَٰٓأَيُّهَا ٱلَّذِينَ ءَامَنُوٓاْ إِذَا نُودِيَ لِلصَّلَوٰةِ مِن يَوۡمِ ٱلۡجُمُعَةِ فَٱسۡعَوۡاْ إِلَىٰ ذِكۡرِ ٱللَّهِ وَذَرُواْ ٱلۡبَيۡعَۚ ذَٰلِكُمۡ خَيۡرٞ لَّكُمۡ إِن كُنتُمۡ تَعۡلَمُونَ 9﴾
"Enyi mlio amini! Ikiadhiniwa Swala siku ya Ijumaa, nendeni upesi kwenye dhikri ya Mwenyezi Mungu, na wacheni biashara. Hayo ni bora kwenu, lau kama mnajua." [Al-Jumu'a: 9].
Na kwa kauli ya Mtume, rehema na amani za Mwenyezi Mungu zimshukie: "Kwa hakika ima wakome watu kuziacha swala za Ijumaa, au Mwenyezi Mungu atawapiga mihuri juu ya mioyo yao, kisha kwa hakika watakuwa ni miongoni mwa walioghafilika"36.
Ya pili: Masharti ya kusihi kwenye Swala ya Ijumaa:
A- Wakati: Na wakati wake ni kama wakati wa Swala ya Adhuhuri, Haisihi kabla ya wakati wake, wala baada ya kutoka wakati wake.
1) Kuhudhuria pamoja na jamaa, na kiwango cha chini cha jamaa ni watu watatu kwa kauli iliyo sahihi. Haikubaliki kwa aliye peke yake, wala kwa watu wawili.
(3) Wawe waswalio ni wakazi wa kudumu katika makazi yaliyojengwa kwa vifaa vya ujenzi vilivyozoeleka. sawa sawa yawe yametengenezwa kwa zege iliyo imarishwa kwa nondo, au kwa mawe, au kwa udongo, na vinginevyo, na hivyo basi, si sahihi kwa watu wa majangwani, wenye mahema na nyumba za manyoya, ambao hawafanyi makazi ya kudumu mahali maalumu, bali huhamahama na hufuata malisho ya mifugo yao.
4- Itanguliwe na hotuba mbili, kwa kuwa Mtume rehema na amani ziwe juu yake alidumu kuzitekeleza.
La tatu: Nguzo za hotuba mbili za Ijumaa:
1- Kumhimidi Mwenyezi Mungu na shahada mbili.
2- Kumsalia Mtume rehema na amani za Allah ziwe juu yake.
3- Usia wa kumcha Mwenyezi Mungu.
4- Kusoma sehemu ya Qur'ani.
5- Mawaidha.
Nne: Mambo yanayopendekezwa kwenye hotuba mbili za Ijumaa:
1. Hotuba kwenye mimbari.
2- Kutenganisha kati ya hotuba mbili kwa kikao kifupi.
3- Kuwaombea katika hotuba mbili hizo Waislamu na viongozi wao.
4- Kuzifupisha.
5- Salamu ya khatibu kwa watu anapopanda mimbari.
Tano: Mambo yanayopendeza siku ya ijumaa:
1- Kupiga mswaki.
2- Kushika marashi iwapo yapo.
3- Kuwahi mapema kutoka kwa ajili ya Swala ya Ijumaa.
4- Kutembea kwa miguu wakati wa kwenda msikitini na kutopanda kipando.
5- Kumkaribia imamu.
6- Dua.
7- Kusoma suratul kahf.
8- Kumswalia Mtume rehema na amani ziwe juu yake.
Sita: Mambo yanayokatazwa kwa anayehudhuria Swala ya Ijumaa:
1- Uharamu wa kuzungumza siku ya Ijumaa wakati imamu akihutubu, kwa kauli yake rehema na amani ziwe juu yake: "Utakapomwambia mwenzako: Nyamaza, siku ya Ijumaa, na imamu akihutubu, basi utakuwa umefanya mchezo."37 Yaani: Umesema upuuzi, na upuuzi: Ni dhambi.
2- Inachukiza kupita juu ya shingo za watu, isipokuwa akiwa ni Imamu, au kupita kwenda kwenye pengo ambalo hawezi kulifikia ila kwa kufanya hivyo.
Kuwahi Swala ya Ijumaa:
Mwenye kuipata rukuu pamoja na Imamu katika rakaa ya pili ya swala ya Ijumaa, basi kwa hakika atakuwa ameidiriki (ameipata) swala ya Ijumaa, na ataikamilisha na kuwa rakaa mbili. Na ikiwa hakupata rukuu ya rakaa ya pili, basi atakuwa ameikosa swala ya Ijumaa, na ataikamilisha kama Dhuhuri rakaa nne, Na vivyo hivyo, aliyekosa swala ya Ijumaa kwa usingizi au kwa sababu nyingine; huyo ataswali Adhuhuri.
Kumi na tano: Swala za watu wenye dharura:
Ya kwanza: Swala ya mgonjwa:
Kwanza: Ni wajibu kwa mgonjwa kuitekeleza swala kwa kadiri ya uwezo wake. Wala hairuhusiwi kwake kuichelewesha swala nje ya wakati wake maadamu akili yake iko timamu.
Pili: Ni namna gani anaswali mgonjwa?
1. Ni wajibu kwa mgonjwa kuswali akiwa amesimama ikiwa anaweza kusimama bila ya tabu wala madhara, na atarukuu na atasujudu.
2- Ikiwa atadhurika kwa kurukuu au kusujudu pamoja na kuwa na uwezo wa kusimama; basi ataashiria kurukuu akiwa amesimama, na kusujudu akiwa amekaa.
3- Ikiwa hatoweza kuswali akiwa amesimama, basi ataswali akiwa amekaa, na sunna ni kwamba aketi katika sehemu ya kusimama akiwa amekunja miguu yake, na ataashiria kwa kurukuu, na atasujudu juu ya ardhi ikiwa itawezekana, la sivyo ataashiria kwa kusujudu, na kunakuwa kuashiria kwake kwa kusujudu kumeinama zaidi kuliko kuashiria kwake kwa kurukuu.
4- Ikiwa hatoweza kuswali akiwa amekaa; ataswali kwa ubavu wake, na uso wake upande wa kibla, na ubavu wa kulia ndio bora ikiwa itawezekana, na ataashiria kwa kichwa chake kurukuu na kusujudu.
5- Ikiwa hatoweza kuswali kwa ubavu wake, basi ataswali chali (kwa kulalia mgongo), na miguu yake ikielekea kibla, na ataashiria kwa kurukuu na kusujudu.
6- Ikiwa hatoweza kuashiria kwa mwili wake katika rukuu na sijida, ataashiria kwa kichwa chake; na ikawa ni tabu kwake, basi kuashiria hakutamlazimu, na atayafanya matendo ya Swala kwa moyo wake, hivyo atanuia matendo ya Swala ya rukuu, sijida na kukaa huku akiwa katika hali yake hiyo, na ataleta adhkari zake.
7- Mgonjwa hutekeleza katika masharti ya swala yale anayoyaweza, kama vile: kuelekea kibla, kutia udhu kwa maji, au kutayamamu anapokuwa hawezi, na kuondoa najisi; na akishindwa jambo lolote miongoni mwa hayo, huondoka ulazima juu yake, na ataswali kulingana na hali yake, wala asichelewesha swala ikatoka katika wakati wake.
8- Sunna ni kwamba mgonjwa akae mkao wa kukunja miguu yote katika sehemu ya kusimama na rukuu, na katika mengineyo akae iftirashi (kukalia mguu wa kushoto na kuusimamisha wa kulia).
Ya pili: Swala ya Msafiri:
1- Na miongoni mwa watu wenye dharura: Msafiri; hivyo imewekwa sheria kwake kupunguza swala yenye rakaa nne, kutoka rakaa nne hadi rakaa mbili, Kwa maneno yake Mtukufu:
﴿وَإِذَا ضَرَبۡتُمۡ فِي ٱلۡأَرۡضِ فَلَيۡسَ عَلَيۡكُمۡ جُنَاحٌ أَن تَقۡصُرُواْ مِنَ ٱلصَّلَوٰةِ...﴾
"Na mnapo safiri katika nchi si vibaya kwenu kama mkifupisha Swala..." [An-Nisaa: 101].
Kutoka kwa Anas bin Malik -radhi za Allah ziwe juu yake- amesema: "Tuliondoka pamoja na Mtume, rehema na amani ziwe juu yake, kutoka Madina kwenda Makka, akawa anaswali rakaa mbili mbili, mpaka tuliporejea Madina."38
Huanza kupunguza swala msafiri atakapokuwa ametoka katika makazi ya mji wake; kwa sababu Mwenyezi Mungu ameruhusu kupunguza swala kwa anayesafiri katika ardhi, kabla ya kutoka katika mji wake, hatakuwa mwenye kupiga mwendo katika ardhi wala msafiri; na kwa kuwa Mtume, rehema na amani ziwe juu yake, hakupunguza swala zenye rakaa nne kuwa rakaa mbili isipokuwa pale alipoondoka kuanza safari.
2- Masafa ambayo, msafiri akikusudia kuyakata, yafaa kwake kupunguza swala ni takribani kilomita themanini.
3. Na msafiri anaruhusiwa kufupisha Swala wakati wa kurudi kwake hadi aingie kwenye mji wake alikotoka.
4- Ikiwa msafiri atafika katika mji fulani na akataka kukaa humo; basi ana hali tatu:
A) Akikusudia kukaa zaidi ya siku nne; inampasa kukamilisha swala kuanzia siku ya kwanza alipotulia, na wala hatatumia ruhusa za safari.
b) Akiwa amenuia kukaa siku nne au pungufu yake; basi inafaa kwake kupunguza Swala na kutumia ruhusa za safari.
c. Asikusudie kukaa kwa muda maalumu ulio bainishwa; bali anaweza kubaki siku moja au siku kumi kulingana na kufaa kwa mahali hapo kwake, au ana haja ya matibabu au ahadi na daktari; na pindi haja yake inapokamilika hurudi nchini kwake. Hivyo, msafiri huyu inafaa kwake kupunguza Swala na kuchukua ruhusa za safari hadi atakaporejea, hata kama muda wa kukaa kwake utazidi siku nne.
5. Ikiwa msafiri ataswali nyuma ya imamu mkazi, ni wajibu kwake akamilishe swala bila kufupisha, hata kama hakumkuta isipokuwa katika Tashahudi ya mwisho.
6. Ikiwa mkazi ataswali nyuma ya msafiri anaye punguza swala, basi ni wajibu kwa mkazi akamilishe swala yake baada ya imamu kutoa salamu.
Kumi na sita: Swala ya Iddi mbili:
Sikukuu za Waislamu ni sikukuu za Kiuungu, zilizo idhinishwa kwao na Mwenyezi Mungu Mtukufu, wala hawakuzitunga wao, hawana ila Iddi mbili tu, nazo ni: Iddil Fitri na Iddil Adh-ha. Kinyume na sikukuu za makafiri au sikukuu za uzushi ambazo Allah Mtukufu hakuziweka katika sheria wala hakuziamuru; bali wao wenyewe ndio waliozitunga kutoka katika nafsi zao.
Hukumu ya Swala za Idi mbili:
Faradhi kifaya (ya kujitosheleza); Mtume -rehema na amani ziwe juu yake- alidumu kuitekeleza, na Makhalifa waongofu -radhi za Mwenyezi Mungu ziwe juu yao wote- nao wakadumu kuitekeleza, nayo ni miongoni mwa nembo za Uislamu na alama zake za wazi.
Wakati wa Swala ya Iddi mbili: Unaanza jua linapo nyanyuka kiasi cha mkuki; yaani: baada ya robo saa takribani tangu kuchomoza jua, na unamalizika wakati wa kupinduka jua.
