من خلق الكون؟ ومن خلقني؟ ولماذا؟ (سواحيلي)

كتاب "من خلق الكون؟ ومن خلقني، ولماذا؟" يناقش أصل وجود الكون والإنسان، مؤكدًا أن الكون لم يأتِ بالصدفة أو من العدم، بل له خالق عظيم هو الله، الذي وضع قوانين دقيقة تحكم الحياة والكون. يوضح الكتاب صفات الله وأهمية الإيمان بالرسل والكتب السماوية، ويؤكد أن الإسلام هو الدين الحق الذي جمع رسالات الأنبياء، داعيًا للإيمان به لتحقيق السعادة الحقيقية في الدنيا والآخرة.

  • earth Lugha
    (سواحيلي)
  • earth Mtunzi:
    اللجنة العلمية برئاسة الشؤون الدينية بالمسجد الحرام والمسجد النبوي
PHPWord

 

 

 

مَنْ خَلَقَ الكَونَ؟ وَمَنْ خَلَقَنِي؟ وَلِمَاذَا؟

 

 

Nani aliye umba Dunia? na ni nani aliye niumba mimi? na kwanini ameniumba?

 

 

اللَّجْنَةُ العِلْمِيَّةُ

بِرِئَاسَةِ الشُّؤُونِ الدِّينِيَّةِ بِالمَسْجِدِ الحَرَامِ وَالمَسْجِدِ النَّبَوِيِّ

 

Kamati ya Kielimu ya usimamizi wa mambo ya Dini ya Msikiti Mtukufu wa Makkah na Madinah

 


بِسْمِ اللهِ الرَّحمَنِ الرَّحِيمِ

Nani aliye umba Dunia? na ni nani aliye niumba mimi? na kwanini ameniumba?

Kamati ya kielimu kwa usimamizi wa mambo ya kidini kwa msikiti mtukufu wa Makka na Madina

Je mimi nipo katika njia sahihi?

Nani aliyeumba mbingu na ardhi na vilivyomo ndani yake miongoni mwa viumbe vikubwa ambavyo havijulikani ukubwa wake ni wa kiasi gani?

Ni nani aliyetengeneza mpangilio huu madhubuti ulio sawa katika mbingu na ardhi?

Ni nani aliyemuumba mwanadamu kisha akampa usikivu na kuona na akili na akamjalia uwezo wa kuwa na utambuzi na kufahamu uhakika wa mambo?

Ni nani aliyeumba utengenezaji huu madhubuti ndani ya viungo vya mwili wako, kisha akakupa sura na akaifanya nzuri sura yako?

Tafakari uumbaji wa viumbe hai pamoja na tofauti zake na aina zake.Ni nani aliye viumba kwa muonekano usio na mipaka?

Ni namna gani unapangika na kutulia ulimwengu huu mkubwa kwa kanuni zake ambazo zinaudhibiti kwa undani kwa miaka nenda rudi?

 

Ni nani aliyeweka mifumo inayoendesha Dunia hiii (Uhai na kifo, kuzaana kwa viumbe hai, usiku na mchana, na kubadilika kwa misimu, na vinginevyo)?

Je Dunia hii ilijiumba yenyewe? au imezuka baada ya kutokuwepo?au imekuwepo kwa kuzuka? Amesema Mwenyezi Mungu Mtukufu:

﴿أَمۡ خُلِقُواْ مِنۡ غَيۡرِ شَيۡءٍ أَمۡ هُمُ ٱلۡخَٰلِقُونَ٣٥ أَمۡ خَلَقُواْ ٱلسَّمَٰوَٰتِ وَٱلۡأَرۡضَۚ بَل لَّا يُوقِنُونَ 36

"Au wameumbwa bila ya kutokana na chochote au wao wamejiumba (35)

Au wao ndio wameumba mbingu na ardhi, bali wao si wenye kuwa na yakini" [Surat Tuur: 35-36]

Kama hatuna uwezo wa kuziumba nafsi zetu na nakuwa ni muhali iwe tumetokana na kisichokuwepo, au ni kwa kuzuka basi ukweli usiokuwa na shaka ndani yake:Nikuwa Dunia hii lazima iwe na muumbaji mkuu mwenye uwezo, hivyo basi ni muhali iwe Dunia hii imejiumba yenyewe au imezuka!

Kwanini mwanadamu anaamini uwepo wa vitu asivyoviona? (kama kutambua, na akili, na roho, na hisia, na kupenda) inakuaje mwanadamu anapinga uwepo wa muumbaji wa Dunia hii kubwa na yeye anaona athari ya viumbe wake na uumbaji wake na huruma yake?!

 

Hakuna yeyote mwenye akili anayekubali kuambiwa: Hakika nyumba hii imejileta yenyewe bila kuwepo aliyeijenga au aambiwe: Hakika kukosekana ndio kitu kilichosababisha upatikanaji wa nyumba hii, inakuaje baadhi ya watu wamkubalie yule anayesema: Dunia hii kubwa imejileta bila ya muumbaji? vipi atakubali mwenye akili aambiwe: Mpangilio huu ulio madhubuti kwa ajili ya Dunia umezuka ghafla?

Yote haya yanatufikisha katika jibu moja, nalo ni kuwa Dunia hii ina mlezi mkubwa mwenye uwezo mwenye kuiendesha, na kuwa yeye ndiye peke yake anayestahiki kuabudiwa, na kila kitu kinachoabudiwa kinyume na yeye kukiabudu kitu hicho ni batili, na wala hakina haki ya kuabudiwa.

Mola Mlezi muumbaji Aliyetukuka

Kuna Mlezi muumbaji mmoja tu, na yeye ndiye mmiliki mpangiliaji wa mambo ya waja mtoaji wa riziki mwenye kuhuisha na kufisha, na ni Yeye aliyeumba ardhi na akaifanya kuwa dhalili, na akaijalia kuwa inafaa kwa viumbe wake, na ni yeye aliyeumba mbingu na vilivyo ndani yake miongoni mwa viumbe vyake vikubwa, na akalifanya jua na mwezi na mchana na usiku kwa mpangilio huu madhubuti unaojulisha juu ya ukubwa wake.

 

 

Na ni Yeye aliyeidhalilisha hewa kwetu sisi ambayo hakuna maisha bila ya hewa, na ni Yeye anayeteremsha juu yetu mvua na ametudhalilishia Bahari na Mito, na ni yeye anayetulisha na anatuhifadhi sisi tukiwa vichanga ndani ya matumbo ya mama zetu bila ya sisi kuwa na nguvu, na ni Yeye anayeipitisha damu ndani ya mishipa yetu kuanzia kuzaliwa kwetu mpaka kufa.

Huyu Mola Mlezi muumbaji mtoa riziki ndiye Mwenyezi Mungu Aliyetakasika na Kutukuka.