Sifa ya Sala ya Idd mbili:
1- Katika rakaa ya kwanza ataleta Takbira ya kuhirimia, kisha atasoma dua ya ufunguzi wa sala, kisha ataleta takbira mara sita, akiinua mikono yake pamoja na kila takbira, na atamhimidi Mwenyezi Mungu na kumsifu, na amswalie Mtume, rehema na amani za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake, kati ya takbira hizo; kisha ataomba kinga kwa kusema (audhubillahi minash-shaitwaanir-rajiim), na atasema (Bismillaahir Rahmanir Rahiim), kisha ataanza kusoma.
2- Ataleta takbira katika rakaa ya pili baada ya takbira ya kuhama takbira tano, kisha ataomba kinga na atasema Bismillahir-Rahmanir-Rahim, na aanze kusoma. Na inapendekezwa asome katika rakaa ya kwanza baada ya Al-Fatiha suratul-A‘laa, na katika rakaa ya pili suratul-Ghaashiyah.
3- Akitoa salamu imamu, atapanda mimbari, kisha atahutubu hotuba mbili, na atakaa kidogo kati ya hotuba mbili, kama ilivyo katika hotuba ya Ijumaa.
Sunna za Idi:
A- Kuoga.
B- Kujisafisha na kujipulizia manukato.
C- Kula kabla ya kutoka kwenda kuswali Eidil Fitri, na kula baada ya kuswali katika Eidil Adh-ha kutoka katika kichinjo chake ikiwa ana kichinjo.
C- Kutoka kwa miguu.
E- Kwenda kwa njia moja, na kurudi kwa njia nyingine.
Kuwahi mapema katika eneo la kuswalia kwa maamuma pasina imam.
Takbira:
Ni sunna kuleta Takbira katika siku mbili za Eid mbili, na katika siku kumi za Dhul-Hija, na katika siku za Tashriiq (kubanika nyama); nayo ina aina mbili:
Aina ya kwanza: Takbira za moja kwa moja: Nazo ni zile ambazo hazikufungamanishwa na wakati maalumu.
1- Takbira katika Idd ya kufungua (Iddil fitiri): Kuanzia kuzama kwa Jua usiku wa Idd, mpaka kuanza kwa Swala ya Idd.
2- Katika Idd ya Adh-ha: Tangu kuzama kwa jua usiku wa siku ya kwanza ya Dhul-Hijja mpaka kuzama kwa jua katika siku ya mwisho ya siku za Tashriiq (kubanika nyama).
Aina ya pili: Takbira zenye mipaka: Nazo ni zile zinazofungamanishwa na baada ya swala za faradhi.
1- Asiye katika ihram: Kuanzia asubuhi ya siku ya Arafa mpaka siku ya mwisho ya kutanda Nyama.
2- Mwenye Ihram: Kuanzia swala ya Adhuhuri ya siku ya Idd mpaka swala ya Lasiri ya siku ya mwisho ya kutanda Nyama.
Kumi na saba: Swala ya kupatwa Jua:
Maana ya kupatwa kwa Mwezi na Jua:
Kupatwa kwa Mwezi: Ni kufutika mwangaza wa mwezi au baadhi yake usiku.
Na Kupatwa kwa Jua: Ni kupotea kwa mwanga wa jua au baadhi yake wakati wa mchana.
Hukumu ya Swala ya kupatwa kwa Jua:
Ni Sunna iliyotiliwa mkazo; na dalili juu ya hilo ni kitendo cha Mtume -rehema na amani ziwe juu yake- kwani aliiswali wakati jua lilipopatwa katika zama zake. Kama ilivyothibitishwa na amri yake kwayo, na makubaliano ya wanachuoni kwamba ni jambo lililo katika sheria.
Muda wake:
Kuanzia mwanzo wa kupatwa jua au mwezi mpaka kuachiwa; na kuachiwa huko ni kuondoka kwa kupatwa jua au mwezi.
Namna yake:
Idadi ya rakaa zake ni rakaa mbili, na katika rakaa hizo mbili atasoma kwa sauti, na namna yake ni kama ifuatavyo:
A- Ataleta takbira ya kuingia katika swala, na atasoma du'a ya kufungua, na ataomba kinga, na atasoma bismillahi, na atasoma Al-Fatiha, kisha atarefusha kisomo.
B- Kisha atarukuu rukuu ndefu.
C- Kisha atainuka kutoka katika rukuu, na atasema: "Samiallahu liman hamidahu", kisha atasoma Al-Fatiha, kisha atasoma kwa kurefusha kisomo, lakini kifupi kuliko kile cha kwanza.
D- Kisha atarukuu rukuu ndefu, lakini itakuwa fupi kuliko rukuu ya kwanza.
E- Kisha atanyanyuka kutoka katika rukuu, akisema: "Sami'allaahu liman hamidah" (Amemsikia Mwenyezi Mungu mwenye kumhimidi).
Na- Kisha atasujudu sijida mbili ndefu.
z- Kisha atanyanyuka kwa ajili ya rakaa ya pili, nayo ni kama rakaa ya kwanza, lakini ni fupi kuliko ya kwanza.
Suna zake:
(a)- Wito wake kwa kusema: (Asswalaatu Jaami’a)
(b) Iswaliwe katika kundi.
(c)- Kurefusha katika Swala kwa kisimamo chake, rukuu yake, na sijida yake.
(d)- Inatakiwa rakaa ya pili iwe fupi kuliko ya kwanza.
(e)- Mawaidha baada yake, na himizo la kufanya matendo ya utiifu na kuyaacha maovu.
(f)- Kukithirisha dua, na kuomba kwa unyenyekevu, na kuomba msamaha kwa Mwenyezi Mungu, na kutoa sadaka.
Kumi na nane: Swala ya kuomba Mvua:
(1) Kuomba mvua: Ni kuomba kunyeshelezewa na Mwenyezi Mungu Aliyetukuka kwa kuiteremsha mvua wakati wa ukame.
Wakati wa kusuniwa kwa Swala ya kuomba Mvua:
Imewekwa kisheria kuswali Swala ya kuomba Mvua iwapo ardhi imekumbwa na ukame, Mvua imezuilika, na madhara yametokea kutokana na kukosekana kwake; basi hawana budi ila kujinyenyekea kwa Mola wao, wamuombe awateremshie Mvua, na wamuombe nusura kwa aina mbalimbali za unyenyekevu.
A- Mara nyingine kwa kuswali kwa pamoja, au mmoja mmoja.
B- Na mara nyingine kwa dua katika hotuba ya ijumaa, muhutubu ataomba dua, na Waislamu wataitikia dua yake.
C- Na wakati mwingine kwa kuomba dua wakati wowote, bila swala wala hotuba.
Hukumu ya Swala ya kuomba Mvua:
Ni Sunna iliyokokotezwa pale inapopatikana sababu yake, kwa kitendo cha Mtume rehema na amani ziwe juu yake, kama ilivyo katika hadithi ya Abdullah bin Zaidi, radhi za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake, amesema: "Alitoka Mtume, rehema na amani ziwe juu yake, kuelekea uwanja wa kuswalia, akaomba mvua, akaelekea kibla, akageuza shuka lake, na akasali rakaa mbili."39
Sifa ya Swala ya kuomba Mvua:
Sifa ya Swala ya kuomba Mvua katika mahali pake ni kama Swala ya Idd. Na ni sunna kuiswali katika mswala kama Swala ya Eid, na hukumu zake ni kama hukumu za Swala ya Eid; katika idadi ya rakaa, na kusoma kwa sauti, na kwamba inasaliwa kabla ya hotuba, na katika takbira za ziada katika rakaa ya kwanza na ya pili kabla ya kusoma, kama ilivyokwisha kubainishwa katika Swala ya Iddi Mbili. Na atatoa hotuba moja.
La kumi na tisa: Hukumu za jeneza:
Kwanza: Kwa yule anayehudhuria mtu anayekaribia kufa:
1- Imeamrishwa kumtamkisha shahada mtu anaye karibia kufa ya: "Laa ilaaha illa llaah" Hakuna mungu apasaye kuabudiwa kwa haki ila Mwenyezi Mungu.
2- Na ni Sunna aelekezwe kibla.
3- Na inapendekezwa kufunga macho yake.
4. Na ni sunna kumsitiri maiti kwa nguo baada ya kufariki kwake.
5- Yapasa kuharakisha katika kumwandaa maiti.
6- Na ni wajibu kuharakisha kukidhi madeni yake.
7- Maiti huoshwa na huvikwa sanda, na vyote viwili ni faradhi ya kifaya.
Ya pili: Hukumu za Swala ya maiti:
Hukumu yake: Faradhi ya kifaya.
Sharti zake:
(1) Kuelekea kibla.
(2) Kusitiri uchi.
(3)- Kuiepuka najisi.
(4) Twahara ya mwenye kuswali na anayeswaliwa.
(5) Uislamu wa anayeswali na anayeswaliwa.
(6) Kuhudhuria jeneza ikiwa yupo mjini.
(7) Awe mwenye kuwajibika kisheria.
Nguzo zake:
(1) Kusimama ndani yake.
(2) Takbira nne.
(3) Kusoma Suratul Fatiha.
(4) Kumswalia Mtume rehema na amani ziwe juu yake.
5- Kumuombea dua maiti.
(6) Mpangilio.
(7) Kutoa salamu.
Sunna zake:
(1) Kunyanyua mikono pamoja na kila takbira.
(2) Kuomba kinga.
(3) Kuomba kwa ajili ya nafsi yake na kwa Waislamu.
(4) Kusoma kwa sauti ya chini.
(5)- Kusimama kwa muda mfupi baada ya takbira ya nne na kabla ya kutoa salamu.
(6) Kuweka mkono wa kulia juu ya kushoto juu ya kifua.
(7) Kugeuka kulia wakati wa kutoa salamu.
Sifa yake:
Imamu na mtu mmoja mmoja asimame upande wa kifua cha mwanaume na katikati ya mwanamke, na alete Takbiiratul Ihraam, na aombe kinga kwa kusoma Audhubillah, wala hatosoma Dua ya ufunguzi wa swala, na ataje jina la Mwenyezi Mungu (Bismillaah), na asome suratul Faatiha.
Kisha atafanya takbira, na amswalie Mtume, rehema na amani za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake, kisha atafanya takbira, na ataomba dua kwa ajili ya maiti kwa yale yaliyopokelewa; Kama kauli yake Mtume -rehema na amani ziwe juu yake: "Allaahummagh-fir lihayyinaa wamayyitinaa, waswaghiirinaa wakabiirina, wa dhakarinaa wa unthaanaa, wa shaahidinaa wa ghaa ibinaa, Allaahumma man Ahyaitahu minnaa fa ahyihi a'lal iimaan, waman tawaffaitahu minnaa fatawaffahu a'lal Islaam, Allaahumma Laa tahrimnaa ajrahu, walaa tudhwillanaa ba'dahu" Tafsiri: "Ewe Mwenyezi Mungu, msamehe aliye hai katika sisi na aliyekufa, na mdogo wetu na mkubwa wetu, na mwanamume kati yetu na mwanamke, na aliyepo na asiyekuwepo. Ewe Mwenyezi Mungu, unayemueka hai kati yetu, basi mweke hai katika Iman, na uliyemfisha miongoni mwetu, basi mfishe katika Uislamu. Ewe Mwenyezi Mungu, usitunyime thawabu zake wala usitupoteze baada yake" (40).40
Na kauli yake: "Allaahummagh-fir lahuu warhamhu, wa aafihi wa afu anhu, wa akrim nuzulahu, wawas si'mud-khalahu, wagh-silhu bil maai wath-thalji wal-baradi, wanaqqihi minal-khatwaayaa kamaa naqqaitath-thaubal abyadh minad-danasi, wa abdil-hu daaran khairan min daarihi, wa ahlan khairan min ahlihi, wa zaujan khairan min zaujihi, wa adkhil-hul Jannata, wa aidh-hu min adhaabil-qabri, wa min adhaabin-naari" Tafsiri: Ewe Mwenyezi Mungu, msamehe na umrehemu, na umpe salama na umwachie, na mtukuze katika kushuka kwake, na upanue mahali pake pa kuingia, na muoshe kwa maji na theluji na barafu, na mtakase kutokana na makosa kama inavyotakaswa nguo nyeupe kutokana na uchafu, na mbadilishie nyumba bora kuliko nyumba yake, na jamaa bora kuliko jamaa zake, na mke bora kuliko mke wake, na muingize Peponi, na mkinge mbali na adhabu ya kaburini, na adhabu ya Motoni (41).41 Kisha atatoa takbira, na atasimama baada yake kidogo, kisha atoe salamu moja tu upande wake wa kulia.
Mada ya Tatu: Zaka:
1- Maana ya Zaka na nafasi yake:
Zaka katika lugha: Ni kukua na kuongezeka.
Zaka kwa mujibu wa sheria: Ni haki ya wajibu katika mali maalumu kwa kundi maalumu.
Na ni Nguzo ya Tatu miongoni mwa nguzo za uislamu, nayo imefuatana na swala katika Qur'an katika sehemu themanini na mbili, kinachoonyesha ukuu wa daraja yake.
Amesema Mwenyezi Mungu Mtukufu:
﴿وَأَقِيمُواْ ٱلصَّلَوٰةَ وَءَاتُواْ ٱلزَّكَوٰةَ...﴾
"Na shikeni Swala na toeni Zaka..." [Al-Baqara: 43].
Na amesema rehema na amani ziwe juu yake: "Uislamu umejengwa juu ya nguzo tano: Kushuhudia kwamba hakuna apasaye kuabudiwa kwa haki ila Mwenyezi Mungu, na kwamba Muhammad ni Mtume wa Mwenyezi Mungu, na kusimamisha Swala, na kutoa Zaka, na kuhiji Nyumba Tukufu, na kufunga mwezi wa Ramadhani."42
Na wamekubaliana Waislamu wote kwamba ni faradhi, na juu ya ukafiri wa yeyote anayekanusha ulazima wake, Na kupigana na anayezuia kuitoa.
2- Masharti ya Ulazima wa Zaka:
(a)- Uhuru: Basi si wajibu juu ya mtumwa; kwa sababu hana mali, na kilicho mikononi mwake ni mali ya bwana wake; hivyo zaka ya mali hiyo huwa juu ya bwana wake.
(b) Uislamu: Si wajibu kwa kafiri; kwa kuwa ni ibada ya kujikurubisha kwa Mwenyezi Mungu na utiifu, na kafiri si miongoni mwa watu wa kujikurubisha kwa Mwenyezi Mungu na utiifu.
(c)- Kumiliki kiwango: Basi zaka haiwajibiki katika kilicho chini ya kiwango, nacho ni kiasi maalumu cha mali.
(d)- Ukamilifu wa umiliki: Kwamba mali iwe ina milikiwa na mtu kwa umiliki ulio kamilika na kamili; basi hakuna zaka katika mali ambayo umiliki wake haujathibiti, kama deni la mkataba.
(e)- Mali Kupitiwa mwaka: Kwa Hadithi marfu'u ya Aisha -radhi za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake-: "Hakuna zaka katika mali mpaka ipitiwe na mwaka"43.
3- Mali zinazowajibika kutolewa zaka:
Ya kwanza: Wanyama wa kufugwa,
Nao ni ngamia, ng'ombe, na mbuzi, na ni wajibu kutoa zaka katika hao kwa masharti mawili:
1- Ifugwe kwa ajili ya maziwa na uzazi, si kwa kazi.
2- Wawe ni wanyama wa malisho (yaani: wanaokula malishoni), basi si wajibu kutoa zaka juu ya wanyama wafugwao wanaolishwa kwa malisho aliyonunua kwa ajili yao, au aliyoyakusanya kutoka katika majani ya malishoni au mengineyo. Wala hakuna zaka kwa wanyama wanaochungwa malishoni baadhi ya sehemu ya mwaka, si mwaka wote wala zaidi ya mwaka.
4- Kiwango cha wanyama wafugwao:
1- Zaka ya ngamia:
Ikiwa masharti yatakamilika; itawajibika katika kila Ngamia watano Mbuzi mmoja, na katika Ngamia kumi Mbuzi wawili, na katika Ngamia kumi na tano Mbuzi watatu, na katika Ngamia ishirini Mbuzi wanne, kama ambavyo Sunna na makubaliano ya wanachuoni yame ashiria hilo. Na wakifikia Ngamia ishirini na tano, basi katika hao atatoa Bintu makhadhi; naye ni Ngamia aliyekamilisha mwaka mmoja na kuingia mwaka wa pili; ikiwa atamkosa basi atatoa Ibnu labuun: (Ndama wa Ngamia anayenyonyesha).
Ikiwa atafikisha Ngamia thelathini na sita atatoa Bint Labuun; naye ni Ngamia mwenye miaka miwili.
Na pindi idadi ya ngamia inapofikia arobaini na sita, hupasa kutolewa Hiqqah, nayo ni ngamia jike aliyeitimiza miaka mitatu.
Na wakifikia Ngamia Sitini na Moja, basi atatoa Jadh'ah moja; naye ni Ngamia mwenye miaka minne.
Na wakifikia Ngamia Sabini na sita, atatoa Bint Labuuni wawili.
Ikiwa Ngamia watafikia Tisini na moja; basi atatoa Zaka Hiqqah mbili.
Ikiwa idadi ya Ngamia itazidi mia moja na ishirini kwa mmoja, basi atatoa Bint labuuni watatu, kisha fungu litabakia katika kila idadi ya Ngamia Arobaini atatoa Zaka ya Bint labuun mmoja, na katika kila Ngamia hamsini atatoa Hiqqah.
2- Zaka ya Ngo'mbe:
Zaka inawajibika humo ikiwa masharti yametimia, ikifikia Thelathini: Atatoa Tabii'iy au Tabii'at; (Ni ndama alieanza kufuatana na kundi machungani) na kila mmoja kati yao amekamilisha mwaka mmoja na kuingia mwaka wa pili.
Na wala hakuna zaka chini ya Ng'ombe thelathini.
Basi ikifikia Arobaini; itawajibika kutoa Musinnah; naye ni ng'ombe mwenye miaka miwili.
Ikiwa idadi ya Ngo'mbe itazidi Arobaini; basi itawajibika katika kila thelathini atatoa Tabii'iy; au Tabii'at, na katika kila Arobaini atatoa Musinnat.
3- Zaka ya Mbuzi:
Idadi ya kondoo na mbuzi ikifikia arobaini, iwe ni kondoo au mbuzi, basi atatoa Zaka ya Mbuzi mmoja; ambaye ni Jadha'a (Mbuzi wa miezi saba au nane) ya kondoo, au mbuzi jike.
Na Mbuzi hawatolewi Zaka ikiwa idadi yao ni chini ya Arobaini. Na ikifikia jumla ya Mbuzi mia moja na Ishirini na moja, basi atatoa Mbuzi wawili. Basi ikifikia mia mbili na moja; atatoa Mbuzi watatu.
Kisha fungu litabakia baada ya kiwango hiki, basi katika kila mia moja hutolewa Mbuzi mmoja; hivyo katika mia nne atatoa Mbuzi wanne, na kadhalika.
Pili: Zaka ya chenye kutoka Ardhini.
Kitokacho ardhini kina aina mbili:
1- Nafaka na matunda.
2- Madini.
Aina ya kwanza: Nafaka na matunda:
Na Zaka ni wajibu katika nafaka; kama: nNano, shayiri, na mchele. Na miongoni mwa matunda; kama vile: Tende na zabibu kavu, Wala si wajibu katika yasiyokuwa hayo miongoni mwa mimea; kama vile mikunde na mbogamboga.
Masharti ya ulazima wa Zaka katika nafaka na matunda:
1- Iwe ya kuhifadhiwa: Hakuna Zaka katika vile visivyohifadhiwa kama matunda na mboga mboga.
2- Iwe inapimika kwa vibaba: Hakuna Zaka katika vile vinavyouzwa kwa kuhesabu au kwa uzani; kama tikiti maji, vitunguu, komamanga, na vinginevyo.
3- Kufikia kiwango: Nacho ni wasqi tano (maana yake itakuja mbeleni), basi hakuna zaka kwa kilicho chini ya hapo.
4- Mwenye kutoa zaka amiliki kiwango stahiki wakati wa uwajibu wa zaka.
Basi yeyote atakayemiliki mali hiyo baada ya wakati wa uwajibu wa Zaka, si wajibu juu yake kutoa Zaka, kama vile akinunua au akapewa zawadi baada ya mavuno.
Wakati wa Ulazima wa kutolewa Zaka:
Zaka ni wajibu katika nafaka na matunda yanapoanza kukomaa na kuiva. Na alama ya kudhihiri kuiva au kukomaa ni kama ifuatavyo:
a- Katika mbegu: Ikikomaa, ikawa ngumu, na ikawa thabiti.
b- Katika matunda ya mitende: Kwa kuwa mekundu au ya njano.
c- Katika zabibu: Ziwe laini na tamu.
Kiwango chake:
Kiwango cha nafaka na matunda: Ni Awsaq tano, Alwasq moja ni vibaba sitini. Hivyo kiwango cha chini ni vibaba mia tatu kwa kipimo cha vibaba vya Mtume, rehema na amani za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake, na kiasi chake kwa kilogramu ni takribani kilogramu 900.
Kiasi cha Zaka ya wajibu ndani yake:
Kilicho wajibu kutoa ni moja ya kumi ikiwa mitende na mazao yalinyweshelezwa maji bila gharama wala juhudi ya mkulima, kama vile kwa maji ya mvua na chemchemi.
Ni wajibu kutoa nusu ya moja ya kumi katika kile kilichonyeshelezwa kwa juhudi na gharama; kama vile kinachonyeshelezwa kwa maji yanayovutwa kutoka katika visima na mito kwa kutumia wanyama au mitambo ya kisasa.
Aina ya pili: Madini:
Miongoni mwa aina za vinavyotoka ardhini: Ni Madini, na hayo ni yale yanayotolewa kutoka ardhini yasiyokuwa katika aina yake; kama dhahabu, fedha, chuma na vito vya thamani.
Wakati wa Ulazima wa Zaka:
Akishaipata na kuimiliki; aitoe Zaka yake mara moja, kwa kuwa si sharti kusubiri kupita mwaka. Kiwango chake ni kile cha dhahabu na fedha, na hutolewa robo ya kumi ya thamani yake, 2.5%.
Tatu: Zaka ya dhahabu na fedha:
Vyombo vya malipo ni: Dhahabu, fedha, na pesa za karatasi, na Zaka yake ni wajibu. Na ushahidi ni kauli yake Allah Mtukufu:
﴿وَالَّذِينَ يَكْنِزُونَ الذَّهَبَ وَالْفِضَّةَ وَلَا يُنْفِقُونَهَا فِي سَبِيلِ اللَّهِ فَبَشِّرْهُمْ بِعَذَابٍ أَلِيمٍ 34﴾
"Na wanaokusanya dhahabu na fedha, wala hawazitumii katika Njia ya Mwenyezi Mungu, wabashirie khabari ya adhabu iliyo chungu." [At-Tauba: 34].
Na imekuja katika Hadithi: “Hakuna mwenye dhahabu wala fedha ambaye hazitolei Zaka yake isipokuwa Siku ya Kiyama atatandikiwa sahani za moto.”44
Wamekubaliana wanachuoni juu ya uwajibu wa Zaka katika dhahabu na fedha, na fedha za noti au sarafu zinachukua hukumu ya dhahabu na fedha kwa kuwa zimechukua nafasi ya dhahabu na fedha katika muamala wa fedha.
Kiwango cha Zaka katika vitu vya thamani (dhahabu na fedha), na kiwango cha wajibu ndani yake:
Kiwango cha pesa za karatasi ni kile cha dhahabu au fedha; kwa kuwa zimeingia katika hukumu ya dhahabu na fedha katika thamani, basi zikifikia kiwango cha mojawapo kati ya viwili hivyo, hutolewa Zaka. Na kwa kawaida, kiwango cha pesa za karatasi leo hukadiriwa kwa fedha; kwa sababu fedha ni nafuu kuliko dhahabu, hivyo hufikia kiwango chake kabla ya dhahabu. Hivyo, iwapo Muislamu atamiliki mali yenye thamani inayolingana na gramu mia tano tisini na tano (595) za fedha, na mwaka mmoja ukapita, basi mwenye nazo atalazimika kutoa zaka. Thamani ya gramu ya fedha hubadilika mara kwa mara; kwa hiyo yeyote mwenye mali kidogo asiyefahamu kama imefikia kiwango cha chini au la, aulize wafanyabiashara wa fedha kuhusu thamani ya gramu ya fedha, kisha aizidishe kwa (595), na kiasi kitakachopatikana ndicho kiwango cha chini.