Amesema Mwenyezi Mungu Mtukufu:

﴿إِنَّ رَبَّكُمُ ٱللَّهُ ٱلَّذِي خَلَقَ ٱلسَّمَٰوَٰتِ وَٱلۡأَرۡضَ فِي سِتَّةِ أَيَّامٖ ثُمَّ ٱسۡتَوَىٰ عَلَى ٱلۡعَرۡشِۖ يُغۡشِي ٱلَّيۡلَ ٱلنَّهَارَ يَطۡلُبُهُۥ حَثِيثٗا وَٱلشَّمۡسَ وَٱلۡقَمَرَ وَٱلنُّجُومَ مُسَخَّرَٰتِۭ بِأَمۡرِهِۦٓۗ أَلَا لَهُ ٱلۡخَلۡقُ وَٱلۡأَمۡرُۗ تَبَارَكَ ٱللَّهُ رَبُّ ٱلۡعَٰلَمِينَ54

"Hakika Mola wenu ni Mwenyezi Mungu aliyeziumba mbingu na ardhi katika siku sita, kisha akatulizana juu ya kiti cha Enzi. Huufunika usiku kwa mchana ufuatao upesi upesi. Na ameliumba jua na mwezi na nyota zimetiishwa kwa amri yake. Eleweni vyema kuumba ni kwake na amri zote ni zake. Ametukuka Mwenyezi Mungu Mola wa walimwengu wote". [Al-Aaraf: 54].

Mwenyezi Mungu ndiye Mola Mlezi muumba wa kila kitu kilichopo ndani ya Dunia tukionacho na tusichokiona, na kila kisicho kuwa yeye Allah basi hicho ni kiumbe miongoni mwa viumbe vyake,

Na ni Yeye anayestahiki kuabudiwa peke yake, na asiabudiwe pamoja na yeye yeyote asiyekuwa yeye, hana mshirika katika umiliki wake au uumbaji wake au uendeshaji wake au ibada zake.

Lau tujalie mjadala uwepo wa mungu mwingine pamoja na Allah aliyetakasika na kutukuka Dunia ingeharibika: Kwa sababu haifai waungu wawili kuiendesha Dunia kwa wakati mmoja,amesema Allah Mtukufu:

﴿لَوۡ كَانَ فِيهِمَآ ءَالِهَةٌ إِلَّا ٱللَّهُ لَفَسَدَتَا...107

"Lau wangelikuwamo humo miungu wengine isipokuwa Mwenyezi Mungu basi bila ya shaka hizo mbingu na ardhi zingepatwa na uharibifu" [Al-Anbiyaai: 107].

Sifa za Mola Mlezi muumbaji

Mola Mlezi aliyetakasika anayo majina mazuri yasiyo na idadi, na ni mwenye sifa za juu nyingi tukufu ambazo zinajulisha juu ya ukamilifu wake, miongoni mwa majina yake: Muumbaji, na "Allah" na maana yake:

Mwenye Uungu mwenye kustahiki kuabudiwa peke yake asiye na mshirika, aliyehai na aliyesimama kwa dhati na mwenye kurehemu, na mwenye kutoa riziki, na mkarimu, Amesema Allah aliyetakasika ndani ya Qur'ani tukufu:

 

﴿ٱللَّهُ لَآ إِلَٰهَ إِلَّا هُوَ ٱلۡحَيُّ ٱلۡقَيُّومُۚ لَا تَأۡخُذُهُۥ سِنَةٞ وَلَا نَوۡمٞۚ لَّهُۥ مَا فِي ٱلسَّمَٰوَٰتِ وَمَا فِي ٱلۡأَرۡضِۗ مَن ذَا ٱلَّذِي يَشۡفَعُ عِندَهُۥٓ إِلَّا بِإِذۡنِهِۦۚ يَعۡلَمُ مَا بَيۡنَ أَيۡدِيهِمۡ وَمَا خَلۡفَهُمۡۖ وَلَا يُحِيطُونَ بِشَيۡءٖ مِّنۡ عِلۡمِهِۦٓ إِلَّا بِمَا شَآءَۚ وَسِعَ كُرۡسِيُّهُ ٱلسَّمَٰوَٰتِ وَٱلۡأَرۡضَۖ وَلَا يَـُٔودُهُۥ حِفۡظُهُمَاۚ وَهُوَ ٱلۡعَلِيُّ ٱلۡعَظِيمُ255

"Mwenyezi Mungu hapana mola ila Yeye aliyehai, msimamia mambo yote milele, kusinzia hakumshiki wala kulala, ni vyake pekee vyote viliomo mbinguni na ardhini, ni nani huyo awezaye kuombea mbele yake bila ya idhini yake, anayajua yaliyo mbele yao na yaliyo nyuma yao, wala wao hawajui chochote katika vilio katika ujuzi wake, ila kwa atakalo mwenyewe, kiti chake kimeenea mbingu na ardhi, wala kuvilinda hivyo hakumshindi. Na Yeye ndiye aliye juu, na ndiye Mkuu". [Suratul Baqara: 255].

Na amesema Mwenyezi Mungu Mtukufu:

﴿قُلۡ هُوَ ٱللَّهُ أَحَدٌ١ ٱللَّهُ ٱلصَّمَدُ ٢ لَمۡ يَلِدۡ وَلَمۡ يُولَدۡ ٣ وَلَمۡ يَكُن لَّهُۥ كُفُوًا أَحَدُۢ4

"Sema Yeye Mwenyezi Mungu Mmoja (1)

«Mwenyezi Mungu ambaye peke yake ndiye mwenye kukusudiwa kwa kila haja (2)

«Hakuzaa wala hakuzaliwa (3)

«Wala hakuna yoyote katika viumbe vyake mwenye kufanana naye hata mmoja". [Surat Al Ikhlaswi: 1-4].

Mola Mlezi mwenye kuabudiwa anasifika kwa sifa za ukamilifu.

Miongoni mwa sifa zake nikuwa yeye ni mwen ye uungu mwenye kuabudiwa, na kisichokuwa yeye basi ni kiumbe kinakalifishwa na kinapewa amri na kinatenzwa nguvu.

Miongoni mwa sifa zake ni kuwa yeye yuko hai na mwenye kusimamia mambo yote basi kila kilicho hai hapa duniani Allah ndiye aliyekipa uhai au amesababisha uwepo wake baada ya kutokuwepo, na yenye amesimamia uwepo wake na riziki zake na kinacho mtosheleza. Mola Mlezi yupo hai hafi na haiwezekani kwake kumalizika, msimamizi halali, na hapatwi na kusinzia wala kulala.

Miongoni mwa sifa zake nikuwa Yeye ni Mjuzi ambaye hakijifichi juu yake kitu ardhini wala mbinguni,

miongoni mwa sifa zake, Yeye ni Msikivu Mwenye kuona ambaye anasikia kila kitu, na anaona kila kiumbe, anatambua kila kinachotia wasi wasi nafsi

Na yale yanayofichwa na vifua, na wala hakuna chochote kinachofichikana kwake Mtukufu mbinguni wala ardhini.

 

Miongoni mwa sifa zake nikuwa Yeye ni Muweza asiyeshindwa na chochote na wala hakuna yeyote mwenye kuzuia matashi yake, anafanya anayoyataka na anazuia anayoyataka, na anatanguliza na anachelewesha na ni mwenye hekima ya juu zaidi.

Miongoni mwa sifa zake nikuwa, Yeye ni muumbaji mtoa riziki mwenye kuendesha mambo, aliyeumba viumbe na akavipangilia, na viumbe vipo katika mashiko yake na chini ya nguvu zake.

Miongoni mwa sifa zake nikuwa, Yeye ndiye anayemjibu aliye dhikika, na anamsaidia mwenye shida, na anamtatulia mwenye haja, na kila kiumbe kinapoingia kwenye tatizo au dhiki kinaelekea kwake kwa lazima.

Ibada haiwi isipokuwa kwa ajili ya Allah Mtukufu, basi yeye ndiye aliyekamilika anayestahiki ibada hiyo peke yake bila ya kuchanganywa na chochote, na kila kinachoabudiwa kinyume na yeye basi kinaabudiwa kwa batili, na kiabudiwa hicho kinamapungufu, na kinazungukwa na kifo na kumalizika.

Mwenyezi Mungu Mtukufu ametupa akili zenye kufahamu sehemu katika utukufu wake, na akapandikiza kwetu maumbile yenye kupenda heri, na kuchukia shari, Na akili zinatulia zinapoelekea kwa Mola Mlezi wa viumbe,

 

Na maumbile haya yanajulisha juu ya ukamilifu wake na kuwa yeye haiwezekani kwake kusifika kwa sifa zenye mapungufu Mtakasifu.

Haipasi kwa mwenye akili kumuabudu isipokuwa mkamilifu, vipi aabudu kiumbe chenye mapungufu mfano wake au dhalili kuliko yeye!

Mwenye kuabudiwa haiwezekani awe Mwanadamu au sanamu au mti au mnyama!

Mola Mlezi yupo juu ya mbingu zake, ameenea juu ya kiti chake cha enzi, ametengana na viumbe wake, hakuna chochote katika dhati yake kinachotokana na viumbe wake, na wala hakuna katika viumbe wake chochote kinachotokana na dhati yake, na wala haingii ndani wala hajibadili mwili katika chochote miongoni mwa viumbe vyake.

Mola Mlezi hana chochote chenye kufanana naye, naye ni msikivu mwenye kuona, na hana wa kulinganishwa naye, naye amejitosheleza kutohitajia kwa viumbe wake, halali wala hali chakula, naye ametakasika haiwezekani awe na mke au mtoto, muumba mwenye sifa tukufu na wala haiwezekani milele kusifika na sifa ya kuhitajia au ya upungufu.

Amesema Mwenyezi Mungu Mtukufu:

 

 

﴿يَٰٓأَيُّهَا ٱلنَّاسُ ضُرِبَ مَثَلٞ فَٱسۡتَمِعُواْ لَهُۥٓۚ إِنَّ ٱلَّذِينَ تَدۡعُونَ مِن دُونِ ٱللَّهِ لَن يَخۡلُقُواْ ذُبَابٗا وَلَوِ ٱجۡتَمَعُواْ لَهُۥۖ وَإِن يَسۡلُبۡهُمُ ٱلذُّبَابُ شَيۡـٔٗا لَّا يَسۡتَنقِذُوهُ مِنۡهُۚ ضَعُفَ ٱلطَّالِبُ وَٱلۡمَطۡلُوبُ ٧٣ مَا قَدَرُواْ ٱللَّهَ حَقَّ قَدۡرِهِۦٓۚ إِنَّ ٱللَّهَ لَقَوِيٌّ عَزِيزٌ74

"Enyi watu! Unapigwa mfano, basi usikilizeni. Hakika wale mnao waomba badala ya Mwenyezi Mungu, hawatoweza kuumba hata Nzi ijapokuwa watajumuika kwa hilo. Na Nzi akiwapokonya kitu hawawezi kukipata kwake. Amedhoofika kweli huyo mwenye kutaka na mwenye kutakwa" (73)

Hawa washirikina hawakumuheshimu Mwenyezi Mungu vile anavyostahiki kuheshimiwa, na hali Yeye ndiye mwenye nguvu aliyeumba kila kitu, ndiye mshindi asiyeshindwa". [Suratul-Hajj: 73-74].

Kwanini ametuumba huyu muumbaji Mtukufu? na ni kitu gani anahitaji kutoka kwetu?

Je akili inakubali kuwa Allah ameumba viumbe wote bila malengo, je ameviumba hivi hivi ilhali yeye ni mwenye hekima mjuzi?

Je akili inakubali kuwa yule aliyetuumba kwa mpangilio huu na umaridadi na akatudhalilishia viliomo mbinguni na ardhini, atuumbe bila malengo au atuache bila majibu yatokanayo na maswali muhimu ambayo yanayotushughulisha, mfano: Kwa nini tupo hapa?

Na nini kitakuwa baada ya kifo? na malengo ya kuumbwa kwetu ni yapi?

Na je akili inakubali kutokuwepo kwa adhabu kwa mtu dhalimu na malipo kwa wafanyao mema?

Amesema Mwenyezi Mungu Mtukufu:

﴿أَفَحَسِبۡتُمۡ أَنَّمَا خَلَقۡنَٰكُمۡ عَبَثٗا وَأَنَّكُمۡ إِلَيۡنَا لَا تُرۡجَعُونَ115

"Je! Mlidhani ya kwamba tulikuumbeni bure na ya kwamba nyinyi kwetu hamtarudishwa?" [Al-muuminina: 115].

Isipokuwa Allah alituma mitume ili tufahamu malengo ya uwepo wetu, na akatuongoza namna tumuabudu na tujikurubishe kwake, na nini anahitaji kwetu na vipi tupate radhi zake, na akatueleza mwisho wetu baada ya kifo?

Na Allah ametuma mitume ili watueleze kuwa yeye Allah peke yake ndiye mwenye kustahiki kuabudiwa, na ili tufahamu namna ya kumuabudu, na watufikishie maamrisho yake na makatazo yake, na watufundishe mambo mazuri ambayo tukiyachukua maisha yetu yatakuwa mazuri yaliyoenewa na heri na baraka.

Na hakika Allah aliwatuma mitume wengi mfano: (Nuhu, Ibrahim, Mussa, Issa) na akawapa alama na miujiza inayojulisha juu ya ukweli wao na kuwa wao wametumwa kutoka kwake yeye Allah Mtukufu, na wa mwisho wao ni Muhammadi- Rehema na amani ziwe juu.