Faida: Anapotaka kutoa Zaka ya mali yake; agawanye mali iliyofikia kiwango kwa arobaini, basi kitakachotoka ndicho kiwango cha wajibu.
Nne: Zaka ya Mali za biashara:
Ni bidhaa zinazoandaliwa kwa ajili ya kuuzwa na kununuliwa ili kuchuma na kupata faida, bidhaa za biashara zinajumuisha aina zote za mali zisizo za fedha; kama vile magari, nguo, vitambaa, chuma, mbao, na vinginevyo vilivyotayarishwa kwa ajili ya biashara.
Masharti ya wajibu wa Zaka ya Mali za biashara:
1. Aimiliki kwa matendo yake; kama vile uuzaji, na mkataba wa kukodisha, na mengineyo katika njia za kupata kipato.
2- Aimiliki kwa nia ya biashara; yaani akikusudia kujipatia mapato kwayo, kwani matendo huzingatiwa nia, na biashara ni tendo; hivyo ni lazima kuambatanisha nia kama ilivyo kwa matendo mengine.
3- Thamani yake ifikie kiwango ya mojawapo ya sarafu mbili: Dhahabu au Fedha.
4- Kukamilika kwa mwaka juu yake, yaani kupita kwa mwaka.
Jinsi ya kutoa Zaka ya mali ya Biashara:
Nikuwa bidhaa zilizoandaliwa kwa ajili ya biashara hutathminiwa mwishoni mwa mwaka kwa mojawapo ya sarafu mbili: Dhahabu au fedha, basi ikikadiriwa thamani yake na ikafikia kiwango kwa mojawapo kati ya dhahabu au fedha, atatoa robo ya kumi, 2.5%, ya thamani yake.
Tano: Zakatul Fitiri:
Nayo ni sadaka ya wajibu mwishoni mwa mwezi wa Ramadhani, na ilifaradhishwa katika mwaka wa pili wa Hijiria.
Hekima yake:
Zakatul fitiri ni lazima kwa kila Muislamu anayemiliki akiba ya ziada ya chakula siku ya iddil fitiri na usiku wake kinachomtosha yeye na watu wa nyumbani kwake. Na ni wajibu kwa kila Muislamu; wa kiume au wa kike, mdogo au mkubwa, huru au mtumwa, Kwa mujibu wa hadithi: "Alifaradhisha Mtume rehema na amani ziwe juu yake zakatul-fitiri kwa mtumwa na aliyehuru, na mwanaume na mwanamke, na mdogo na mkubwa katika waislamu."45 Maana ya neno (Faradhi) ni: Kulazimisha na kufanya kuwa lazima.
Hekima ya kuwekwa kuwa sheria:
Amesema bin Abbas, Mwenyezi Mungu awaridhie: "Alifaradhisha Mtume rehema na amani ziwe juu yake zakatul-fitiri; kuwa ni utakaso kwa mfungaji kutokana na maneno ya upuuzi na mambo ya uchafu, na ni chakula kwa masikini." 46
Wakati wa uwajibu wake na wakati wa kuitoa:
Zakatul-fitiri inakuwa ni lazima kwa kuzama kwa Jua usiku wa Idd. Inapendekezwa kuitoa siku ya Iddi kabla ya kwenda katika swala ya Iddi. Na wala haifai kuchelewesha kuitoa baada ya swala ya Iddi. Ikiwa ataichelewesha Zaka ya Fitri mpaka baada ya Swala ya Iddi; basi ni wajibu juu yake kuilipa, na atapata dhambi kwa kuichelewesha nje ya wakati uliowekwa.
Inafaa kuitoa kabla ya Iddi kwa siku moja au mbili.
Kiwango chake na kile kinachotolewa kwacho:
Kibaba cha chakula kilichozoeleka kwa watu wa mji; kama vile mchele, tende na ngano, au vinginevyo. Na kiwango cha kibaba kimoja ni takribani kilogramu tatu. Haifai kutoa thamani kwa kulipa pesa badala yake, kwa sababu ni kinyume na amri ya Mtume -rehema na amani ziwe juu yake-.
Kutoa Zaka na migawanyo ya Zaka:
Wakati wa kuitoa:
Lazima kutoa zaka haraka unapoingia wakati wa uwajibu wake. Na wala haifai kuchelewesha Zaka isipokuwa kwa dharura, kama vile mali kuwa katika nchi iliyo mbali naye wala hayupo mtu wa kumu wakilisha.
Mahali pa kuitoa:
Lililo bora ni kutoa Zaka katika mji iliyopo mali hiyo. Inaruhusiwa kuihamisha kutoka mji ambako iko na kuipeleka katika mji mwingine katika hali zifuatazo:
a- Ikiwa katika nchi hakuna muhitaji wa zaka.
b- Iwapo atapatikana ndugu wa karibu muhitaji katika nchi nyingine.
c- Ikiwa kutapatikana maslahi ya kisheria yanayohitaji kuihamisha zaka, kama vile: kuipeleka katika maeneo ya waislamu waliopatwa na majanga ya njaa na mafuriko.
Ni wajibu kutoa Zaka katika mali ya mtoto mdogo na mwendawazimu; haya ni kwa ujumla wa ushahidi mbalimbali, na ataitoa mlezi wao kwa niaba yao. Wala haifai kutoa zaka ila kwa nia. Kwa kauli ya Mtume -rehema na amani ziwe juu yake: "Hakika matendo yote huzingatiwa nia"47.
Wenye kupewa Zaka:
Makundi yanayopewa Zaka ni manane:
Kundi la kwanza: Mafukara:
Hao ndio wasiopata mahitaji yao ya msingi ya makazi, chakula na mavazi. Na kiwango wanachopewa kutoka katika zaka ni kile kinachowatosheleza wao na wanaowategemea kwa mwaka mmoja.
Kundi la pili: Masikini:
Nao ni wale wanaopata cha kuwatosheleza kwa kiasi kikubwa, lakini hawapati kwa ukamilifu wake; kama vile: mwenye mshahara, lakini haumtoshi kwa mwaka mzima.
Kiwango wanachopewa kutoka katika zaka: Ni kutosheleza mahitaji yao kikamilifu na mahitaji ya wale wanaowategemea kwa mwaka mzima.
Aina ya tatu: Wenye kuishughulikia Zaka:
Nao ni wale ambao kiongozi anawapa jukumu la kukusanya Zaka, au wanaotekeleza jukumu la kuilinda au kuifikisha kwa wahitaji.
Kiasi wanachopewa kutoka katika zaka: Ni kadiri ya malipo ya kazi wanazozifanya, ili mradi wasiwe na malipo au mshahara kutoka serikalini.
Aina ya nne: Wanaotiwa nyoyo zao mapenzi ya Uislamu:
Nao ni kila ambaye, kwa kumpa mali, kunatarajiwa: Kuingia kwake katika Uislamu, au kuimarika kwa imani yake, au kuzuia shari yake dhidi ya Waislamu.
Kiasi wanachopewa kutoka katika Zaka: Ni kiasi kitakachoweza kuwalainisha nyoyo zao.
Wa tano: Watumwa:
Na kinachokusudiwa ni: Kuwaachilia huru watumwa na walioingia mkataba wa kujikomboa.
Na aliyeandikishana: Ni mtumwa ambaye amenunua nafsi yake kutoka kwa bwana wake, Na pia ndani yake hujumuishwa kutoa fidia kwa ajili ya kuwatoa huru mateka wa waislamu katika vita.
Aina ya sita: Wadaiwa, nao wana aina mbili:
Wa kwanza: Aliye na deni kwa sababu ya haja binafsi, na wala hapati cha kulilipa deni lake. Na anapewa kiasi kinachotosheleza kulipa deni lake.
Wa pili: Aliye na deni kwa sababu ya kusuluhisha baina ya watu, na hupewa kiasi cha kulipa deni lake, hata akiwa tajiri.
Aina ya saba: Aliyeko kwenye njia ya Mwenyezi Mungu:
Nao ni wale wanaopigana Jihadi katika njia ya Mwenyezi Mungu.
Kiasi wanachopewa kutoka katika zaka: Kile kina chowatosheleza katika jihadi kwa ajili ya Mwenyezi Mungu; kama kipando, silaha, chakula, na mfano wake.
Aina ya nane: Mpita njia:
Naye ni msafiri ambaye matumizi yake yamekwisha, au ameibiwa, na wala hakubakiwa na chochote katika mali yake kitakachomfikisha anapoishi.
Kiasi wanachopewa kutoka katika zaka: Ni kiasi kinachowafikisha hadi mji wao, hata kama ni matajiri huko.
Mjadala wa Nne: Swaumu:
Kufunga ni:
Kumuabudu Mwenyezi Mungu Mtukufu kwa kujizuilia na vitu vyote vyenye kufunguza, kuanzia kuchomoza kwa Alfajiri hadi kutua kwa jua.
Nayo ni nguzo katika nguzo za Uislamu, na ni faradhi miongoni mwa faradhi za Mwenyezi Mungu Aliyetukuka, yanayojulikana katika Dini kwa dharura. Na ushahidi unaothibitisha ulazima wake ni Qur'ani, Sunna na makubaliano ya Waislamu.
Amesema Mwenyezi Mungu Mtukufu:
﴿شَهۡرُ رَمَضَانَ ٱلَّذِيٓ أُنزِلَ فِيهِ ٱلۡقُرۡءَانُ هُدٗى لِّلنَّاسِ وَبَيِّنَٰتٖ مِّنَ ٱلۡهُدَىٰ وَٱلۡفُرۡقَانِۚ فَمَن شَهِدَ مِنكُمُ ٱلشَّهۡرَ فَلۡيَصُمۡهُ...﴾
"Mwezi wa Ramadhani ambao imeteremshwa humo Qur'ani kuwa ni uongofu kwa watu, na hoja zilizo wazi za uongofu na upambanuzi. Basi ataye kuwa mjini katika mwezi huu na afunge..." [Al Baqara: 185].
Masharti ya ulazima wa kufunga Mwezi mtukufu wa Ramadhani:
1- Uislamu; haikubaliki kwa kafiri.
2- Kubalehe; sio wajibu kwa mtoto mdogo, Inakubalika funga ya mtoto anayeweza kung'amua mambo, na kwake inakuwa ni funga ya sunna.
3- Akili; si wajibu kufunga kwa mwendawazimu, wala funga yake haikubaliki; kwa sababu ya kukosekana nia.
4- Uwezo wa kufunga, Basi si wajibu juu ya mgonjwa asiyeweza kuitekeleza, wala si wajibu kwa msafiri, na watazilipa pindi udhuru wao utakapoondoka: Ambao ni ugonjwa na safari. Sharti la usahihi wake kwa mwanamke ni: Kukatika kwa damu ya hedhi na nifasi.
Kunathibitika kuingia Mwezi wa Ramadhani kwa moja kati ya mambo mawili, nayo ni:
a- Kuuona mwandamo wa Mwezi wa Ramadhani, Kwa kauli yake Mtume, rehema na amani za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake: "Fungeni kwa kuonekana mwezi mwandamo, na fungueni kwa kuonekana mwezi mwandamo"48.
b- Ulazima wa kukamilisha mwezi wa Shaabani siku thelathini; na hilo ni ikiwa hakukuonekana mwandamo wa mwezi Ramadhani, au mawingu, au vumbi, au mfano wake yatakapoziba kuuona; kwa maneno yake Mtume - rehema na amani za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake: "Na ikiwa utafichikana kwenu, basi kamilisheni idadi ya siku za mwezi wa Shaabani siku thelathini."49.