Na hakika wametueleza mitume kwa uwazi kuwa maisha haya ni mtihani, na kuwa maisha halisi yatakuwa baada ya kifo.

Na huko kutakuwa na pepo kwa waumini waliomuabudu Allah peke yake asiye na mshirika na wakawaamini mitume wote, na kuna moto ambao Allah ameuandaa kwa ajili ya makafiri ambao waliabudu miungu mingine pamoja na Allah au walimpinga mtume yeyote miongoni mwa mitume wa Allah.

Amesema Mwenyezi Mungu Mtukufu:

﴿يَٰبَنِيٓ ءَادَمَ إِمَّا يَأۡتِيَنَّكُمۡ رُسُلٞ مِّنكُمۡ يَقُصُّونَ عَلَيۡكُمۡ ءَايَٰتِي فَمَنِ ٱتَّقَىٰ وَأَصۡلَحَ فَلَا خَوۡفٌ عَلَيۡهِمۡ وَلَا هُمۡ يَحۡزَنُونَ ٣٥ وَٱلَّذِينَ كَذَّبُواْ بِـَٔايَٰتِنَا وَٱسۡتَكۡبَرُواْ عَنۡهَآ أُوْلَٰٓئِكَ أَصۡحَٰبُ ٱلنَّارِۖ هُمۡ فِيهَا خَٰلِدُونَ36

"Enyi wanadamu! Pindi watakapokuja kwenu Mitume wangu, miongoni mwa watu wenu, wakiwasomea aya zangu, basi watakaojikinga na wanayokatazwa na wakafanya mema, hao hawatakuwa na hofu juu yao, wala hawatahuzunika (35)

Na wale waliozikanusha aya zetu na wakaacha kuzifuata kwa kujiona bora, hao ni watu wa Motoni wenye kukaa milele humo". [Al-Aaraf: 35-36].

Amesema Mwenyezi Mungu Mtukufu:

 

 

﴿يَٰٓأَيُّهَا ٱلنَّاسُ ٱعۡبُدُواْ رَبَّكُمُ ٱلَّذِي خَلَقَكُمۡ وَٱلَّذِينَ مِن قَبۡلِكُمۡ لَعَلَّكُمۡ تَتَّقُونَ ٢١ ٱلَّذِي جَعَلَ لَكُمُ ٱلۡأَرۡضَ فِرَٰشٗا وَٱلسَّمَآءَ بِنَآءٗ وَأَنزَلَ مِنَ ٱلسَّمَآءِ مَآءٗ فَأَخۡرَجَ بِهِۦ مِنَ ٱلثَّمَرَٰتِ رِزۡقٗا لَّكُمۡۖ فَلَا تَجۡعَلُواْ لِلَّهِ أَندَادٗا وَأَنتُمۡ تَعۡلَمُونَ ٢٢ وَإِن كُنتُمۡ فِي رَيۡبٖ مِّمَّا نَزَّلۡنَا عَلَىٰ عَبۡدِنَا فَأۡتُواْ بِسُورَةٖ مِّن مِّثۡلِهِۦ وَٱدۡعُواْ شُهَدَآءَكُم مِّن دُونِ ٱللَّهِ إِن كُنتُمۡ صَٰدِقِينَ ٢٣ فَإِن لَّمۡ تَفۡعَلُواْ وَلَن تَفۡعَلُواْ فَٱتَّقُواْ ٱلنَّارَ ٱلَّتِي وَقُودُهَا ٱلنَّاسُ وَٱلۡحِجَارَةُۖ أُعِدَّتۡ لِلۡكَٰفِرِينَ ٢٤ وَبَشِّرِ ٱلَّذِينَ ءَامَنُواْ وَعَمِلُواْ ٱلصَّٰلِحَٰتِ أَنَّ لَهُمۡ جَنَّٰتٖ تَجۡرِي مِن تَحۡتِهَا ٱلۡأَنۡهَٰرُۖ كُلَّمَا رُزِقُواْ مِنۡهَا مِن ثَمَرَةٖ رِّزۡقٗا قَالُواْ هَٰذَا ٱلَّذِي رُزِقۡنَا مِن قَبۡلُۖ وَأُتُواْ بِهِۦ مُتَشَٰبِهٗاۖ وَلَهُمۡ فِيهَآ أَزۡوَٰجٞ مُّطَهَّرَةٞۖ وَهُمۡ فِيهَا خَٰلِدُونَ25

"Enyi watu Muabuduni Mola wenu aliyekuumbeni, na akawaumba waliokuwa kabla yenu, ili muwe ni wenye kumcha Mwenyezi Mungu (21)

(Mwenyezi Mungu) aliyekufanyieni ardhi hii kuwa kama tandiko, na mbingu kama paa. Na akateremsha maji kutoka mbinguni, na akatoa kwa maji hayo mazao yawe riziki zenu. Basi msimfanyie Mwenyezi Mungu washirika, na hali nyinyi mnajua (22)

Na ikiwa mna shaka kwa hayo tuliyomteremshia mja wetu, basi leteni sura moja ya mfano wake, na muwaite mashahidi wenu badala ya Mwenyezi Mungu, ikiwa mnasema kweli (23)

Ikiwa hamuwezi sasa, na hamtaweza wakati unaokuja kabisa, basi uogopeni Moto ambao kuni zake ni watu na mawe, umeandaliwa kwa ajili ya makafiri (24)

Na wape bishara njema wale walioamini na wakafanya matendo mazuri watakuwa na Mabustani, ambayo inapita mito chini yake. Kila wanapopewa na Mwenyezi Mungu humo aina yoyote ya matunda yenye ladha, watasema, “Mwenyezi Mungu alituruzuku aina hii ya matunda kipindi cha nyuma, na watapewa wanayofanana, watakuwa na wake waliosafishika, na watakaa milele, hawafi humo wala hawatoki". [Suratul-Baqara: 21-25].

Kwanini Mitume walikuwa wengi?

Hakika Allah aliwatuma mitume wake kwenda kwa watu, hakuna umma isipokuwa Allah aliwapelekea mtume, ili awaite kwenye ibada ya Mola wao, na awafikishie maamrisho yake na makatazo yake, na yalikuwa malengo ya wito wao wote ni: kumuabudu Allah peke yake, na kila umma unapoanza kuacha au kuvuruga yale aliyokuja nayo mtume wao katika swala la kumpwekesha Allah, Allah anampa amri mtume mwingine asahihishe mwenendo wao, na awarejeshe watu kwenye maumbile yaliyosalimika kwa kumpwekesha Allah na kumtii,

 

mpaka akahitimisha Mwenyezi Mungu mitume kwa utume wa Mtume Muhammad-rehema na amani ziwe juu yake-, aliyekuja kwa dini iliyokamili na sheria itakayobakia milele kwa viumbe wote mpaka siku ya Kiyama.

Mtu hawezi kuwa muumini mpaka awaamini mitume wote

Mwenyezi Mungu ndiye aliyewatuma Mitume, na amewaamrisha watu wote kuwatii, na atakayepinga ujumbe wa yeyote miongoni mwao atakuwa amewapinga Mitume wote, hakuna dhambi kubwa kuliko mtu kumkanusha Allah na ufunuo wake, hivyo basi ili kuingia peponi ni lazima kuwaamini mitume wote.

Basi ni lazima juu ya kila mmoja katika zama hizi amuamini Allah na Mitume wote wa Allah, na aamini siku ya mwisho, na haitakuwa hivyo isipokuwa kwa kuamini na kumfuata wa mwisho wao Muhammad -rehema na amani ziwe juu yake-, aliyetiwa nguvu kwa muujiza uliobakia, nao ni Qur'ani Tukufu, ambayo Allah amedhamini kuihifadhi mpaka atakapoirithi ardhi na viliomo juu yake.

Allah ametaja ndani ya Qur'ani Tukufu kuwa atakayekataa kumuamini Mtume yeyote miongoni mwa Mitume wake atakuwa amemkufuru Mwenyezi Mungu na atakuwa ameupinga ufunuo wake, Mwenyezi Mungu Mtukufu amesema:

﴿إِنَّ ٱلَّذِينَ يَكۡفُرُونَ بِٱللَّهِ وَرُسُلِهِۦ وَيُرِيدُونَ أَن يُفَرِّقُواْ بَيۡنَ ٱللَّهِ وَرُسُلِهِۦ وَيَقُولُونَ نُؤۡمِنُ بِبَعۡضٖ وَنَكۡفُرُ بِبَعۡضٖ وَيُرِيدُونَ أَن يَتَّخِذُواْ بَيۡنَ ذَٰلِكَ سَبِيلًا١٥٠ أُوْلَٰٓئِكَ هُمُ ٱلۡكَٰفِرُونَ حَقّٗاۚ وَأَعۡتَدۡنَا لِلۡكَٰفِرِينَ عَذَابٗا مُّهِينٗا151

"Hakika wale wanaomkataa Mwenyezi Mungu na Mitume wake, na wanataka kufarikisha baina ya Mwenyezi Mungu na Mitume wake, kwa kusema: Wengine tunawaamini na wengine tunawakataa. Na wanataka kushika njia iliyo kati kati ya haya (150)

Hao ndio Makafiri kweli. Na tumewaandalia makafiri adhabu idhalilishayo". [Al-Nisaa: 150-151].

Kwa ajili hiyo sisi waislamu tunamuamini Allah na siku ya mwisho, kama alivyoamrisha Allah, na tunawaamini mitume na vitabu vilivyotangulia, amesema Allah Mtukufu:

﴿ءَامَنَ ٱلرَّسُولُ بِمَآ أُنزِلَ إِلَيۡهِ مِن رَّبِّهِۦ وَٱلۡمُؤۡمِنُونَۚ كُلٌّ ءَامَنَ بِٱللَّهِ وَمَلَٰٓئِكَتِهِۦ وَكُتُبِهِۦ وَرُسُلِهِۦ لَا نُفَرِّقُ بَيۡنَ أَحَدٖ مِّن رُّسُلِهِۦۚ وَقَالُواْ سَمِعۡنَا وَأَطَعۡنَاۖ غُفۡرَانَكَ رَبَّنَا وَإِلَيۡكَ ٱلۡمَصِيرُ285

"Mtume ameamini yaliyoteremshwa kwake kutoka kwa Mola wake, na Waislamu, (pia wameamini hivyo) wote wamemwamini Mwenyezi Mungu, na Malaika wake, na vitabu vyake,

Na mitume wake hatutofautishi baina ya yeyote katika Mitume wake, na husema tumesikia na tumetii (Tunakuomba msamaha Mola wetu na marejeo ni kwako" [Suratul-Baqara: 285].

Qur'ani Tukufu ni nini?

Qur'ani Tukufu ni maneno ya Allah Mtukufu na ufunuo wake aliouteremsha kwa Mtume wa mwisho Muhammad, nayo ni muujiza mkubwa unaojulisha ukweli wa utume wake -rehema na amani ziwe juu yake-, na Qur'ani Tukufu ndio haki katika sheria zake na ukweli katika habari zake,

Na Allah amewatahini wapingaji walete sura moja mfano wa Qur'ani wakashindwa hilo: Kwa uzito wa madhumuni yake na kuenea kwake kwa kila yanayofungamana na watu katika maisha ya dunia na akhera, na imefungamana na kila uhalisia wa kiimani ambao ni lazima kuuamini,

kama yalivyofungamana maamrisho na makatazo ambayo ni lazima mtu ayaendee kwa yale yaliyo kati yake na kati ya Mola wake au kati yake na nafsi yake, au kati yake na viumbe vingine, na yote hayo ni katika mpangilio mzuri katika fasihi na ubainifu,

na kwa hakika kitabu hiki kimesheheni dalili nyingi za kiakili na mambo halisi ya kisayansi yanayoonyesha kuwa kitabu hiki haiwezekani kuwa kimetengenezwa na mwanadamu bali ni maneno ya Mola wa viumbe aliyetakasika.

Uislamu ni nini?

Uislamu ni kujisalimisha kwa Allah Mtukufu kwa kumpwekesha, na kujinyenyekeza kwake kwa kumtii, na kutekeleza sheria zake kwa kuridhia na kukubali, na kupinga kila kinachoabudiwa kinyume na Allah.

Kwa hakika Allah amewatuma mitume kwa ujumbe mmoja nao ni: Kuwaita watu katika kumuabudu Allah peke yake asiye na mshirika, na kupinga kila kinachoabudiwa kinyume na Allah.

Na Uislamu ni dini ya manabii wote, lengo lao ni mmoja na sheria zao ni tofauti, na waislamu leo hii ni wapwekeshaji wenye kushikamana na Dini sahihi ambayo waliyokuja nayo manabii wote, na ujumbe wa uislamu katika zama hizi ni ukweli, nao ni ujumbe wa mwisho kutoka kwa muumba wa viumbe,

Mola mlezi ndiye aliyemtuma Ibrahim na Mussa na Issa amani iwe juu yao na yeye ndiye aliyemtuma mtume wa mwisho Muhammad -rehema na amani ziwe juu yake-, na ilikuja sheria ya kiislamu kufuta sheria zilizokuwa kabla ya sheria ya Uislamu.

Hakika kila dini ambazo watu wanaabudu kupitia dini hizo leo hii -kinyume na Uislamu-ni dini zilizotengenezwa na viumbe, au ni dini zilizokuwa na asili ya Uungu kisha zikachezewa na mkono wa viumbe

 

Zikawa zimechanganyikana na takataka za hovyo na simulizi za kale walizorithishana na jitihada za kibinaadamu.