Nia katika kufunga:
Swaumu kama ibada nyingine, haifai isipokuwa kwa nia. Na wakati wa ulazima wa nia katika swaumu ya wajibu unatofautiana na ule wa funga ya Sunnah, na ufafanuzi wa hilo ni kama ifuatavyo:
La kwanza: Swaumu ya wajibu; kama kufunga mwezi wa ramadhani, au kulipa deni, au nadhiri, ni lazima anuie kufunga usiku kabla ya kuchomoza kwa Alfajiri. Kwa kauli yake Mtume, rehema na amani za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake: "Yeyote atakayelala bila kunuia kufunga usiku, basi mtu huyo hana funga."50
Ya pili: Ni funga ya hiyari, na ni sahihi mtu kuweka nia ya funga hiyo wakati wa mchana, kwa sharti kwamba asiwe ametumia chochote kinachobatilisha funga baada ya kuchomoza Alfajiri.
Mambo yenye kuharibu Funga:
(1) Kujamiiana: Mtu atakapofanya tendo la ndoa basi funga yake itakuwa imebatilika, na ni wajibu juu yake kuilipa siku hiyo aliyofanya tendo la ndoa. Inamlazimu pamoja na kulipa kutoa kafara, nayo ni: Kumuacha huru mtumwa, ikiwa hatopata, itamlazimu afunge miezi miwili mfululizo, na asiyeweza kwa udhuru wa kisheria, basi itamlazimu kuwalisha masikini sitini; kwa kila masikini nusu kibaba cha chakula kinacholiwa katika mji huo.
La pili: Kushusha manii: kwa sababu ya kubusu, au kupapasa, au kujitoa manii, au kuendelea kutazama vyenye kusababisha matamanio, basi analazimika kulipa tu bila kafara; kwa sababu kafara ni mahususi kwa kujamiiana. Ama aliyelala, akipatwa na kushusha manii usingizini na yakamtoka manii, basi hakuna kinacho mlazimu; kwa sababu hilo si kwa hiari yake, hivyo atatakiwa kuoga kama vile anavyooga kwa ajili ya janaba.
Ya tatu: Kula na kunywa kwa kukusudia: Kwa maneno yake Mtukufu:
﴿وَكُلُواْ وَٱشۡرَبُواْ حَتَّىٰ يَتَبَيَّنَ لَكُمُ ٱلۡخَيۡطُ ٱلۡأَبۡيَضُ مِنَ ٱلۡخَيۡطِ ٱلۡأَسۡوَدِ مِنَ ٱلۡفَجۡرِۖ ثُمَّ أَتِمُّواْ ٱلصِّيَامَ إِلَى ٱلَّيۡلِ...﴾
"Na kuleni na kunyweni mpaka ubainike kwenu weupe wa Alfajiri katika weusi wa usiku. Kisha timizeni Saumu mpaka usiku..." [Al-Baqarah: 187].
Ama yule aliyesahau akala au kunywa; hatowajibika kufanya lolote; Kwa hadithi: "Atakayesahau haliyakuwa kafunga akala au akanywa, basi atimize swaumu yake, kwani Mwenyezi Mungu kamlisha na kamnywesha"51.
4- Kujitapisha kwa makusudi. Ama yule anaye shindwa na matapishi bila ya hiari yake, basi hayo hayaiathiri funga yake. Kwa maneno yake Mtume -rehema na amani ziwe juu yake: "Mwenye kutapika bila hiari yake, basi si lazima kufidia saumu. Na mwenye kujitapisha kwa makusudi, basi na alipe saumu ya siku hiyo."52
Tano: Kutoa damu kutoka mwilini; kwa njia ya kupiga chuku (hijama), au kutoa damu chafu, au kutoa damu kwa kutoa msaada ili kumsaidia mgonjwa; basi hufunguza kwa yote hayo. Ama kutoa damu kidogo kwa ajili ya vipimo; hili haliathiri funga. Na vivyo hivyo, kutokwa na damu bila ya hiari yake; kama vile kutokwa na damu puani, au damu zitokanazo kwenye jeraha, au kung'oa jino; basi hili haliathiri funga.
Wale wanaoruhusiwa kufungua katika Mwezi mtukufu wa Ramadhani:
Sehemu ya kwanza: Kuhusu wale wanaoruhusiwa kuvunja saumu, na wanawajibika kuzilipa, nao ni:
Wa kwanza: Mgonjwa aliye na maradhi yanayo tarajiwa kupona, anayepata madhara kwa kufunga au funga kwake inakuwa ni ngumu.
Wa pili: Msafiri; iwe amepata mashaka katika safari au hajapata mashaka.
Na ushahidi juu ya hayo mawili ni kauli ya Mwenyezi Mungu Mtukufu:
﴿...وَمَن كَانَ مَرِيضًا أَوۡ عَلَىٰ سَفَرٖ فَعِدَّةٞ مِّنۡ أَيَّامٍ أُخَرَ...﴾
"Na mwenye kuwa mgonjwa au safarini, basi atimize hisabu katika siku nyengine..." [Al Baqara: 185].
3- Mama mjamzito au mwanamke mwenye kunyonyesha, ikiwa funga kwao inakuwa ni ngumu, au ikawadhuru wawili hao au watoto wao kutokana na kufunga, na wawili hao wako katika hukumu ya mgonjwa, basi inajuzu kwao kufungua, lakini ni wajibu kwao wawili kulipa swaumu katika wakati mwingine.
Wa nne: Mwanamke mwenye hedhi na nifasi, na kufuturu ni wajibu juu yao wawili, na wala haifai swaumu yao, na ni juu yao kuzilipa katika siku zingine.
Sehemu ya pili: Wale wanaoruhusiwa kufuturu, na inawalazimu kutoa kafara bila ya kulipa saumu, nao ni:
Wa kwanza: Mgonjwa ambaye kupona kwake hakutarajiwi.
Wa pili: Mzee, mwenye umri mkubwa, asiyeweza kufunga.
Basi hawa hawafungi, na wanalisha chakula kwa kila siku ya mwezi wa Ramadhani masikini mmoja. Na ama akifikia mzee daraja la uzezeta, basi jukumu la kisheria humuondokea; atafuturu wala hakuna lolote juu yake.
Wakati wa kulipa na hukumu ya kuchelewesha kulipa:
Ni wajibu kulipa swaumu ya ramadhani katika kipindi kilicho baina yake na ramadhani ya pili. Na lililo bora zaidi ni kufanya haraka katika kulipa. Hairuhusiwi kuchelewesha kulipa mpaka baada ya Ramadhani ya pili. Imepokelewa kutoka kwa Aisha -radhi za Allah ziwe juu yake- amesema: "Nilikuwa nikidaiwa swaumu za Ramadhani, basi siwezi kuzilipa isipokuwa katika mwezi wa Shaaban, kwa kuwa nilikuwa nikimhudumia Mtume wa Allah -rehema na amani ziwe juu yake-."53
Na yeyote atakayechelewesha kulipa mpaka ikafika Ramadhani nyingine, mtu huyo ana hali za aina mbili:
1- Awe amechelewesha kwa udhuru wa kisheria, mfano aendelee kuugua mpaka akafikiwa na Ramadhani nyingine, basi mtu huyu analazimika kulipa tu.
2- Awe amechelewesha bila kuwa na udhuru wa kisheria, basi huyu anapata dhambi kwa kuchelewesha, na inamlazimu kutubu, kulipa, na kulisha masikini kwa kila siku.
Funga za Sunna kwa mwenye deni la funga ya faradhi:
Mwenye kudaiwa deni la funga ya Ramadhani, ni bora kufanya haraka kulipa kabla ya kufunga funga za sunna, lakini ikiwa funga za sunna muda wake ni mfinyu kama vile kufunga swaumu ya Arafa na Ashuura, basi atazifunga kabla ya kulipa deni la Ramadhani; kwa sababu deni wakati wake ni mpana. Ama funga ya Ashura na Arafa, hizo muda wake ni mfinyu, lakini asifunge siku sita za mwezi wa Shawwali isipokuwa baada ya kulipa deni la funga ya Ramadhani.
Yaliyo haramu kufunga:
1- Kufunga siku ya Idil Fitri na siku ya Idil Adh-ha; kwa kuwa kuna katazo juu yake.
2- Saumu ya siku za kutandaza nyama katika mwezi wa Dhil-Hija, isipokuwa kwa mwenye kujistarehesha (Mutamatti') na mwenye kuunganisha (Qaarin) katika Hija, ikiwa hakupata dhabihu, siku za Tashriq ni: siku ya kumi na moja, ya kumi na mbili, na ya kumi na tatu katika mwezi wa Dhil-Hija.
3- Siku ya shaka kwa ajili ya shaka, nayo ni siku ya thelathini ya Shaabani, ikiwa usiku wake utakuwa usiku wenye mawingu au vumbi linaloziba kuuona mwandamo wa mwezi.
Yanayochukizwa kufunga:
a- Kutenga mwezi wa Rajabu kwa kufunga. b- Kuitenga siku ya Ijumaa kwa kufunga, kwa kuwa jambo hilo limekatazwa, ikiwa atafunga siku moja kabla yake au baada yake, basi chukizo litaondoka.
Funga za Sunna:
a- Siku sita za mwezi wa Shawwal. b- Kufunga siku tisa (za mwanzo za Dhul-Hija), na iliyosisitizwa zaidi ni siku ya Arafa; isipokuwa kwa mwenye kuhiji, si sunna kwake kuifunga. Na kufunga siku ya Arafa hufuta madhambi ya miaka miwili. Ya tatu: Kufunga siku tatu katika kila mwezi, na bora zaidi ayafanye kuwa katika masiku meupe, ambayo ni: siku ya tarehe kumi na tatu, kumi na nne, na kumi na tano, katika kalenda ya Hijiria. d- Kufunga siku ya juma tatu na Alhamisi kila wiki, kwa kuwa Mtume rehema na amani ziwe juu yake alikuwa akizifunga; kwa kuwa matendo ya waja huwasilishwa katika siku hizo mbili.
Funga za Kujikurubisha:
a- Funga ya Daudi amani iwe juu yake, alikuwa akifunga siku moja na anafungua siku moja.
b- Kufunga mwezi wa Allah Mtukufu wa Muharram, nao ndio mwezi bora zaidi unaosuniwa kufungwa, na uliotiliwa mkazo zaidi ni kufunga siku ya Ashuraa, nayo ni siku ya kumi ya Muharram, na afunge siku ya tisa pamoja nayo. Hili ni kwa kauli ya Mtume, rehema na amani ziwe juu yake: "Ikiwa nitabaki hai mpaka mwaka ujao basi nitafunga tarehe tisa."54 Na hufuta madhambi ya mwaka uliokuwa kabla yake.
Mjadala wa tano: Hijja na Umra.
Hija kwa lugha ya Kiarabu: Kusudio. Katika sheria ya Kiislamu: Ni kukusudia kwenda katika nyumba yake tukufu na maeneo ya ibada matukufu katika wakati maalumu kwa ajili ya kutekeleza ibada maalumu.
Na Umra: kilugha: Ni ziara.
Kisheria: Ni kuitembelea nyumba tukufu katika wakati wowote kwa ajili ya kutekeleza ibada maalumu.
Na Hija ni miongoni mwa nguzo za Uislamu, na miongoni mwa misingi yake mikubwa. Na ilifaradhishwa katika mwaka wa tisa wa Hijiria, na Mtume -rehema na amani ziwe juu yake- alihiji Hija moja tu; nayo ni (Hija ya kuaga).
Na ni wajibu kuhiji mara moja katika umri wa mtu kwa mwenye kuweza. Na chochote kilichozidi ni sunna. Ama Umra, basi ni wajibu kwa kauli ya wengi wa wanachuoni. Kwa dalili ya kauli ya Mtume rehema na amani ziwe juu yake alipoulizwa: "Je wanawake wanalazimika kufanya Jihadi?" Akasema: "Ndiyo, wanalazimika kufanya jihadi ambayo haina kupigana: Hija na Umra."55
Sharti za uwajibu wa Hijja na Umra:
1- Uislamu
2- Akili
3- Kupevuka
4- Uhuru.