Ama dini ya waislamu ni dini moja iliyo wazi haibadiliki, kama ilivyo ibada zao ambazo wanamuabudu Mwenyezi Mungu peke yake kupitia ibada hizo, wote wanasali sala tano, na wanatoa zaka za mali zao, na wanafunga mwezi wa ramadhani, na zingatia katiba yao nao ni Qur'ani Tukufu nacho ni kitabu kimoja katika miji yote, amesema Allah Mtukufu:

﴿...ٱلۡيَوۡمَ أَكۡمَلۡتُ لَكُمۡ دِينَكُمۡ وَأَتۡمَمۡتُ عَلَيۡكُمۡ نِعۡمَتِي وَرَضِيتُ لَكُمُ ٱلۡإِسۡلَٰمَ دِينٗاۚ فَمَنِ ٱضۡطُرَّ فِي مَخۡمَصَةٍ غَيۡرَ مُتَجَانِفٖ لِّإِثۡمٖ فَإِنَّ ٱللَّهَ غَفُورٞ رَّحِيمٞ 3

"Leo hii nimeikamilisha dini yenu na nimetimiza neema zangu juu yenu na nimeridhia Uislamu kuwa dini yenu na mwenye kushurutishwa na njaa bila ya kupendelea dhambi basi hakika Mwenyezi Mungu ni Msamehevu na Mwenye kurehemu" [Suratul Maidah: 3]

Amesema Mwenyezi Mungu Mtukufu katika Qur'ani Tukufu:

﴿قُلۡ ءَامَنَّا بِٱللَّهِ وَمَآ أُنزِلَ عَلَيۡنَا وَمَآ أُنزِلَ عَلَىٰٓ إِبۡرَٰهِيمَ وَإِسۡمَٰعِيلَ وَإِسۡحَٰقَ وَيَعۡقُوبَ وَٱلۡأَسۡبَاطِ وَمَآ أُوتِيَ مُوسَىٰ وَعِيسَىٰ وَٱلنَّبِيُّونَ مِن رَّبِّهِمۡ لَا نُفَرِّقُ بَيۡنَ أَحَدٖ مِّنۡهُمۡ وَنَحۡنُ لَهُۥ مُسۡلِمُونَ ٨٤ وَمَن يَبۡتَغِ غَيۡرَ ٱلۡإِسۡلَٰمِ دِينٗا فَلَن يُقۡبَلَ مِنۡهُ وَهُوَ فِي ٱلۡأٓخِرَةِ مِنَ ٱلۡخَٰسِرِينَ85

"Waambie tumemuamini Mwenyezi Mungu na tumeuamini wahyi Aliouteremsha kwetu na ule Aliouteremsha kwa Ibrāhīm na Ismā'il na Is’ḥāq na Ya'qūb na vizazi vyao, na wahyi aliopewa Mūsā naĪsā na Manabii kutoka kwa Mola wao hatubagui yeyote baina yao na sisi kwake Yeye Allah ni wenye kujisalimisha" (84)

"Na atakeyetaka dini isiyokuwa dini ya uislamu, basi haitokubaliwa kwake naye akhera atakuwa ni mwenye hasara kubwa". [Suratul-Imran: 84-85].

Dini ya Uislamu ni mfumo uliyoenea maisha yote, unaendana na maumbile na akili, na nyoyo zilizo sawa zinaukubali, Allah Mtukufu ameufanya kuwa sheria kwa ajili ya viumbe wake, nayo ni dini yenye heri na utukufu kwa watu wote katika dunia na akhera, na haibagui kati ya ukoo na ukoo mwingine, wala rangi na rangi nyingine na watu wote ni sawa, katika Uislamu hakuna yeyote aliye bora kuliko mwingine isipokuwa kwa kiwango cha matendo yake mema.

Amesema Mwenyezi Mungu Mtukufu:

﴿مَنۡ عَمِلَ صَٰلِحٗا مِّن ذَكَرٍ أَوۡ أُنثَىٰ وَهُوَ مُؤۡمِنٞ فَلَنُحۡيِيَنَّهُۥ حَيَوٰةٗ طَيِّبَةٗۖ وَلَنَجۡزِيَنَّهُمۡ أَجۡرَهُم بِأَحۡسَنِ مَا كَانُواْ يَعۡمَلُونَ97

"Mwenye kufanya mema, akiwa ni mwanamume au ni mwanamke, na huku ni mwenye kumuamini Mwenyezi Mungu na Mtume Wake, basi tutampa maisha mema yenye utulivu duniani hata kama ni mchache wa mali, na tutawalipa huko Akhera thawabu zao kwa uzuri zaidi ya walivyofanya duniani". [An Nahli: 97].

Uislamu ni njia ya kupata furaha na utukufu

Uislamu ni dini ya manabii wote, nayo ni dini ya Allah kwa watu wote, na siyo dini mahususi kwa waarabu.

Uislamu ni njia ya utukufu wa uhakika katika dunia, na neema ya kudumu siku ya mwisho.

Uislamu ndiyo dini pekee inayopokea mahitajio ya roho na mwili, na inatatua changamoto za kibinadamu, amesema Allah Mtukufu:

﴿قَالَ ٱهۡبِطَا مِنۡهَا جَمِيعَۢاۖ بَعۡضُكُمۡ لِبَعۡضٍ عَدُوّٞۖ فَإِمَّا يَأۡتِيَنَّكُم مِّنِّي هُدٗى فَمَنِ ٱتَّبَعَ هُدَايَ فَلَا يَضِلُّ وَلَا يَشۡقَىٰ 123 وَمَنۡ أَعۡرَضَ عَن ذِكۡرِي فَإِنَّ لَهُۥ مَعِيشَةٗ ضَنكٗا وَنَحۡشُرُهُۥ يَوۡمَ ٱلۡقِيَٰمَةِ أَعۡمَىٰ124

"Shukeni kutoka Peponi muende ardhini nyote pamoja, hali yakuwa nyinyi kwa nyinyi ni maadui. Mtakapojiwa na uongofu na maelekezo kutoka kwangu, basi mwenye kufuata uongofu wangu na maelekezo yangu na akayatumia yote mawili, basi atakuwa amefuata usawa duniani na ataongoka, na hatasumbuka huko Akhera kwa kuteswa na Mwenyezi Mungu (123)

Na atakaye jiepusha na mawaidha yangu, basi kwa yakini atapata maisha ya dhiki, na siku ya Kiyama tutamfufua hali ya kuwa kipofu".[Twaha: 123-124].

Ni kitu gani anachofaidika nacho muislamu katika Dunia na Akhera?