5- Uwezo
Kwa mwanamke kuna sharti la sita la ziada; nalo ni uwepo wa mmoja wa maharimu wake wa kiume atakayesafiri pamoja naye kwa ajili ya kuitekeleza Hija, kwa sababu haruhusiwi kusafiri bila ya maharimu, si kwa ajili ya Hija wala kwa ajili ya kitu kingine chochote, kwa kauli yake Mtume, rehema na amani za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake: "Asisafiri mwanamke isipokuwa awe pamoja na maharimu wake, wala asiingie kwake mwanaume isipokuwa akiwa pamoja na maharimu wake."56
Maharimu wa mwanamke ni: Mume wake, au aliye haramu kwake kumuoa kwa uharamu wa milele; kwa nasaba; kama kaka yake, na baba yake, na ami yake, na mtoto wa kaka yake, na mjomba wake, au kwa sababu halali; kama kaka wa kunyonya, au kwa ukwe; kama mume wa mama yake na mwana wa mume wake.
Na kuwa na uwezo ni: Uwezo wa mali na wa mwili, kwamba aweze kupanda chombo cha usafiri na kuhimili safari, na anamiliki gharama za matumizi ya kutosha kwenda na kurudi, na pia anamiliki gharama za matumizi ya kutosha kwa watoto wake na wale ambao ame lazimishwa kuwagharamia matumizi yao hadi atakapo rudi kwao.
Na iwe kuna amani katika safari ya kwenda Makkah kwa nafsi yake na mali yake.
Na yule anayeweza kwa mali yake lakini si kwa mwili wake — kama vile mzee sana au mwenye maradhi endelevu yasiyotarajiwa kupona — lazima amteue mtu atakayehiji kwa niaba yake na kufanya Umra kwa niaba yake.
Inashurutishwa kwa yule anayesihi kufanya Hija na Umra kwa niaba masharti mawili:
1- Awe miongoni mwa wale ambao utekelezaji wa faradhi ya Hija unakuwa sahihi kwao; yaani awe Muislamu aliyebalehe mwenye akili timamu.
2- Awe amekwisha kuhiji kwa ajili ya nafsi yake Hija ya Uislamu.
Vituo vya kimahali vya kuhirimia:
Vituo vya kuhirimia: Na kwa lugha: Ni mpaka. Na kisheria: ni mahali pa ibada au wakati wake.
Kwa Hija zipo nyakati na sehemu za kuhirimia:
a- Nyakati za muda: Mwenyezi Mungu amezitaja kwa kauli yake Mtukufu:
﴿ٱلۡحَجُّ أَشۡهُرٞ مَّعۡلُومَٰتٞۚ فَمَن فَرَضَ فِيهِنَّ ٱلۡحَجَّ...﴾
"Hija ni miezi maalumu. Na anaye kusudia kufanya Hija katika miezi hiyo..." [Al Baqara: 197].
Na miezi hii ni: Shawwal, Dhul-Qa’dah, na siku kumi za Dhul-Hijjah.
b- Vituo vya mahali: Ni mipaka ambayo haijuzu kwa Hujaji kuivuka kuelekea Makka bila kuhirimia, Nayo ni kama ifuatavyo:
1- Dhul-Hulaifa: Ni kituo cha watu wa Madina.
Cha pili: Al-Juhfa, ambacho ni kituo cha watu wa Sham na Misri na Morocco.
3- Qarnul-Manaazil: Ambacho leo kinaitwa 'As-Sail'; kituo cha watu wa Najd.
4- Dhaatu Irqi: Ni kituo cha watu wa Iraq.
5- Yalamlam: Kituo cha watu wa Yemen.
Na yeyote ambaye makazi yake yapo ndani ya vituo hivi, basi atahirimia Hija na Umra kutokea nyumbani kwake. Na yeyote atakayekuwa miongoni mwa watu wa Makka, basi atahirimia kutokea Makka, wala hahitaji kutoka kwenda katika sehemu za kuhirimia (Miiqaat) ili kuhirimia. na ama kwa Umra, basi watatoka waende katika eneo la karibu zaidi nje ya eneo takatifu (al-hill), kisha wahirimie. Na mwenye kutaka kufanya Hija au Umra, basi ni lazima ahirimie kutoka katika vituo alivyoviweka Mtume, rehema na amani ziwe juu yake; navyo ni vituo za mahali vilivyotangulia kubainishwa. Kwa hivyo, haifai kwa mwenye kutaka kufanya Hija au Umra kuvipita bila ya kuhirimia.
Yeyote atakayepitia katika sehemu za kuhirimia (Miiqaat) zilizotajwa naye siyo mtu wa sehemu hizo, basi atahirimia hapo.
Yeyote atakayeelekea Makka, na akawa hapiti mojawapo ya miiqaat (vituo vya kuhirimia) vilivyotajwa kwa nchi kavu, baharini au angani; basi atahirimia (kunuia) atakapolingana na miiqaat iliyo karibu naye zaidi. Kwa kauli ya Omari bin Khattwab Mwenyezi Mungu amridhie: "Tazameni mkabala wake kutoka njia yenu."57.
- Yeyote ambaye safari yake ni kwa ajili ya kutekeleza ibada za Hija au Umra kwa njia ya ndege, basi ni wajibu kwake atie nia (ahirimie) ndege inapopita usawa wa Miqat iliyoko kwenye njia yake, na wala haruhusiwi kuchelewesha kuhirimia mpaka ndege itue uwanjani.
Kuhirimia:
Ni nia ya kuingia ndani ya ibada ya Hija au Umra; katika Hija: Ni nia ya kuingia katika Hija, Na katika Umra, ni nia ya kuingia ndani ya Umra. Hawi katika ihram isipokuwa akiweka nia ya kuingia katika ibada ya Hija au Umra. Ama kuvaa tu nguo za ihram bila kukusudia kuingia katika Ihramu, hakuhesabiwi kuwa Ihramu.
Mambo yanayopendekezwa katika Ihram:
1- Kuoga kabla ya kuhirimia kwa mwili mzima.
2- Mwanaume kujipaka manukato mwilini, si katika nguo za ihramu.
3- Kuingia kwake katika ihram akiwa amevaa kikoi na shuka nyeupe, na ndara mbili.
4- Afanye ihramu hali ya kuwa amepanda, akiwa anaelekea kibla.
Aina za Ibada:
Aliyehirimia ana hiari ya kuchagua atakalotaka miongoni mwa aina tatu za ibada za Hija, nazo ni:
1- Tamattui: Ni mtu kuhirimia Umra katika miezi ya Hija, na akaimaliza, kisha akahirimia Hija ndani ya mwaka wake huo huo.
2- Ifraad: Ni mtu kuhirimia Hija peke yake kutoka katika Miqaat, na atabaki katika ihiramu yake mpaka atakapotekeleza matendo ya Hija.
3- Qiraan: Ni mtu kuhirimia Hija na Umra kwa pamoja, au kuhirimia Umra kisha akaingiza Hija kabla hajaanza kutufu kwa ajili ya Umra. Hivyo atanuia Umra na Hija kuanzia Miqat, au kabla ya kuanza kutufu kwa ajili ya Umra, kisha atatufu kwa ajili ya hizo zote mbili na atafanya sa'ayi.
Na mwenye kujistarehesha (Mutamatti') na mwenye kuunganisha (Qaarin) wanawajibika kutoa fidia, ikiwa si miongoni mwa wakazi wa Msikiti Mtakatifu wa Makka.
Na iliyo bora zaidi kati ya aina hizi tatu za Hija ni Tamattui (Kujistarehesha); kwa sababu Mtume, rehema na amani ziwe juu yake, aliwaamrisha kwayo Maswahaba zake58. Kisha Qiraan (kuunganisha ibada mbili); kwa kuwa humo kuna Hija na Umra, kisha Ifraadi (kufanya ibada moja peke yake).
c- Basi anapohirimia kwa mojawapo ya ibada hizi, ataleta talbiya (Labbaika llaahumma) mara tu baada ya ihramu yake, kwa kusema: "Labbaika llaahumma labbaika. Labbaika laa shariika laka labbaika. Innalhamda wanni'imata laka walmulk laa shariika laka" Yani: Nimekuitika ewe Mwenyezi Mungu nimekuitikia! Nimekuitikia hauna mshirika nimekuitikia. Hakika sifa njema na neema na ufalme ni vyako nimekuitikia huna mshirika!59
Ni sunna, na inapendekezwa kuifanya kwa wingi; mwanamume aiseme kwa sauti, na wanawake waiseme kwa sauti ya chini.
Wakati wake: Huanza baada ya kuingia katika Ihramu, na mwisho wa wakati wake ni kama ifuatavyo:
Kwanza: Mwenye kufanya Umra ataikatisha Talbiya kabla hajaanza Tawafu.
Pili: Mwenye kuhiji ataikatisha talbiya anapoanza kurusha vijiwe kwenye Jamrat al-Aqaba siku ya Idi.
Makatazo ya Ihramu:
Katazo la kwanza: Kunyoa nywele au kuzipunguza au kuzing'oa kutoka sehemu yoyote ile ya mwili.
La pili: Kupunguza kucha au kuzikata kwenye miguu au mikono bila udhuru; ikivunjika kucha akaiondoa, basi hakuna fidia juu yake.
Katazo la tatu: Kufunika kichwa cha mwanaume kwa kitu kinachoshikamana nacho, kama vile kofia na kitambaa.
La nne: Mwanaume kuvaa nguo ya kawaida iliyo shonwa juu ya mwili wake au sehemu ya mwili wake, kama vile shati, kilemba, au suruali. Na nguo zilizo shonwa: Ni kile kilichotengenezwa kwa ukubwa wa kiungo, kama vile khufu mbili (soksi za ngozi laini), glovu, na soksi. Ama mwanamke, atavaa katika nguo atakazotaka wakati wa kuhirimia kwa kadiri ya haja yake ya kujisitiri, isipokuwa hatovaa barakoa, na atafunika uso wake kwa nguo nyinginezo kama mtandio wa kichwani au jilbabu atakapopita mbele yake wanaume wasio maharimu wake. Wala asivae glovu mikononi mwake.
Katazo la tano: Manukato; kwa sababu mwenye ihramu anatakiwa aepuke anasa na mapambo ya dunia na starehe zake, na aelekee Akhera.
Katazo la sita: Kuua viwindwa vya mwituni na kuviwinda. Hivyo, aliye katika Ihram asimuwinde mnyama pori, wala asisaidie katika kuwindwa kwake, wala asimchinje.
Ni haramu kwa aliye katika Ihram kula alichokiwinda, au kilichowindwa kwa ajili yake, au kile alichosaidia katika kuwindwa kwake; kwa sababu ni kama nyamafu kwake.
Ama mawindo ya baharini, si haramu kwa aliye katika Ihram kuyawinda. Wala si haramu kwake kuchinja mnyama wa kufugwa, kama kuku na wanyama wa mifugo; kwa sababu si windo.
Katazo la saba: Kufunga ndoa yeye mwenyewe au kumfungia mtu mwingine, au kuwa shahidi.
Katazo la nane: Kufanya tendo la ndoa. Basi ata kayejamiiana kabla ya kujivua katika Ihramu kwa kwanza, ibada yake itabatilika, na itamlazimu aendelee na akamilishe ibada yake, na atailipa mwaka utakaofuata, na itamlazimu kuchinja ngamia mmoja. Na ikiwa ilikuwa baada ya kujivua katika ihramu kwa mara ya kwanza, basi ibada yake haitobatilika, na anatakiwa kumwaga damu.
Na mwanamke katika hilo ni kama mwanaume ikiwa ni kwa hiari yake.
Katazo la tisa: Kumpapasa mwanamke katika sehemu zisizokuwa tupu; basi ni haramu kwa aliyehirimia kumpapasa mwanamke, kwa kuwa ni njia inayopelekea kufanya tendo la ndoa lililoharamishwa. Na makusudio ya kumpapasa ni: Kumgusa mwanamke kwa matamanio.
Umra:
(a) Nguzo za Umra:
1- Kuhirimia.
2- Kuzunguka Al-kaba
3- As-sa'ayu (kwenda baina ya Swafa na Marwa).