Uislamu unafaida kubwa, miongoni mwazo ni:

-Kufaulu na kupata utukufu duniani kwakuwa mtu ni mja wa Allah, na kama si hivyo angelikuwa ni mtumwa wa kufuata rai zake na shetani na matamanio ya nafsi.

-Kufaulu siku ya mwisho kwa kusamehewa na Allah, na kupata radhi zake, na Allah kumuingiza peponi kwa kupata ridhaa na neema za kudumu, na mtu kuokoka kutokana na adhabu ya moto.

Muumini siku Kiyama atakuwa pamoja na Manabii na waliosadiki na mashahidi na waja wema, uzuri ulioje wa urafiki huo, na asiye amini atakuwa pamoja na miungu inayoabudiwa kinyume na Allah na waovu wafanya makosa na wafanyao ufisadi.

Wale ambao Allah atawaingiza peponi wataishi ndani ya neema za milele bila kufa au kuugua au kuzeeka au maumivu au msongo wa mawazo au huzuni, na atatimiza matakwa yao kwa kila kitu wanacho kihitajia, na wale watakaoingia motoni watakuwa katika adhabu ya milele isiyokatika.

Ndani ya pepo kuna starehe ambazo jicho halijapata kuona, wala sikio kusikia, wala haijawahi kupita katika mawazo ya binadamu yeyote, na miongoni mwa ushahidi wa hayo ni kauli yake Allah Mtukufu:

﴿مَنۡ عَمِلَ صَٰلِحٗا مِّن ذَكَرٍ أَوۡ أُنثَىٰ وَهُوَ مُؤۡمِنٞ فَلَنُحۡيِيَنَّهُۥ حَيَوٰةٗ طَيِّبَةٗۖ وَلَنَجۡزِيَنَّهُمۡ أَجۡرَهُم بِأَحۡسَنِ مَا كَانُواْ يَعۡمَلُونَ97

"Mwenye kutenda mema, mwanamume au mwanamke, naye akawa ni Muumini, tutamhuisha maisha mema; na tutawapa ujira wao kwa malipo bora zaidi ya yale waliyo kuwa wakiyatenda".

[An Nahli: 97].

Na amesema Allah Mtukufu:

﴿فَلَا تَعۡلَمُ نَفۡسٞ مَّآ أُخۡفِيَ لَهُم مِّن قُرَّةِ أَعۡيُنٖ جَزَآءَۢ بِمَا كَانُواْ يَعۡمَلُونَ17

"Hakuna nafsi yoyote inayoyajua yale aliyowawekea Mwenyezi Mungu hawa Waumini ya kutuliza macho na kufurahisha moyo, yakiwa ni malipo yao kwa matendo yao mema". [Suratus-Sajda: 17].

Ni kitu gani anapata hasara asiyekuwa muislamu

Mtu atapata hasara kwa kukosa maarifa na elimu kubwa nayo ni maarifa na elimu ya kumtambua Mwenyezi Mungu, na atapata hasara kutokuwa na imani ambayo inamuwezesha mtu kuwa na amani na utulivu katika dunia na neema za kudumu akhera.

Mtu atapata hasara kwa kutoangalia kitabu kitukufu zaidi alichokiteremsha Allah kwa watu, na kutoamini kitabu hiki kitukufu.

Mtu atapata hasara kwa kutokuwa na imani na manabii wakubwa kama jinsi atakavyopata hasara kutokuwanao pamoja peponi siku ya Kiyama, na atakuwa ni rafiki wa karibu na mashetani na waovu na miungu inayoabudiwa kinyume na Allah ndani ya moto, ubaya ulioje wa nyumba ya moto na ubaya ulioje wa ujirani.

Amesema Mwenyezi Mungu Mtukufu:

﴿قُلۡ إِنَّ ٱلۡخَٰسِرِينَ ٱلَّذِينَ خَسِرُوٓاْ أَنفُسَهُمۡ وَأَهۡلِيهِمۡ يَوۡمَ ٱلۡقِيَٰمَةِۗ أَلَا ذَٰلِكَ هُوَ ٱلۡخُسۡرَانُ ٱلۡمُبِينُ 15 لَهُم مِّن فَوۡقِهِمۡ ظُلَلٞ مِّنَ ٱلنَّارِ وَمِن تَحۡتِهِمۡ ظُلَلٞۚ ذَٰلِكَ يُخَوِّفُ ٱللَّهُ بِهِۦ عِبَادَهُۥۚ يَٰعِبَادِ فَٱتَّقُونِ16

"Sema hakika waliopata hasara ni wale ambao walizipa hasara nafsi zao na watu wao siku ya Kiyama, tambueni huko ndiko kupata hasara kulikokuwa kukubwa (15)

Watakuwa na vivuli vya moto juu yao, na chini yao vivuli vya moto, hayo yote Allah anawahofisha waja wake, enyi waja wangu niogopeni". [Al-zumar: 15-16].

Anayetaka kufaulu Akhera basi ni juu yake awe muislamu mwenye kumtii Allah mwenye kumfuata Mtume wake rehema na amani ziwe juu yake.

Miongoni mwa mambo muhimu waliyokubaliana manabii na mitume amani iwe juu yao ni kwamba hakuna atakaye okoka siku ya Kiyama isipokuwa waislamu waliomuamini Allah Mtukufu na hawakumshirikisha na yeyote katika ibada zake, na wakaamini mitume wote na manabii, wafuasi wote wa wanaowaamini mitume na kuwasadikisha wataingia peponi, na wataokoka na moto.

Basi wale waliokuwa katika zama za nabii Mussa na wakamuamini na wakafuata mafundisho yake hao ni waislamu na ni waumini waja wema, lakini baada ya Allah kumtuma Issa ikawa ni lazima kwa wafuasi wa Mussa kumuamini Issa na kumfuata.

Basi aliyemuamni Issa hao ndio waislamu wema, na aliyekataa kumuamini Issa na akasema nitabaki katika dini ya Mussa huyu sio muumini, kwa kuwa amekataa kumuamini nabii aliyetumwa na Allah,

Kisha baada ya Allah kumtuma mtume wa mwisho ambaye ni Muhammad rehema na amani ziwe juu yake, ikawa ni lazima kwa watu wote kumuamini, Mola Mlezi ndiye aliyemtuma Mussa na Issa na ndiye yeye aliyemtuma mtume wa mwisho Muhammad, basi atakayepinga ujumbe wa Muhammad rehema na amani ziwe juu yake na akasema nitabaki katika kumfuata Mussa au Issa huyu siyo muumini.

Na haitoshi mtu kusema kuwa yeye anawaheshimu waislamu, na haitoshi kufaulu kwake siku ya mwisho kwa kutoa kwake sadaka na kusaidia masikini, lazima amuamini Allah na vitabu vyake na mitume wake na siku ya mwisho, ili Allah akubali matendo yake, hakuna dhambi kubwa kama kumshirikisha na kumpinga Allah na kukataa ufunuo aliouteremsha Allah au akakataa unabii wa mwisho wa manabii wake ambaye ni Muhammad rehema na amani ziwe juu yake.

Mayahudi na Wakristo ambao wamesikia kutumwa kwa Muhammad rehema na amani ziwe juu yake na wakakataa kumuamni na wakapinga dini ya Uislamu watakuwa ndani ya moto wa Jahannamu wataishi humo milele, na hii ndio hukumu ya Allah na sio hukumu ya yeyote miongoni mwa viumbe, amesema Allah Mtukufu:

﴿إِنَّ ٱلَّذِينَ كَفَرُواْ مِنۡ أَهۡلِ ٱلۡكِتَٰبِ وَٱلۡمُشۡرِكِينَ فِي نَارِ جَهَنَّمَ خَٰلِدِينَ فِيهَآۚ أُوْلَٰٓئِكَ هُمۡ شَرُّ ٱلۡبَرِيَّةِ6

"Hakika wale waliokufuru miongoni mwa Mayahudi na Wakristo na Washirikina, mateso yao ni Moto wa Jahanamu. Watakuwa ni wenye kukaa milele humo. Wao ndio viumbe waovu kabisa". [Al-Bayyina: 6].

Kwa kwakuwa umeteremka ujumbe wa mwisho kutoka kwa Allah kwenda kwa viumbe, basi nilazima juu ya kila mtu ausikilize Uislamu na ausikilize ujumbe wa nabii wa mwisho Muhammad -rehema na amani ziwe juu yake, amuamini na afuate sheria zake na amtii katika maamrisho yake na makatazo yake, kwa hivyo basi atakayesikia ujumbe huu wa mwisho kisha akaukataa, Allah hawezi kumkubalia chochote, na siku ya mwisho atamuadhibu.

Na dalili ya hilo ni kauli ya Allah Mtukufu:

﴿‌وَمَن يَبۡتَغِ غَيۡرَ ٱلۡإِسۡلَٰمِ دِينٗا فَلَن يُقۡبَلَ مِنۡهُ وَهُوَ فِي ٱلۡأٓخِرَةِ مِنَ ٱلۡخَٰسِرِينَ85

"Na atakeyetaka dini isiyokuwa dini ya Uislamu, basi haitokubaliwa kwake naye akhera atakuwa ni mwenye hasara kubwa". [Suratul-Imran: 85].

Na amesema Allah Mtukufu:

﴿قُلۡ يَٰٓأَهۡلَ ٱلۡكِتَٰبِ تَعَالَوۡاْ إِلَىٰ كَلِمَةٖ سَوَآءِۭ بَيۡنَنَا وَبَيۡنَكُمۡ أَلَّا نَعۡبُدَ إِلَّا ٱللَّهَ وَلَا نُشۡرِكَ بِهِۦ شَيۡـٔٗا وَلَا يَتَّخِذَ بَعۡضُنَا بَعۡضًا أَرۡبَابٗا مِّن دُونِ ٱللَّهِۚ فَإِن تَوَلَّوۡاْ فَقُولُواْ ٱشۡهَدُواْ بِأَنَّا مُسۡلِمُونَ64

"Sema enyi Mayahudi na Manaswara njooni katika neno la sawa baina yetu na nyie tusimuabudu isipokuwa Allah na wala tusimshirikishe na chochote na wala baadhi yetu wasiwafanye baadhi kuwa ni miungu kinyume na Allah kama mtaenda kinyume basi semeni shuhudieni ya kuwa sisi ni waislamu". [Suratu Al-Imran: 64].

Kipi kinachomlazimu Muislamu?

Kinachomlazimu Muislamu ni kuamini nguzo hizi sita:

Kumuamini Allah Mtukufu na kuwa yeye ni mumbaji mtoaji wa riziki muendeshaji wa mambo mwenye kumiliki.

Hakuna chochote mfano wake, hana mke wala mtoto, ni yeye pekee ndiye mwenye kustahiki kuabudiwa, na asiabudiwe yeyote pamoja na aitakidi kuwa ibada ya kila kinachoabudiwa kinyume na Allah ibada hiyo ni batili.

Kuamini Malaika kuwa wao ni waja wa Allah Mtukufu, Allah amewaumba kwa nuru, na akajalia miongoni mwa kazi zao ni kuteremsha ufunuo kwenda kwa manabii wake.

Kuamini vitabu vyote ambavyo vimeteremshwa na Allah kwa manabi wake (kama vile Taurati na Injili -kabla ya kupotoshwa kwake-) na kitabu cha mwisho ni Qur'ani Tukufu.

Kuamini Mitume wote kama vile Nuhu na Ibrahim na Mussa na Issa na wa mwisho wao ni Muhammad na wao ni viumbe, Allah aliwatia nguvu kwa kuwashushia ufunuo na akawapa miujiza na alama +ambazo zinajulisha juu ya ukweli wao.

Kuamini siku ya mwisho pale ambapo Allah atakapo wafufua wa mwanzo na wa mwisho na atahukumu baina viumbe wake na atawaingiza waumini peponi na kuwaingiza wapingaji motoni.

Kuamini makadirio na kuwa Allah anajua kila kitu kilichopita na kijacho mbeleni, na kuwa Allah alikwishajuwa na alikwisha andika hayo na alitaka hivyo, na ameumba kila kitu.

Na utamuabudu Allah kwa yale aliyo yawekea sheria kama Swala na Zaka na Swaumu, na kuhiji ikiwa utaweza kutekeleza hilo. kisha ni juu yake ajifundishe dini ambayo ndiyo msingi wa utukufu wake Duniani na kufaulu kwake Akhera.

 

 

***

Yaliyomo

Mola Mlezi muumbaji Aliyetukuka 4

Huyu Mola Mlezi muumbaji mtoa riziki ndiye Mwenyezi Mungu Aliyetakasika na Kutukuka. 5

Sifa za Mola Mlezi muumbaji 6

Mola Mlezi mwenye kuabudiwa anasifika kwa sifa za ukamilifu. 8

Kwanini ametuumba huyu muumbaji Mtukufu? na ni kitu gani anahitaji kutoka kwetu? 11

Kwanini Mitume walikuwa wengi? 15

Mtu hawezi kuwa muumini mpaka awaamini mitume wote 16

Qur'ani Tukufu ni nini? 18

Uislamu ni nini? 19

Uislamu ni njia ya kupata furaha na utukufu 22

Ni kitu gani anachofaidika nacho muislamu katika Dunia na Akhera? 23

Ni kitu gani anapata hasara asiyekuwa muislamu 25

Anayetaka kufaulu Akhera basi ni juu yake awe muislamu mwenye kumtii Allah mwenye kumfuata Mtume wake rehema na amani ziwe juu yake 26

Kipi kinachomlazimu Muislamu? 29