(b)- Yaliyo wajibu katika Umra
1- Kuhirimia kutoka kwenye Miqat iliyotambuliwa kisharia.
2- Kunyoa nywele za kichwa au kupunguza.
(c): Namna ya kufanya Umra:
Jambo la kwanza analoanza nalo mwenye kufanya Umra ni kufanya tawafu mizunguko saba, akiianza kwenye Jiwe Jeusi na kuimalizia hapo, Na awe katika tawafu yake akiwa na twahara, akiwa ameusitiri uchi wake kuanzia kitovu hadi magotini, Na ni sunna kwake kuvaa lubega katika Tawafu yote; nayo ni kufunua bega lake la kulia, na kuweka shuka yake chini ya bega lake la kulia, na kuweka ncha zake kwenye bega lake la kushoto. Anapokamilisha mzunguko wa saba, ataacha kuvaa lubega, na atafunika mabega yake kwa shuka lake.
Atalielekea Jiwe jeusi. Ikiwa ataweza kulibusu, atalibusu. Na ikiwa sivyo, ataligusa kwa mkono wake wa kulia kama hilo litawezekana, kisha aubusu mkono wake. Ikiwa haitakuwa rahisi kwake kuligusa Jiwe jeusi (Hajarul-Aswad), ataliashiria akiwa ameinua mkono wake wa kulia, akisema: “Allahu Akbar” mara moja, wala asiubusu mkono wake, wala asisimame. Kisha ataendelea katika tawafu yake; akiweka Al-Kaaba upande wake wa kushoto, na ni sunna kwenda kwa kasi katika mizunguko mitatu ya mwanzo. Kuharakisha: Ni kwenda mwendo wa haraka kwa hatua za karibu karibu.
Na akipita kwenye kona ya Yemeni - nayo ndiyo kona ya nne ya Al-Kaaba - ikiwezekana ataigusa kwa mkono wake wa kulia bila kusema: "Allaahu Akbar" “Mwenyezi Mungu ni Mkubwa” wala kuibusu. Na ikiwa itakuwa vigumu kwake kuigusa, ataiacha na kuendelea na tawafu yake, na asiiashirie wala asiseme: “Mwenyezi Mungu ni Mkubwa.” Atasema baina ya kona ya Yemen na Jiwe Jeusi:
﴿...رَبَّنَآ ءَاتِنَا فِي ٱلدُّنۡيَا حَسَنَةٗ وَفِي ٱلۡأٓخِرَةِ حَسَنَةٗ وَقِنَا عَذَابَ ٱلنَّارِ﴾
"Rabbanaa aatinaa fid-duniyaa Hasanatan wafil Aakhirati Hasanatan waqinaa adhaaban Naari" Yaani: Mola wetu Mlezi, tupe duniani mema, na Akhera mema, na utulinde na adhabu ya Moto! [Al-Baqara: 201].
Akimaliza tawafu, ataswali rakaa mbili nyuma ya Maqam Ibrahim ikiwa hilo litakuwa rahisi. Vinginevyo, ataswali rakaa mbili katika sehemu yoyote ya Msikiti Mtakatifu (Al-Haram). Na ni Sunna asome katika rakaa ya kwanza baada ya suratul-Fatiha suratul kaafiruuna, na katika rakaa ya pili, baada ya Al-Fatihah, atasoma suratul Ikhlaas, kisha ataelekea kwenye Mas'aa (Mahali pa Swafa na Marwa), na atafanya sa'yi kati ya Swafa na Marwa mizunguko saba; kwenda ni mzunguko mmoja, na kurudi ni mzunguko mwingine.
Ataanza sa'yi kwa Swafa, apande juu yake au asimame hapo karibu; kupanda juu yake ndiyo bora zaidi ikiwezekana. Na atasoma wakati huo kauli ya Mwenyezi Mungu Mtukufu:
﴿إِنَّ ٱلصَّفَا وَٱلۡمَرۡوَةَ مِن شَعَآئِرِ ٱللَّهِ...﴾
"Hakika vilima vya Swafaa na Marwa ni katika alama za Mwenyezi Mungu..." [Al-Baqarah: 158].
Na inapendekezwa kwamba aelekee Kibla, amsifu na kumtukuza Mwenyezi Mungu, aseme: "Laa ilaaha illa llaahu, wallaahu akbar. Laa ilaaha illa llaahu wahdahuu laa shariika lahuu, lahul-mulku walahul-hamdu, yuhyi wa yumiitu, wahuwa alaa kulli shay-in Qadiir. Laa ilaaha illa llaahu wahdahuu, anjaza wa'dahuu, wanaswara abdahuu, wa hazamal-ahzaaba wahdahuu."
Yaani: Hakuna mungu apasaye kuabudiwa kwa haki isipokuwa Mwenyezi Mungu, na Mwenyezi Mungu ni Mkubwa. Hakuna mungu apasaye kuabudiwa kwa haki isipokuwa Mwenyezi Mungu, Yeye pekee asiye na mshirika. Ufalme ni wake, na sifa njema ni zake. Yeye huhuisha na hufisha, naye ni Muweza wa kila kitu. Hakuna mungu apasaye kuabudiwa kwa haki isipokuwa Mwenyezi Mungu, Yeye pekee. Alitimiza ahadi yake, na akamnusuru mja wake, na akayashinda makundi ya maadui peke yake.60 Kisha ataomba awezacho huku ameinua juu mikono, na atairudia dhikri hii na dua hii mara tatu, Kisha atateremka, na atembee akienda Marwa, mpaka afikie alama (taa ya rangi ya kijani kibichi), na hapo mwanamume ataharakisha mwendo wa kutembea mpaka afikie kwenye alama ya pili. Ama mwanamke, yeye hajawekewa kuharakisha mwendo katika sheria kati ya alama mbili hizo, kwa sababu yeye ni uchi. Badala yake, inampasa kutembea katika sa'ayi yote. Kisha atatembea na kupanda Marwa au atasimama karibu nayo. Na kupanda juu yake ni bora ikiwa hilo litakuwa rahisi. Atasema na kufanya juu ya Marwa kama alivyosema na kufanya juu ya Swafa, isipokuwa kusoma aya ile, ambayo ni kauli ya Mwenyezi Mungu Mtukufu:
﴿إِنَّ ٱلصَّفَا وَٱلۡمَرۡوَةَ مِن شَعَآئِرِ ٱللَّهِ...﴾
"Hakika vilima vya Swafaa na Marwa ni katika alama za Mwenyezi Mungu..." Hilo limewekwa tu wakati wa kupanda juu ya Swafa katika mzunguko wa kwanza pekee, Kisha atashuka, atembee kwa miguu mahali pa kutembea, na aharakishe mwendo mahali pa kuharakisha, mpaka afikie Swafa. Atafanya hivyo mara saba, kwenda ni mzunguko mmoja na kurudi ni mzunguko mwingine. Inapendekezwa kwamba afanye dhikri na kuomba dua kwa wingi katika sa'yi yake awezavyo. Pia inapendekezwa kwamba awe safi kutokana na hadathi kubwa na ndogo. Hata hivyo, ikiwa ataifanya bila twahara, basi hilo litamtosheleza, vivyo hivyo, ikiwa mwanamke atapata hedhi au damu ya baada ya kuzaa baada ya tawafu, atafanya sa'ayi, na hiyo itamtosheleza; kwa sababu twahara si sharti katika sa'ayi, lakini ni jambo linalopendekezwa tu.
Anapomaliza Sa’yi, atanyoa nywele za kichwa chake au atazipunguza, na kwa mwanamume kuzinyoa ndiyo bora.
Na kufikia hapa atakuwa amekamilisha matendo ya Umra.
Hija:
A- Nguzo za Hija:
1- Kuhirimia.
2- Kusimama katika uwanja wa Arafa.
3- Twawafu (Mzunguko katika Alkaaba) wa kumalizia.
4- As-sa'ayu.
(b) Mambo yaliyo wajibu katika Hijja:
1- Kuhirimia katika vituo (Miqat).
2- Kusimama Arafa siku ya tisa ya Dhul-Hijja mpaka jua lizame kwa yule atakayesimama hapo mchana.
3- Kulala usiku huko Muzdalifa usiku wa siku ya kumi ya Dhul-Hijja mpaka nusu usiku.
4- Kulala Mina usiku katika siku za Tashriq.
5- Kutupa vijiwe kwenye Jamaraat.
6- Kunyoa nywele za kichwa au kupunguza.
7- Tawafu ya kuaga.
c-: Namna ya kufanya Hija:
Ni kwamba Muislamu atahirimia Hija anapofika miqat akiwa amefanya Hija pekee (Ifrad) ikiwa muda umebana; basi akifika Makka atazunguka Kaaba twawafu kisha atakwenda kutembea kati ya Swafa na Marwa (Sa'yi), na atabaki katika ihiramu yake mpaka aelekee Arafa siku ya Arafa, siku ya tisa, na atabaki hapo mpaka jua kuchwa.
Kisha ataondoka akitoa talbia kwenda Muzdalifa, na atakaa hapo mpaka aswali Alfajiri, kisha atabaki hapo akimtaja Mwenyezi Mungu na akitoa talbia na kuomba dua mpaka anga liwe la njano.
Mawingu yatakapokuwa ya njano, ataondoka kwenda Mina -kabla jua halijachomoza-; kisha atairushia Jamaratil Akaba kwa vijiwe saba, kisha atanyoa kichwa chake au atapunguza, na kunyoa ndiyo bora.
Kisha atafanya Tawaf al-Ifadhwa, na inamtosheleza sa'ayi ya kwanza; na kwa hilo Hija yake inakuwa imekamilika, na anakuwa ametoka kabisa katika ihram.
Na kinachobakia juu yake ni kutupa vijiwe katika siku ya kumi na moja na ya kumi na mbili, ikiwa ataharakisha kuondoka; basi atarusha vijiwe vile Jamarati tatu, kila moja ataitupia vijiwe saba, na atatoa takbira kwa kila kijiwe. Ataanza na ile ndogo iliyo karibu na Msikiti wa Khaif, kisha ile ya kati, kisha Jamaratul-Aqaba nayo ndiyo ya mwisho. Kila Jamara ataitupia vijiwe saba. Na akitaka kuchelewa baada ya siku ya kumi na mbili; atarusha vijiwe kwenye Jamarati tatu siku ya kumi na tatu kama alivyofanya katika siku ya kumi na mbili na siku ya kumi na moja.
Na wakati wa kurusha vijiwe ni baada ya jua kupita katikati ya mbingu katika siku tatu.
Na akitoka Mina katika siku ya kumi na mbili kabla ya jua kuzama, hapana ubaya. Na akisalia mpaka azipige vijiwe Jamarat siku ya kumi na tatu baada ya kupinduka jua, hilo ndilo bora, kama alivyosema Mwenyezi Mungu Mtukufu:
﴿...فَمَن تَعَجَّلَ فِي يَوۡمَيۡنِ فَلَآ إِثۡمَ عَلَيۡهِ وَمَن تَأَخَّرَ فَلَآ إِثۡمَ عَلَيۡهِۖ لِمَنِ ٱتَّقَىٰ...﴾
"...Lakini mwenye kufanya haraka katika siku mbili (akarejea) si dhambi juu yake; na mwenye kukawia pia si dhambi juu yake, kwa mwenye kumchamungu..."
[Al-baqara: 203]
Na akitaka kusafiri, atatufu tawafu ya kuaga mizunguko saba bila kufanya sa'i.
Na lililo bora zaidi kwa yule ambaye hana mnyama wa kuchinja (hadyi) ni kuhirimia Umra kwa njia ya kujistarehesha, kisha akahirimia Hija siku ya nane, na atende yale yaliyotangulia miongoni mwa matendo ya Hija. Na akihirimia Hija na Umra kwa pamoja, basi hakuna ubaya; hii inaitwa Qiraan, nayo ni kuhirimia Umra na Hija kwa pamoja kwa kutufu na kutembea Swafa na Marwa (saiyi) mara moja.
Sura ya tatu:
Masuala yanayohusiana na miamala
Wamebainisha wanachuoni, Mwenyezi Mungu awarehemu, elimu ya lazima ambayo ni wajibu kwa kila mtu mmoja mmoja kujifunza, na wakazungumzia kiasi ambacho ni wajibu binafsi kwa kila Muislamu kukijifunza, na miongoni mwa waliyoyataja: Kujifunza hukumu za mauzo kwa anayejishughulisha na biashara, Ili asije akatumbukia katika haramu au riba bila ya kujua, na imepokelewa kutoka kwa baadhi ya Maswahaba -radhi za Mwenyezi Mungu ziwe juu yao- kinacho thibitisha hilo.
Alisema Omar bin Khattwab -radhi za Allah ziwe juu yake-: "Asiuze sokoni kwetu isipokuwa yule aliyepata maarifa katika dini"61.
Na amesema Ally bin Abii Twaalib radhi za Allah ziwe juu yake: Atakayefanya biashara kabla ya kujifunza Fiqhi; atatumbukia katika riba, kisha atatumbukia, kisha atatumbukia. Yaani: Ataingia katika riba."62
Na amesema Ibn Abidiin akimnukuu Al-Alami: "Na imefaradhishwa juu ya kila mwenye kuwajibika, sawa awe mwanaume au mwanamke, baada ya kujifunza elimu ya dini na uongofu, kujifunza elimu ya udhu, kuoga, Swala, Saumu, na elimu ya Zaka kwa mwenye kumiliki kiwango, na Hija kwa yule ambaye imewajibika juu yake, na elimu ya mauzo kwa wafanyabiashara, ili wajiepushe na shubuha (utata) na machukizo katika miamala yote; na vivyo hivyo wenye fani mbalimbali, na kila anayeshughulika na jambo lolote, basi ni faradhi juu yake kuijua elimu yake na hukumu zake ili ajiepushe na haramu ndani yake"63.
Amesema Nawawi Mwenyezi Mungu amrehemu: "Na ama biashara na ndoa, na yanayofanana navyo miongoni mwa mambo ambayo asili yake si wajibu, basi ni haramu kujiingiza humo ila baada ya kujua masharti yake."64
Hizi ni baadhi ya kanuni zinazohusiana na miamala ya mali, ambazo zimeletwa na sheria ya Kiislamu:
1- Uhalalishaji wa kila kilicho na masilahi halisi au yaliyo na uzani mkubwa; kama vile kuuza na kununua vitu vilivyo halali, kukodisha, na shuf'aa65.
2- Uhalali wa kila chenye kudhamini haki za watu na kuzihifadhi; kama rehani na ushahidi.
3- Uhalali wa kila kilicho na masilahi kwa pande mbili za mkataba; kama vile kufuta muamala kwa kuridhiana, hiari, na masharti katika kuuza.
4- Uharamu wa kila kinachojumuisha kuwadhulumu watu, na kula mali zao kwa dhuluma; kama riba, uporaji kwa nguvu, na kuhodhi.
5- Uhalali wa kila jambo lenye kusaidiana katika kheri; kama mkopo, kuazimisha, na amana.
6- Kukataza kila kinachojumuisha kula mali bila kazi wala manufaa wala tabu; kama kamari na riba.
7- Kukataza kila muamala unaotawaliwa na kuto julikana na udanganyifu; kama vile mtu kuuza asicho kimiliki na kuuza kitu kisichojulikana.
8- Kuzuia kila kitu chenye hila ya kuhalalisha haramu; kama Biashara ya riba ya hila66.
9- Kuzuia yale yanayomshughulisha mbali na utiifu kwa Mwenyezi Mungu; kama vile kuuza na kununua baada ya adhana ya pili ya Ijumaa.
10- Kuzuia kila jambo lenye madhara, au linalos ababisha uadui baina ya Waislamu; kama vile uuzaji wa vitu vilivyoharamishwa, na mtu kuuza juu ya biashara ya mwenzie.
Na inapomtatiza Muislamu hukumu ya jambo miongoni mwa mambo, basi awaulize wanachuoni kuhusu hilo, wala asilifanye isipokuwa baada ya kujua hukumu ya kisharia kuhusu jambo hilo, kama alivyosema Allah Mtukufu:
﴿...فَاسْأَلُوا أَهْلَ الذِّكْرِ إِنْ كُنْتُمْ لَا تَعْلَمُونَ﴾
"Basi waulizeni wenye kujua kama nyinyi hamjui." [An-Nahl: 43].
Haya ndiyo tuliyoweza kuyakusanya, na Mwenyezi Mungu ndiye mwenye kuombwa aturuzuku elimu yenye manufaa na amali njema. Hakika Yeye ndiye Mpaji, Mkarimu. Na rehema na amani nyingi za Allah ziwe juu ya Mtume wetu Muhammad na ali zake na Maswahaba zake.
***
***
Imepokelewa na Imamu Ahmad katika Musnadi wake, kwa nambari (6072), na Tirmidhiy kwa nambari (1535), na Tirmidhiy akasema: Hadithi Hasan.
Ameitoa Bukhari katika Adabu Al-Mufrad kwa nambari 716, na Ahmad katika Al-Musnad kwa nambari 19606, na Adh-Dhiyaau Al-Maqdisiy katika Al-Ahaadiyth Al-Mukhtaarah 1/150, na ameisahihisha Albaani katika Sahih Al-Jaami'i Asswaghiir kwa nambari 3731.
Imepokelewa na Muslim, nambari (121), na Ahmad, nambari (10434).
(Madhii): Nayo ni maji meupe mepesi yenye utelezi hutoka wakati wa kuchezeana kimahaba, au kwa kukumbuka tendo la ndoa au kuikusudia, au kwa kutazama na kadhalika; hutoka kama matone, na huenda asihisi kutoka kwake. (Wadi): Nayo ni maji meupe mazito yanayotoka mara baada ya kukojoa, au wakati wa kubeba kitu kizito.
Ameitoa hadithi hii Muslim nambari 224.
Ameitoa Maalik katika Al-Muwattaa kwa nambari (680 na 219), na Daaramiy kwa nambari (312), na Abdurrazzaaq katika Muswannaf wake kwa nambari (1328), na ameisahihisha Albaniy katika Irwaai Al-Ghaliil kwa nambari (122).
Ameitoa Al-Nnasaai kwa nambari 12808, na Ahmad kwa nambari 15423, na ameisahihisha Albaniy katika Irwaai Al-Ghaliil kwa nambari 121.
Imepokelewa na Ibn Majah kwa nambari 594, na Ibn Hibbaan kwa nambari 799, na Al-Albani akaidhoofisha katika “Dhaifu Sunani At-Tirmidhiy” kwa nambari 146.
Imepokelewa na Bukhari, nambari (142), na Muslim, nambari (122).
Imepokelewa na Bukhari, nambari (7288), na Muslim, nambari (6066).
Alisema Samahatu Sheikh Abdul-Aziiz bin Baaz, rahimahullah, katika Majmuu’ Fatawa zake (juzuu ya 29/141): (Al-Baihaqiy ameongeza kwa sanad nzuri kutoka kwa Jabir, baada ya kauli yake: "Alladhii wa'attah" “Ile uliyomuahidi”: “Hakika Wewe huendi kinyume na ahadi”).
Imepokelewa na At-Tirmidhiy, nambari (2635).
Imepokelewa na Muslim, nambari (82).
Ameitoa Hadithi hii At-Tirmidhiy kwa nambari 265, na akasema: Hadithi hii ni nzuri, sahihi, na si ya kawaida (Hasanun Sahihun Ghariib), na ameisahihisha Albaani katika Sahihi At-Targhiib wat-Tarhiib.
Imepokelewa na Bukhari, nambari (1117).
Imepokelewa na Bukhari, nambari (6251), na Muslim, nambari (884).
Imepokelewa na Bukhari, nambari (756), na Muslim, nambari (872).
Imepokelewa na Bukhari, nambari (793), na Muslim, nambari (398).
Imepokelewa na Bukhari, nambari (812), na Muslim, nambari (490).
Imepokelewa na Muslim, nambari (498).
Imepokelewa na Bukhari, nambari (724), na Muslim, nambari (398).
Ameipokea Bukhari (797) na Muslim (402).
Imepokelewa na At-Tirmidhiy, nambari (839).
Imepokelewa na Bukhari, nambari (6008).
Imepokelewa na Bukhari, nambari (1110).
Imepokelewa na Bukhari, nambari (835).
Imepokelewa na Bukhari, nambari (743), na Muslim, nambari (399).
Imepokelewa na At-Tirmidhiy, nambari (266).
Imepokelewa na Muslim, nambari (588).
Imepokelewa na Abuu Daud, nambari (5168).
Imepokelewa na At-Tirmidhiy, nambari (284).
Imepokelewa na Muslim, nambari (1484).
Imepokelewa na Bukhari, nambari (609), na Muslim, nambari (602).
Imepokelewa na Bukhari, nambari (4130), na Muslim, nambari (842).
Imepokelewa na Muslim, nambari (865).
Imepokelewa na Bukhari, nambari (934), na Muslim, nambari (851).
Imepokelewa na Bukhari, nambari (1081), na Muslim, nambari (693).
Imepokelewa na Bukhari, nambari (1012), na Muslim, nambari (894).
Ameitoa Abuu Daudi kwa nambari (3201), na At-Tirmidhi kwa nambari (1024), na akasema: Hadith Hasan na Sahihi.
Imepokelewa na Muslim, nambari (962).
Imepokelewa na Bukhari, nambari (8), na Muslim, nambari (111).
Imepokelewa na Ibn Majah, nambari (1792), na At-Tirmidhi, nambari (63) na (631).
Imepokelewa na Bukhari, nambari (1402), na Muslim, nambari (2287).
Imepokelewa na Bukhari, nambari (1432), na Muslim, nambari (984).
Ameitoa Hadithi hii Abuu Daud kwa nambari (1609), na Ibnu Majjah kwa nambari (1827), na ameisahihisha Al-Albaani katika Sahihi Sunan Abi Daud kwa nambari (1609).
Imepokelewa na Bukhari, nambari (1), na Muslim, nambari (1907).
Imepokelewa na Bukhari, nambari (1810), na Muslim, nambari (1086).
Imepokelewa na Bukhari, nambari (1909).
Ameitoa Ahmad kwa nambari (26457), na Abuu Daud kwa nambari (2454), na An-Nasaai kwa nambari (2331), na tamko ni lake.
Imepokelewa na Bukhari, nambari (6669), na Muslim, nambari (2709).
Imepokelewa na Abu Daawuud, nambari (2380), na At-Tirmidhiy, nambari (719), na Ibn Maajah, nambari (676).
Imepokelewa na Bukhari, nambari (1849), na Muslim, nambari (1846).
Imepokelewa na Muslim, nambari (1134).
Imepokelewa na Ahmad 25198, An-Nasai 2627, na Ibn Majah 2901.
Imepokelewa na Bukhari, nambari (1862), na Muslim, nambari (1341).
Imepokelewa na Bukhari, nambari (1531).
Imepokelewa na Muslim, nambari (1211).
Imepokelewa na Bukhari, nambari (1549).
Imepokelewa na Muslim, nambari (1218).
Ameipokea Hadithi hii At-Tirmidhiy kwa nambari 487, na akasema: Hadithi hii ni nzuri Ghariibu (Hasanun Ghariib). Na Al-Albaani akasema kwamba ni hadithi Hasan.
Tazama: Mughni al-Muhtaj (2/22)
Haashiya ya Ibnu Aabidiin (1/42).
Tazama: Al-Majmu' (1/ 50).
Shuf'a: Ni haki ya mshirika ya kuitwaa sehemu ya mshirika mwenzake kutoka kwa yule aliyehamishiwa kwa mbadala wa mali.
Biashara ya riba ya hila: Ni mtu kumuuzia mwenzake kitu kwa bei ya mkopo, akamkabidhi, kisha baadaye akakinunua kilekile kabla ya kuipokea ile thamani aliyomuuzia kwa mkopo, kwa bei ndogo kuliko hiyo, kwa fedha taslimu.
Imepokelewa na Bukhari, nambari 8.